Hii ndiyo simu kali mpya kutoka lg ‘g flex’ zenye uwezo wa kujifuta mikwaruzo

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,761
5,877
Kampuni ya LG ya Korea Kusini imetoa simu mpya LG G Flex zilizotengenezwa kwa material yanayoziwezesha simu hizo kurudi katika hali yake ya upya, hata baada ya kupata mikwaruzo ya kawaida ambayo hufanya simu ionekane kuchakaa.

Simu hizo zina uwezo wa kujirudisha katika hali ya kawaida (self-healing) mara baada ya kupata mikwaruzo ya kitu chenye ncha kama funguo,kisu nk, na baada ya muda alama zote za mikwaruzo zinapotea na kurudi
ilivyokuwa.

Pia display ya simu hizo za LG G Flex
imetengenezwa kwa plastic badala ya kioo kama zilivyo simu zingine, na pia muundo wake wa kujikunja (curve) unairuhusu simu kunyooka pindi inapokandamizwa kwa nguvu na kurudi katika hali yake bila kuvunjika.

Kwa simu hizi za G Flex, mtumiaji hatapata yale maumivu ambayo huwakuta watumiaji wengi ya kuvunjika kwa kioo, au simu kupata mikwaruzo mingi inayosababisha kuifanya ichakae haraka.

GG Flex zimezinduliwa kwa soko la kimataifa Jumanne (December 3) huko Hong Kong.

Bei ya simu hizo kwa Korea ni 999,990KRW sawa na Tsh milioni moja na nusu.
 

Attachments

  • 1386087450624.jpg
    1386087450624.jpg
    23.7 KB · Views: 708
  • 1386087464662.jpg
    1386087464662.jpg
    8.7 KB · Views: 587
  • 1386087471992.jpg
    1386087471992.jpg
    17.2 KB · Views: 594
Milioni moja na nusu nikanunue simu!
Hata kama nimeokota hiyo pesa itapata matumizi mengine tu! Kweli watu tumetofautiana
 
Milioni moja na nusu nikanunue simu!
Hata kama nimeokota hiyo pesa itapata matumizi mengine tu! Kweli watu tumetofautiana

Mbona pesa ya kawaida sana hiyo...hii sio simu kwa perception uipatayo ukisikia neno simu, ni zaidi ya kufanya calls au texts.
 
Milioni moja na nusu nikanunue simu!
Hata kama nimeokota hiyo pesa itapata matumizi mengine tu! Kweli watu tumetofautiana

ukiwa hivyo inabidi uwe na subira ikifika 2009 hii simu utaipata mkononi hata elfu 30 tu.
 
hawa wangeweka inayogichaji yenyewe bado gharama zko juu sana mafisadi watanunua
 
ukiwa hivyo inabidi uwe na subira ikifika 2009 hii simu utaipata mkononi hata elfu 30 tu.

I assume you wrote 2019 not 2009.

BTW brother, this curved screens sio Samsung's idea/Technology? I think somebody is asking for a BAN here as your favorite Nokia did to HTC One Mini. Right? chief-mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Mbona pesa ya kawaida sana hiyo...hii sio simu kwa perception uipatayo ukisikia neno simu, ni zaidi ya kufanya calls au texts.

Ina nini cha ziada ambacho siwezi kukipata kwingine?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom