Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka

Kikwete naye atakuja na lake, kama atapita hapa ataishia kuwambia anaunda tume ya kuchunguza hili pia, Maana yule naye kwa tume mpaka singine tunazisahau kwa sababu simekuwa nyingi mno na nyingi ni tume za kinafiki tu

Na baadaye kutakuwa na tume ya kuchunguza haya yaliyochunguzwa na hiyo tume ya kwanza ya kuchunguza kamati ya ushauri ambayo ilikuwa inachunguza ushauri wa Thailand kusaidia Tanzania kutengeneza mvua ili kusaidia TRA iweze kuosha magari mengi inayoyashikilia bila sababu za msingi pale bandarini.
 
Kuna mambo mengi tunayoweza kujifunza hapa.

1. Kwanza angalia juhudi zilizofanywa na mhusika huyo ili biashara yake isiathirike.

2. Angalia ushirikiano alioupata kutoka katika ubalozi wa nchi yao.

3. Fikiria namna jinsi tunavyokabili matatizo. 'Always dismissive' Aaah, hili ni tatizo dogo, ngoja tutalishughulikia - kama alivyoonyesha huyo mtu wa TRA. Mwisho wake, hakuna lolote la maana lililofanyika. Hakutaka kulielewa tatizo hata wakati alipoelezwa kwa ufasaha kamili.

Ni namna hii ya utendaji kazi ndio inayowapeleka watendaji wengi katika mambo ya rushwa.

Huyu Mjapan wa Autorec angeweza kabisa kuchoka na mizunguko yote hii, na kutafuta njia za mkato kutatua shida - kutoa chochote.

4. Hata mahali tunapogundua kuwa hapana utendaji mzuri, hatuwachukulii hatua watu wanaohusika.

5. Jambo kama hili lingekuwa lilishaamuliwa siku nyingi ndani ya TRA, na utaratibu unaokubalika kuwekwa wazi kimaandishi, na sio maamuzi ya mtu mmoja tu kutoa hukumu siku kwa siku. Siku akiamka vibaya, basi magari yote yenye mikanda fulani ni haramu.

6. Wateja wote waliopatikana na mkasa huu na kulazimika kulipia hiyo 20%; nadhani jambo hili lingeweza kufikishwa mahakamani wangeweza kuwasaidia na wengine zaidi.

7. Mtiririko wa mawazo ya makala hiyo hapo juu ni mzuri na unajitosheleza kabisa kueleza tatizo lililopo au liliokuwepo.
 
Huyo customs commissioner ameonyesha udhaifu mkubwa kabisa ktk ufuatuliaji. Hapa ni sawa na kuvuliwa nguo mbele ya kadamnasi.
Yeye alipewa task ya kupata ukweli kwa kushauriwa awasiliane na wenyewe Japan, yeye akala kona mita chache akatinga DT Dobie.

Yaani hakuelewa kwamba hapo ni kama yard tu ya magari na hawana maelezo ya ndani ambayo technical na walitakiwe waulizwe wahusika wenyewe. Waajiriwa wenyewe hapo DT ni waswahili wenzetu, hayo mambo ya ndani ya manufacturer watajuaje?

Yaani hawa jamaa wa TRA wanafikiri watu kama wajapan wamefikia hatua kubwa ya maendeleo kwa kubangaiza kama ambavyo tumeuzoea hapa nyumbani.Nadhani wakisoma huo waraka utasaidia kujisahihisha katika utendaji wao.

Hii dunia ya sasa si lelemama kama wanavyoichukulia TRA
 
Nimekuwa nikiwaza sana.

Nadhani imefikia wakati tuishawishi serikali yetu ifufue kile kiwanda chetu cha magari cha nyumbu.

Hii itasaidia kwani pato la taifa litaongezeka kwani usafiri ni muhimu katika shughuli za kila siku.

Pia hii dhana iliyojengwa na TRA ya kutoamini magari ya Japan itakuwa imetafutiwa ufumbuzi wa kudumu hivyo kuwaondelea usumbufu na hasara wanayoipata wateja kutokana na penalties.

