Hii ndiyo pembetatu ya Bermuda (Bermuda triangle)

Brother hizo ni paukwa pakawa hadithi za kufikirika mbiguni hakuwezi kutokea vita hata siku moja, futa kabisa akilini mwako, waligombea ni utawala, biashara, umiliki, utajiri au wanawake? kinachotia utata watowaji wa hekaya hizo wanadhania malaika wanaishi kama binaadam,
Kwa mtazamo wako inaonyesha wewe si Mkristo wala Muislamu, tuambie Imani yako ili tujue jini ya kukuelimisha. Unashangaza sana Brother. Sasa shetani alitoka wapi.na chazo chake ni wapi?.
 
Kwa mtazamo wako inaonyesha wewe si Mkristo wala Muislamu, tuambie Imani yako ili tujue jini ya kukuelimisha. Unashangaza sana Brother. Sasa shetani alitoka wapi.na chazo chake ni wapi?.
Shetani ni sifa wala si kiumbe maalumu
Kiumbe mwenye kutenda maovu na kukana amri za Allah huyo huitwa shetani, kama vile kiumbe anaye iba huitwa mwizi
 
Unapoingia katika tundu la North pole, haina maana kuwa ni tundu kama la chupa ukiingia huwezi kutoka. Kufuatana na force of gravity, tundu ni pana sana, ambapo chombo kama vile engine boat kinaweza kuingia bila ya kuporomoka kwenda chini. Na vile vile chombo kinaweza kusafiri kutoka chini kurudi huu nje ya North pole bila kuona tofauti. Maji yako kawaida, tofauti ni kuwa nchi hiyo lko tofauti kabisa na sehemu tunayoishi kwa sababu unapoingia sehemu hiyo unakuwa umeingia katika dimension tofauti na tunayoishi. Sehemu hiyo sio kuzimu, Lakini wanaishi Demons au malaika waliofukuzwa Mbinguni au viumbe hybrid ya aliens na wanaadamu . Richard Byrd, askari rubani wa jeshi la Amerika aliingia katika North pole na alisafiri kwa masaa zaidi ya sita na kufika sehemu hiyo, Lakini alidhibitiwa na vifaa tofauti vilivyo vya duara (UFO). Alishikiliwa katika mji mkubwa wenye teknologia ya juu sana, na watu wa kule ni watu walikuwa na lafudhi ya kijerumani, na Celtic. Pia aliona alama za NAZI,(swastica). Baada ya muda aliongzwa kurudi alikotoka akiwa salama Lakini hakuweza kueleza zaidi habari za nchi ile.
Hakusimulia, ilijulikanaje habari za huko?
 
Mkuu mm naomba niongeze swali kidogo unisaidie.
Ni kwa nini hiyo sehem ikawa Triangle?
Sehemu hiyo imekuwa triangle kufuatana na mzunguuko wa safari majini kutoka Miami kuenda kisiwa cha Bermuda kuelekea kisiwa cha Puerto Rico na kurdi Miami.
Mzunguuko huo unachora imaginary trial angle majini, na Bermuda ni kisiwa kunaharakati za maisha kama kawaida tizama hapo
bermuda-triangle.jpg
 
Kwa wale wanaopenda kujua matukio mbalimbali, basi watakuwa wanaifahamu vyema historia ya bermuda triangle.


Tangu mwaka 1945, zaidi ya meli 100 zimeshazama na vifo vya watu zaidi ya 1,000 vimeshatokea katika eneo hili ambalo ni maarufu sana kwa vyombo vya safari kupita. Pia ni eneo ambalo linasifika sana kwa kubadilika kwa hali ya hewa kwa haraka na bila kutarajiwa.


Matukio mengi yalitokea katika kipindi cha miaka ya 1940 - 1960, nayo yalihusu upoteaji wa kiajabu wa vyombo vya usafiri hasa ndege na meli.


Mwaka 1944, Dick Stern alikuwa anaruka na ndege ya kivita eneo hili, ghafla ilipoteza uelekea kwa muda na ikawa inaelekea kuanguka Bahari ya Atlantiki, lakin baadaye iliweza kutulia yeneyewe na kuendelea na safari vizuri. Na katika miaka ya 60 alipita tena eneo hilo akiwa na mkewe katika ndege ya kawaida wakapata msukosuko mkubwa.


Kwenye miaka ya 1945, 1958, 1964 na 1967 kuna ndege zilipotea tena katika eneo hilo ambapo mabaki yake hayakuweza kupatikana kabisa. Kuna baadhi ya marubani ambao waliwahi kuripoti kabla ya kupotea au kuokoka kwamba rada zao zilikupoteza uelekeo na kiasi kwamba wakashindwa kujua wako wapi, kuna mmoja aliripoti kuongezeka kwa kasi ya kwenda kwa ndege na kila kitu kikapoteza control, na baadaye vikarudi sawasawa.



