Hii ndiyo Sababu Kubwa na Pekee kwa nini uogope Kufa. Nje ya hapo ni uoga wa kijinga.

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Sababu pekee ni kutokujua kwa nini ulikuja duniani.
Nini mapenzi ya Mungu ambayo anataka uyatekeleze katika kipindi cha uhai wako.

Unaogopa kwa kuwa hunauhakika kama kile kilichokufanya uwepo duniani umekitekeleza.
watu ambao hawaogopi kifo bila unafiki ni wale tu ambao wanausadikisho moyoni mwao kuwa wanatekeleza yale yaliyowafanya kuwepo duniani.
Ni wale wanaojua wametimiza mapenzi ya Mungu ya kwa nini wawepo duniani.
Watu wa namna hii Kifo ni tishio dogo sana na la mwisho. Tishio Kubwa linalowatetemesha ni kitotekeleza kile ambacho wamegundua wameitwa kutekeleza ktk siku za uhai wao.


Mifano:
Ktik Bibilia kuna Mtu anaitwa Paulo. Masimulizi ya kifo chake yanasema. Akiwa anaelekea Kukatwa kichwa na shoka, Alikuwa anasura yenye furaha kama Bwana harusi anayeenda kumpokea Bibiharusi. Kwake Kifo kilikuwa ni Zawadi ya pumziko baada ya kazi kubwa ya kutekeleza alichogundua Mungu alitaka akifanye akiwa hai.

'' Usiku wake alikuwa kaandika Barua kwa kijana wake ambaye alikuwa anamfanyia '' Mentorship'' Stephano''.

''Nimevipiga vita vilivyo vizuri, Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda, Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, atanipa siku ile, wala si mimi tu, bali na wote pia waliopenda kufunuliwa kwake'' Paulo ( Sauli wa tarso).



Mimi naogopa Kufa, maana Bado sijaona kama natembea katika viwango na wito ambao Mungu anataka niutekeleze ktk maisha yangu.

Kila mmoja anawito wake hapa duniani. Iwe Uongozi, Utawala, Biashara, Uchungaji, Uinjilisti, Upatanishi, uhandisi, kusaidia watu, Kuimba, etc.
 
Kuishi ni Kristo kufa ni faida siogopi kifo maana shetani awezi kuniua na wakati wa Bwana ukifika taji langu liko tayar nina hakika kwasababu namuishi ktk mpz yake.
 
Back
Top Bottom