Vilevile itakuwa imekwamua wananchi wengi kwani tutaweza kupata magari kwa mkopo kama wanavyofanya wenzetu.
 
Mugi,

Hata hili watakuambia kuwa wanatafuta mtaalamu kutoka nje aje kuwapatia ushauri. Nchi hiyo ni kama imelaaniwa na huko TRA ndio hakuguswi kabisa.

Magazeti mengi yamejaribu kuandika haya mambo lakini habari zinaishia kwenye masikio mfu ya viongozi. Labda Kikwete atasoma hapa na kufanya kitu.

Thanks!

Sio nchi imelaaniwa, watu wake ndio walio laaniwa. Hawana wanachoweza kukifanya bila ya wataalam, sisi waungwana tunasema "once a slave always a slave". Kama ulivyo wewe ni mtumwa huko uliko au unabisha? unalipwa kitu kidogo kuliko hao unaofanya nao kazi, kwa nini? simpo, kwa kuwa wewe ni slave, modern slave.
 
Sio nchi imelaaniwa, watu wake ndio walio laaniwa. Hawana wanachoweza kukifanya bila ya wataalam, sisi waungwana tunasema "once a slave always a slave". Kama ulivyo wewe ni mtumwa huko uliko au unabisha? unalipwa kitu kidogo kuliko hao unaofanya nao kazi, kwa nini? simpo, kwa kuwa wewe ni slave, modern slave.

teh teh teh teh !!
 
Kama TRA wanacharge tax kwenye skuna unazomtumia mama watoto watashindwa ku over price na kutax gari.

What i don't understand ni how much wanazicharge zile RANGE ROVER za wazito dar? Double standard ndio matatizo yake
 
Huu ubabaishaji wetu yaani hata kusingizia utumwa hapana, maana mtumwa angalau atamjali mtumwa mwenzie kidogo maana wote wanapigika, lakini sisi tunanyanyasana, tunanyonyana, tunatukanana na kuibiana sisi kwa sisi, akija mgeni aah tunampa heshima na akileta gari sidhani kama atanyanyasika kama mwenyeji. Huyo Mjapani aliyezunguka kuwaona hao vigogo mnadhani angekuwa mwananchi hata kumsikiliza wangemsikiliza? Safari bado ndefu sana.
 
Naona kuondoa adha hii napendekeza iwekwe frat rate, sedan below cc2500 zilipiwe us$800, SUV below cc4500 us$1500, center fuso chesis za maroli na mabasi ziwe duty free.

Tukumbuke wamiliki magari wanalipa kodi kubwa sana kupitia mafuta, insurance, parking systems, sumatra na road licence.
 
Kwa nyongeza, mnaweza kupitia makala fulani hapa JF ambayo imejadili suala hili kwa undani sana. tulijaribu pia kulinganisha sera za TRA na zile za KRA katika uingizaji wa magai yaliyotumika.
Pitia kiungo hiki:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6475
 
Mlalahoi
Nimesoma michango yako ya topic hii. Kuna mahali umesema kuna mtu amekuambia PM Lowasa anaonekana kuwa na "akili" kuliko JK. Ninakuhakikishia the opposite is true. Wote ni mabomu, ila JK is far better kuliko huyo mmasai. Trust me. One of his major weaknesses is kukurupuka compounded with with uwezo mdogo wa kufikiri.
Ooops!

Wandugu hii hoja bado iko alive. Any comments so far? JamboForums magazine on its way. Make sure your post is among the 1st posts to be in the magazine.

Invisible
 
Ooops!

Wandugu hii hoja bado iko alive. Any comments so far? JamboForums magazine on its way. Make sure your post is among the 1st posts to be in the magazine.

Invisible

Mkuu,

Tanzania tunayoitaka bado hatujaipata hivyo tuachie hii tuendelee kuhangaika nayo, by the grace of GOD mayb tutaipata Tanzania tunayoitaka...
 
