Hii ndiyo sababu ya Uingereza kutopatana na Roman Catholic

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,603
2,000

Anaitwa Mfalme Henry VIII

Alimuona mwanamke mrembo anayeitwa Catherine wa Wales. Ni mwanamke aliyempenda ila tatizo lilikuja pale ambapo mwanamke huyo kila alipokuwa akipata mimba, alizaa watoto wa kike tu.

Henry alikasirika kwani alikuwa akihitaji mtoto wa kiume hivyoo kumfuata Papa aliyekuwa kipindi hicho, Papa Clement VII na kumwambia aivunje ndoa yake kwani mkewe hakuweza kumpatia mtoto wa kiume wa kuuchukua ufalme wake (Kumbuka kipindi hicho Uingereza ilikuwa chini ya Roman Catholic)

Papa akamwambia haiwezekani kwani ndoa hiyo hata Mungu alikuwa akiijua. Mfalme Henry akakasirika sana, alichokifanya ni kuiondoa Uingereza katika dhehebu la Catholic na kuanzisha dhehebu lake ambalo ni Anglikana.

Akamuacha Catherine na kumuoa mwanamke mwingine ambaye alimpatia mtoto wa kiume kitu kilichomfurahisha.

Ukiona mpaka leo Uingereza haipatani na Roman Catholic....usijiulize sana, nimekupa jibu.


Credit: Nyemo Chilongani
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,675
2,000
Uko sahihi mleta mada, baada ya Uingereza kujitoa Vatican na kuanzisha Church of England ilitengwa na nchi za Ulaya. Walianzisha motto sawa na hapa kazi tu na kwa kiasi kikubwa ilichangia maendeleo. Hiki kilikuwa kipindi cha mvuko kutoka Agricultural society to Industrial society.

Wengi waliokataa kujiunga na Church of England waliuliwa. Mmoja wapo ni Mtakatifu Thomas More aliyekuwa mwanasheria na councillor pia mmoja wa washauri wa mfalme Henry. Wakati ananyongwa St Thomas More alisema “I die King’s good servarnt but God’s first “.

Mpaka leo hii ni vigumu kuwa waziri mkuu wa Uingereza kama wewe ni mkatoliki. Wakati wa utawala wa Tony Blair, mke wake Cherrie akiwa mkatoliki, Tony alisubiri mpaka alipotoka madarakani ndipo alijiunga na ukatoliki.

Kwenye misa za RC tukimuombea Pope, Maaskofu na Maparoko, CE wanamuombea Malkian Prince Phillip, Prince Charles na Camilla, William na Kate.
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,684
2,000
Uko sahihi mleta mada, baada ya Uingereza kujitoa Vatican na kuanzisha Church of England ilitengwa na nchi za Ulaya. Walianzisha motto sawa na hapa kazi tu na kwa kissing kikubwa ilichangia maendeleo. Hiki kilikuwa kipindi cha mvuko kutoka Agricultural society to Industrial society.
Ba ndio maana ukisikia habari yeyote kuhusu kanisa katoliki katika bbc ujue ni habari hasi..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom