Hii ndiyo taarifa ya SUGU kuhusu usuluhishi

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Taarifa:

kwanza poleni na samahanini kwa hali ya sintofahamu iliyotokea leo kutokana na taarifa za ghafla za usuluhishi kati yetu na Ruge/Clouds fm, ni kutokana na unyeti wa issue yenyewe ilibidi tufanye hivyo kwa nia njema kabisa...

Kwanza naomba tujipongeze kwa kuwa tukio la leo ni ushindi kwa vinega kwa maana kwamba madai yetu yote ya msingi ndio yalikuwa msingi wa majadiliano na Ruge amekubali kuyatekeleza yote...

Kuanzia suala la studio ya rais kurudishwa kwa BASATA ili iwe ya wasanii wote, pia T.F.U ijikabidhi kwa chama halali cha wasanii yaani T.U.M.A kama ambavyo tulikuwa tunadai na mpaka issue za wasanii kunyanyaswa na kubaniwa na pia suala la malipo hafifu vyote vimejadiliwa na kukubaliwa kwa utekelezaji...

Haikuwa kazi rahisi,

Kwanza ilianza kwa wao kumpigia mwenyekiti wangu Mbowe kutaka tukae chini, ambapo kamanda Mbowe alinishauri tukae nao chini kama kweli wana nia ya kuyamaliza...

baadaye wakampigia Mr Shigongo ambaye ni wazi kuwa ni kati ya watu wangu wa karibu naye baada ya kuongea na Mr. Kusaga tu alinipigia na kunishauri hivyo hivyo...na kama haikutosha wakalifikisha hili suala kwenye kamati ya bunge ambayo ilinitaka niipe maelezo ya kiini cha mgogoro na nikafanya hivyo ambapo pia baada ya kunielewa wakashauri nikae nao chini...na hatimaye suala hili likaishia mikononi mwa waziri Nchimbi pamoja na Mhe. Tundu Lissu(MB) kuwa wapatanishi wetu...

Waziri nchimbi akaanza kwa kumuita Ruge Dodoma, ambapo alikuja tukakaa kwa hatua ya kwanza na hatimaye leo tukakaa tena makao makuu ya Wizara ya Utamaduni chini ya Dr. Nchimbi na mhe Tundu Lissu na hatimaye tukafikia hatua hii ya leo...

Vita yetu ilikuwa na hoja hatukuwa tunapigana tu kwa chuki binafsi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanajaribu kuiweka. Kwa hiyo kama hoja zetu zimeeleweka kwa sasa tunatakiwa kushukuru na kufurahia... Lakini naomba niwahakikishie misimamo iko pale pale na nimewaweka wazi kuwa anti-virus itaendelea kuwepo ili kuendelea ku-scan virus wengine kama mameneja masoko na wengine watakaojitokeza kwani nchi inaposhinda vita au hata kufikia tu makubaliano ya amani na nchi adui yake haina maana nchi hiyo inavunja jeshi lake...

Asanteni sana...
 
ndo hapo nakuja amini kuwa chadema ni chama makini kam mr 2 ameweza kusimamia na kudai matakwa ya wasanii wanaoonewa naleo hii imewezekana nashukuru sana.mwanzoni nilielewa kuwa huu ni mgogoro wa wapenda haki dhidi ya waonevu.big up kwa mr tu kwa kuweza kutumia nafasi zake katika bunge kupambana na matunda yake ndo hayo hivyo hivyo endelea kupambana kwenye masuala ya msingi yaliyobakia
 
Sina imani nae tena na mimi ni mmja kati ya watu watakao mnyima kura 2015 kwa usaliti alio tufanyia vinega wa Mwanjerwa, mama john, makunguru, iyunga ,Iremi mpaka Mabatini na Meta.
 
Sugu bana kweli umeota sugu na unatokea kulekule watokako watata ..yaan ruge mwenyewe kasalimu amri? Tatizo ruge alikuwa anaponzwa na vilaza km kibonde.
 
Inapendeza kwa hatua iliyofikiwa na Ruge na Mh. Sugu..sasa cjui Kibonde atakua upande gani maana alikua anaingilia ugomvi uco muhusu..shame on him
 
Kwa makubaliano yale kamayalivyosomwa na Nchimbi jana kupitia TBC yakitekelezwa wasanii watafaidika kiasi fulani, sasa inabidi Sugu aendelee kuvuta uzi ili yale waliyokubaliana yatekelezwe. Big up Sugu, nadhani ulionesha uko serious zaidi kwa kumleta T. Lissu katika suala hilo, kwa upande wangu sichukulii suala hili kama mzaha.

Upande wa vinega nadhani there is much to write and rap about as far as ANTIVIRUS ishakuwa brand iliyosimama, wajipange waendeleze harakati za ku address challenge na matatizo mbalimbali yaliyopo ktk sanaa na jamii kwa ujumla.
 