Kwa nyongeza, mnaweza kupitia makala fulani hapa JF ambayo imejadili suala hili kwa undani sana. tulijaribu pia kulinganisha sera za TRA na zile za KRA katika uingizaji wa magai yaliyotumika.
Pitia kiungo hiki:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6475


Hili suala pamoja na kujadiliwa huko nyuma halikupatiwa ufumbuzi.

Imebidi lifufuke upya maana malalamiko ameleta mjapan baada ya kuona wananchi wananyanyaswa na serikali machoni kwake wakikosa pa kukimbilia.

Hii haivumiliki tena.Inahitaji mapambano mbele kwa mbele kuanzia sasa.
 
Whats the point ya kuwapa tender hao wanaofanya Pre-shipment inspection kabla ya gari kusafirishwa?

Kama hamuawaamini kwanini watu walipie hizo inspection certificate halafu gari likifika Dar kama hicho cheti hakitambuliki?
 
Whats the point ya kuwapa tender hao wanaofanya Pre-shipment inspection kabla ya gari kusafirishwa?

Kama hamuawaamini kwanini watu walipie hizo inspection certificate halafu gari likifika Dar kama hicho cheti hakitambuliki?

Huu ni wizi nakukuza wigo wa rushwa , kuwanyanyasa wanao agiza gari zao na kuwakomoa kwa jina la sheria .
 
JOHN Nolan, yule raia wa Ireland aliyejaribu kuighilibu Serikali ya Tanzania imruhusu aanzishe mashamba ya kamba (prawns) ambayo yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kuliambia gazeti moja la Uingereza kwamba kati ya nchi za "ajabu" alizopata kuishi ni Tanzania .

Nolan aliliambia gazeti hilo ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na akaondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea!

Alitoa mfano wa yeye mwenyewe kwamba aliingia Tanzania akiwa hana kitu, lakini 'akatengeneza pesa' akiwa katika chumba chake cha hoteli kutokana na dili walizochonga na viongozi ambao walimwamini kwa kuwa tu ni Mzungu!

Lakini Nolan si mgeni pekee aliyepata kuikejeli Tanzania . Mwaka jana gazeti la Mtanzania lilipata kumnukuu mwekezaji mmoja kutoka China , anayefanya biashara ya kuuza kamba na kambakochi Mashariki ya Mbali, akiikejeli Tanzania kwamba rushwa yake ni "poa".

Kwa mujibu wa Mchina huyo, ni katika Tanzania tu ambapo unaweza kumwita hakimu nyumbani kwako na kumpa rushwa ya Sh. 100,000 tu, na kisha kumpa maelekezo ya namna ya kutoa hukumu ya kesi ya mamilioni ya pesa inayokuhusu!

Lakini kama utashangaa na kutoziamini kauli hizo za Nolan na za Mchina huyo, utasemaje kuhusu hii ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanzisha kampuni yake ya biashara (ANBEM) yeye na mkewe, mwaka 1999, akiwa bado Ikulu?. Kwa kufanya hivyo, Mkapa akawa Rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kufanya biashara akiwa Ikulu. Historia bwana, nani hapendi kuweka historia ya ujasiriamali?

Lakini hakuishia hapo. Mwaka mmoja kabla ya kuondoka madarakani; yaani Desemba 29, 2004, Mkapa huyo huyo akashirikiana na aliyekuwa Waziri wake wa Fedha na baadaye Nishati na Madini, Daniel Yona, kusajili kampuni nyingine binafsi iitwayo Tanpower Resources Company, na akaisimamia kununua asilimia 85 ya uliokuwa mradi wa umma wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

Lakini pia hakuishia hapo. Akautumia wadhifa wake wa urais kuhakikisha kampuni yake hiyo mpya – wakurugenzi wakiwa ni pamoja na mkewe na mtoto wake, kuingia mkataba wa kuiuzia Tanesco megawati 200 za umeme katika gridi ya taifa.

Raia wema waliohoji iwapo hakuna mgongano wa maslahi kwa Rais kufanya biashara akiwa bado Ikulu; huku akinunua kampuni ya umma (Kiwira) na kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni nyingine ya umma (Tanesco), walinyamazishwa haraka kwa kuambiwa Mkapa ni "mjasiriamali" , na kwamba anaonyesha "ujasiriamali" kwa vitendo akiwa Ikulu! Upo hapo?

