Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,439
Anaitwa Mfalme Henry VIII
Alimuona mwanamke mrembo anayeitwa Catherine wa Wales. Ni mwanamke aliyempenda ila tatizo lilikuja pale ambapo mwanamke huyo kila alipokuwa akipata mimba, alizaa watoto wa kike tu.
Henry alikasirika kwani alikuwa akihitaji mtoto wa kiume hivyoo kumfuata Papa aliyekuwa kipindi hicho, Papa Clement VII na kumwambia aivunje ndoa yake kwani mkewe hakuweza kumpatia mtoto wa kiume wa kuuchukua ufalme wake (Kumbuka kipindi hicho Uingereza ilikuwa chini ya Roman Catholic)
Papa akamwambia haiwezekani kwani ndoa hiyo hata Mungu alikuwa akiijua. Mfalme Henry akakasirika sana, alichokifanya ni kuiondoa Uingereza katika dhehebu la Catholic na kuanzisha dhehebu lake ambalo ni Anglikana.
Akamuacha Catherine na kumuoa mwanamke mwingine ambaye alimpatia mtoto wa kiume kitu kilichomfurahisha.
Ukiona mpaka leo Uingereza haipatani na Roman Catholic....usijiulize sana, nimekupa jibu.
Credit: Nyemo Chilongani