Inawezekana bado kukawepo na kutoeleweka kwa makubaliano haya miongoni mwa Vinega, lakini kiukweli Sugu na Ruge wamefanya kitu muhimu sana kwa maendeleo ya wasanii na sanaa ya muziki wa vijana kwa hapa bongo
 
the point it there lets see what will happen in the future kama ruge atapiga nyimbo za sugu ,dudu baya,karapina,sister p
 
Taarifa:

kwanza poleni na samahanini kwa hali ya sintofahamu iliyotokea leo kutokana na taarifa za ghafla za usuluhishi kati yetu na Ruge/Clouds fm, ni kutokana na unyeti wa issue yenyewe ilibidi tufanye hivyo kwa nia njema kabisa...

Kwanza naomba tujipongeze kwa kuwa tukio la leo ni ushindi kwa vinega kwa maana kwamba madai yetu yote ya msingi ndio yalikuwa msingi wa majadiliano na Ruge amekubali kuyatekeleza yote...

Kuanzia suala la studio ya rais kurudishwa kwa BASATA ili iwe ya wasanii wote, pia T.F.U ijikabidhi kwa chama halali cha wasanii yaani T.U.M.A kama ambavyo tulikuwa tunadai na mpaka issue za wasanii kunyanyaswa na kubaniwa na pia suala la malipo hafifu vyote vimejadiliwa na kukubaliwa kwa utekelezaji...

Haikuwa kazi rahisi,

Kwanza ilianza kwa wao kumpigia mwenyekiti wangu Mbowe kutaka tukae chini, ambapo kamanda Mbowe alinishauri tukae nao chini kama kweli wana nia ya kuyamaliza...

baadaye wakampigia Mr Shigongo ambaye ni wazi kuwa ni kati ya watu wangu wa karibu naye baada ya kuongea na Mr. Kusaga tu alinipigia na kunishauri hivyo hivyo...na kama haikutosha wakalifikisha hili suala kwenye kamati ya bunge ambayo ilinitaka niipe maelezo ya kiini cha mgogoro na nikafanya hivyo ambapo pia baada ya kunielewa wakashauri nikae nao chini...na hatimaye suala hili likaishia mikononi mwa waziri Nchimbi pamoja na Mhe. Tundu Lissu(MB) kuwa wapatanishi wetu...

Waziri nchimbi akaanza kwa kumuita Ruge Dodoma, ambapo alikuja tukakaa kwa hatua ya kwanza na hatimaye leo tukakaa tena makao makuu ya Wizara ya Utamaduni chini ya Dr. Nchimbi na mhe Tundu Lissu na hatimaye tukafikia hatua hii ya leo...

Vita yetu ilikuwa na hoja hatukuwa tunapigana tu kwa chuki binafsi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanajaribu kuiweka. Kwa hiyo kama hoja zetu zimeeleweka kwa sasa tunatakiwa kushukuru na kufurahia... Lakini naomba niwahakikishie misimamo iko pale pale na nimewaweka wazi kuwa anti-virus itaendelea kuwepo ili kuendelea ku-scan virus wengine kama mameneja masoko na wengine watakaojitokeza kwani nchi inaposhinda vita au hata kufikia tu makubaliano ya amani na nchi adui yake haina maana nchi hiyo inavunja jeshi lake...

Asanteni sana...
Ingawa ilkuwani ushindi kwake, nahisi kama ametumia lugha kali kivileee! Alipaswa kuongea kwa lugha ya kawaida kabisa ili kukwepa uwezekano wa wengine kuonekana kama 'wameshindwa' ili hali jamb zima lilikuwa ni la kuwekana sawa.
 
the point it there lets see what will happen in the future kama ruge atapiga nyimbo za sugu ,dudu baya,karapina,sister p

mzee mbona la kalapina zinapigwa pigwa, alishasalimu amri long time kitambo
 
Sina imani nae tena na mimi ni mmja kati ya watu watakao mnyima kura 2015 kwa usaliti alio tufanyia vinega wa Mwanjerwa, mama john, makunguru, iyunga ,Iremi mpaka Mabatini na Meta.

We kweli akili huna,sasa ulitaka waendelee kutoelewana wakati Ruge kakubali kufiki maAfikino ambayo ni matakwa ya wasAnii ambao wamekua wakinyAnyAswA.Mpe pongezi Sugu ametenda jambo lA maAnA kupigAniA HAKI
 
Sina imani nae tena na mimi ni mmja kati ya watu watakao mnyima kura 2015 kwa usaliti alio tufanyia vinega wa Mwanjerwa, mama john, makunguru, iyunga ,Iremi mpaka Mabatini na Meta.
Umesaritiwa kivipi mbona naona mambo yako wazi kabisa....binafsi nampongeza sana sugu
 
Ingawa ilkuwani ushindi kwake, nahisi kama ametumia lugha kali kivileee! Alipaswa kuongea kwa lugha ya kawaida kabisa ili kukwepa uwezekano wa wengine kuonekana kama 'wameshindwa' ili hali jamb zima lilikuwa ni la kuwekana sawa.
Alipo anza vita hizi SUGu binafsi niliamini atashinda na ameshinda hakuna haja ya kukwepesha ukweli huu kwani karibu madai yao yote yametekelezwa sasa hapo mshindi nani?...Hongera sana kamanda SUGU
 
Back
Top Bottom