Kama hiyo haitoshi kukuthibitishia vioja vya Tanzania , utaielezeaje hii ya Jeetu Patel kufanikiwa kughushi na kuchota Sh. bilioni 90 kutoka Benki Kuu kwa kutumia makampuni manane tofauti aliyoyasajili?

Ilikuja ya kwanza ikachota, ikaja ya pili ikachota, ikaja ya tatu ikachota, na vivyo hivyo mpaka kampuni ya nane! Na bado Watanzania tunatakiwa tuamini kwamba hakuna aliyejua kuwa hati zilizotumiwa na makampuni hayo ni za kughushi, hadi majuzi ripoti ya ukaguzi ya Ernest & Young ilipotua mezani kwa Rais Kikwete!

Lakini kama hilo halikushangazi au kukushtua, hebu tafakari na hili jingine: Watanzania masikini wanapandishiwa umeme kwa asilimia 21 kwa sababu Tanesco iko hoi kifedha. Kwa nini iko hoi? Kwa sababu vigogo serikalini wameiingiza katika mikataba mibovu ya Richmond , IPTL na Songas.

Kwa sababu ya mikataba hiyo mibovu, Tanesco inailipa IPTL Sh. bilioni 3.3 kila mwezi, Songas Sh. bilioni 5.8 na Richmond Sh.. bilioni 4.7. Kwa viwango hivvyo vya malipo, unahitaji kuwa na kampuni yenye utajiri wa Microsoft ya Bill Gates, kutotetereka kifedha. Na hivyo Tanesco ilitetereka. Ili isife, ikaamua kuongeza umeme kwa asilimia 21!

Hiyo maana yake ni nini? Hiyo maana yake ni kwamba Watanzania masikini na walalahoi wa nchi hii ndiyo "wanaobebeshwa" zigo hilo la Tanesco la kufidia gharama zilizosababishwa na vigogo serikalini za mikataba ya IPTL, Richmond na Songas. Cha kushangaza zaidi, vigogo hao waliotubebesha zigo hilo kwa kuingia mikataba hiyo mibovu, bado wanadunda mpaka leo serikalini!

Na bado wameona hiyo haitoshi. Sasa Serikali inajiandaa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuziruhusu kampuni binafsi kufanya biashara ya kuuza umeme nchini. Yaani; Serikali inakuwa mstari wa mbele kulitafutia shirika lake (Tanesco) wapinzani wa kuliua kibiashara, tena inafanya hivyo ikiwa yenyewe tayari imeshalikamua hadi kuwa hoi bin taaban!

Na Tanesco ikifa na biashara hiyo ikashikwa na makampuni binafsi ya nje, (ambayo bila shaka baadhi ya vigogo nchini watakuwa na hisa), nani atayazuia yasipange bei ya pamoja ya kuuzia umeme (cartel) ili yanufaike zaidi kwa kuwakamua zaidi Watanzania? Na bado tunaambiwa kuna vita inayoendelea nchini ya kuwakomboa masikini.

Biashara ya chakula ipo mikononi mwa watu binafsi, nishati nayo sasa inawekwa mikononi mwa watu binafsi, maji nayo yataelekea huko huko …mwishowe sekta zote nyeti zinazohusu usalama wa taifa zitakuwa mikononi mwa watu binafsi hususan wageni. Tusisahau Nyerere alitabiri: "Mtabinafsisha hata Magereza."

Lakini yawezekanaje mambo yote haya yatokee nchini na umma wa Watanzania ukae kimya tu? Jibu ni kwamba ni kwa sababu Tanzania ni nchi 'poa', nchi ya amani. Watanzania ni watu wasiotaka makuu, na ndiyo maana kina Nolan wanaamini kwamba duniani hakuna nchi kama Tanzania . Hayo aliyoyaona Nolan akiwa Tanzania ni Made in Tanzania tu. Huwezi sehemu yoyote Duniani !
 
Back
Top Bottom