Pia kuna rubani mmoja wa ndege ndogo alitaka kutua eneo hilo, lakini alipofika sehemu aliyotaka kutua, hakuiona ilhali watu waliokuwa chini walikuwa wanamuona na kumshangaa akizunguka tu hewani na kisha kuondoka. Baadaye alikiri kuzunguka juu baada ya kutokuona sehemu aliyotaka kutua wakati compass yake ilimuonyesha ameshafika.



Meli amabazo zimekumbwa na misuko sehemu hiyo zimekuwa zikiripotiwa kukutana na mvutano wa ajabu wa kwenda chini na mwishowe kuzama, au kukutana na machafuko ya bahari ya ghafla.


Kuna baadhi ya wafanyakazi wa meli walio okolewa waligeuka na kuwa vichaa!


Kituko cha funga dimba ni kile kilichoripotiwa mwaka 1967 kutoka kwa watu waliokuwa kwenye meli ya Elizabeth I pale waliposhuhudia ndege ndogo ikiwa mita chache kutoka walipo ikipotea ghafla ikiwa inaruka!!!!


Maajabu makubwa ambayo tutayaongelea, KWANZA ni kupotea kwa ndege nyingi ambazo zimepita katika anga la eneo hilo PILI ni kupotea kwa meli nyingi zinazopita katika eneo hilo. na kubwa zaidi ni kutopatikana kwa taarifa yoyote kuhusu mahali ambapo meli na ndege hizo huelekea baada ya kupotea. Swali kubwa linalozuka ni Je ninini chanzo kikubwa cha kupotea kwa vyombo hivyo? kwa miaka mingi iliyopita chanzo chake hakikujulikana, lakini katika uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na kituo kikubwa ulimwenguni cha uchunguzi wa anga NASA, inahisiwa kuwa eneo hilo limezungukwa na nguvu za usumaku zinazofanya kutokea kwa nguvu kubwa ya uvutano inayovuta kitu chochote kinachopatikana eneo hilo au katika anga la eneo hilo

Pia inahisiwa kuwa katika eneo hilo kuna kemikali ya METHANE iliyoyeyuka na kuchangamana na maji hayo jambo linalofanya maji ya eneo hilo kutokuwa na uwezo wa kuhimili uzito wa meli katika eneo hilo, swali ni je kuna uhusiano gani kati ya upotevu wa ndege na uwepo wa kemikali katika maji..

Jamani hili eneo hadi wameliita pembe tatu ya shetani au mlango wa kuzimu kuna nini hapa panapopelekea hadi meli na ndege kubwa kuzama na zaidi zikizama hazijulikani zinaenda wapi,? Mara hii sehemu tunaambiwa ALIENS wanakaa eneo hili kwaio sababu wao wana teknolojia isiyoweza kushindanishwa na za huku duniani wanasema inawezekana pia kitu chochote kinachopita eneo.hilo kinashindwa kuhimili hio nguvu ya teknolojia yao kwaio inapelekea wao kuzichukua kwa sababu zao au kuzitokomeza.

View attachment 657810


HABARI,
"PATO8221,
Hongera kwa kuanzisha mada nzuri,Kwangu mimi binafsi nimeshasikia habari hizi siku nyingi sana ila ukisoma maelezo mengi maelezo yanajibu nadharia tu.Kuna mtu amezungumzia NASA hapo juu sawa ila hata wao pia NAS hawajatoa jibu kamili labda niwe sijalisoma.Kwangu binafsi nafikiria sana na mawazo ya baadhi wa wachangiaji hapa.Hasa wanaosema mambo ya guvu za mvutano-usumaku, nafikiria pia kuwepo na mkondo mkubwa wa maji mara nyingi zaidi ya pale nungwi kwenda zanzibar unaopita pale ukijumlisha na hizo nguvu za mvutano ila si muda mrefu tutapata majibu.Lakini pia mbona kwa sasa hatujasikia visa vingine vikitokea pale Nahisi pia isije ikawa kuna baadhi ya taifa kubwa lilikuwa linafanya majaribio yake ya kisayansi ya silaha na mambo mengine wakatengeneza mada ya kuwa ni sehemu yenye guvu za ajabu ni kitu kinachofikirika hicho.

LUMUMBA
 
Kuna kipindi nilifuatilia sana, nikashangaa. Majanga yake hadi kwenye ndege zinaozopita pale kwa juu, ukijichanganya pale na ukatoka salama toa sadaka ya shukurani. Sina maelezo ya kisayansi ila ipo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom