Halidi Mtumbuka
New Member
- Jun 10, 2017
- 2
- 1
Hii ndiyo safari ya soka la Afrika Kusini
Chama cha mpira wa miguu nchini Afrika Kusini kilianza safari ya mafanikio na maendeleo kwa waamuzi na viongozi. Waliwatengeneza waamuzi wenye weledi wanaofanya kazi zao 'kiprofeshino' na viongozi wenye sifa zote kumi na mbili za kuwa kiongozi bora lengo likiwa ni kutafuta maendeleo kuanzia kwa vijana (grassroots) mpaka kufikia ngazi ya taifa.
SAFA walitafuta udhamini kwenye nyanja zote ambazo waliamini ndiyo mafanikio na maendeleo ya soka yalipo. Shule za Soka, mashindano mbalimbali, ung'amuzi wa vipaji vipya, makocha ikiwa sanjari na kutengeneza msingi imara wa kiuchumi ili kuhakikisha hawayumbi. Msingi huu ulikuwa na ubunifu kwenye soko la uchumi.
Uwanjani walianza na vijana chini ya umri wa miaka 12 kimashindano kwenye klabu mbalimbali ambazo zilicheza hadi hatua ya fainali kitaifa. Hawa pia waliunda timu ya timu ya taifa ya umri huo. Chini ya udhamini wa Cadbury, mashundano hayo yalikwenda kwa mafanikio makubwa sana. Simba nayo ilidhamini vituo 11 vya kukuzia vijana nchi nzima na kuajiri makocha 28 ambao walikuwa na jukumu la kuzalisha vijana 60 kutoka kwenye kila kituo wataokwenda kwenye Kituo cha Soka cha SAFA.
Kwa vijana chini ya miaka 14 walidhaminiwa na Shirika la Reli la Afrika Kusini ambao mchakato ulikuwa kama huo wa hapo juu hatimaye vijana waliohitajika kujiunga na SAFA School of Excellence walipatikana. Vijana hawa pia wanashiriki michuano ya Kombe la Nike.
Pia wana timu ya vijana chini ya miaka 17 ambao hushiriki michuano ya mbalimbali kwa ngazi ya dunia ambao hupatikana kutoka kwenye michuano ya Copa Coca Cola.
Timu ya taifa chini ya miaka 20 inadhaminiwa na United Bank. Timu hii ilionesha mafanikio tangu mwaka 1997 nchini Malaysia na Morocco iliposhiriki michuano ya Dunia na Afrika. Mwaka 1994 walianzisha timu ya taifa chini ya miaka 23 wakiwa chini ya udhamini wa kampuni ya Sasol Oil. Ilipofika mwaka 1997 kundi la wachezaji 42 walichaguliwa kutoka kwenye timu hii waliotakiwa kushiriki miacho ya All-Africa Games iliyopangwa kufanyika mwaka 1999 huku Afrika Kusini ikifuzu moja kwa moja kama waandaaji wa michuano hiyo iliyofanyika Johannesburg. Pia walitakiwa kushiriki Sadney Olympic mwaka 2000.
Ilipofika mwaka 1998 wachezaji hawa walikusanywa katika misingi imara ya kisoka. Walishiriki michuano ya Toulan chini Ufaransa wakifuatiwa na kambi nchini Ujerumani. Haya ndiyo mafanikio ya SAFA kuanzia kwa vijana hadi ngazi ya taifa. Siku zote swala hawezi kuchomoka mbele ya mdomo wa simba mwenye njaa kali. Vijana wadogo pia bado wanashiriki michezo na bado wanasoma. Maendeleo haya yanarithiwa kutoka uongozi mmoja hadi uongozi mwingine. Ndiyo maana Nigeria hawakuwa na cha kufanya mbele yao.
Wako;
Halidi Mtumbuka.
halidimtumbuka@gmail.com