Hii ndiyo njia pekee inayoweza muokoa Mdude CHADEMA

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Wakuu habari zenu, poleni na Corona!

Naomba niende kwenye point.

Hili tukio la mdude kukamatwa na siku tatu bila kujulikana nini sababu ya kukamatwa huku akiyimwa dhamana, wengi tulijua kuwa anaundiwa kesi. Na wamefanikiwa 100%.

Kusema ukweli hii kesi mdude hachomoki kama wakina Mbowe ambavyo waliteseka kwenye kesi ya Aqwilina.

Isitoshe, akitaka kuwa mbishi nakutaka kuprove sio guilty, atakaa maabusu muda mrefu sana. Kesi ya kuhujumu uchumi unaweza wekwa maabusu huku ukisubiri ushahidi ukamilike kwa muda usiojulikana.

Ushauri wangu ni: Wanasheria watusaidie tujue kesi ya namna hii kwa sana sana mdude anaweza kuhukumiwa kufungwa kwa muda gani au fine yake ni kiasi gani.

23g ya madawa ya kulevya ni kidogo sana. Kwa uelewa wangu ( legal illiterate) sidhani kama anaweza kuhukumiwa kufungwa zaidi ya miaka 3. Na fine yake kisheria sifikiri kama ni zaidi ya m 200.

Kama watu "wamebatiziwa" kesi za uhujumu uchumi na wakashauriwa wakubali na walipe fine. Kwanini mdude asifanye ivyo?

Tuassume kama hii kesi anaweza kuhukumiwa kulipa fine. And if so, kwanini as plead guilty tu mapema ili asipoteze muda na "wazalendo" tumchangie atoke mapema iwezekanavyo?

Hili ndilo wazo langu ila sijui sheria kiundani labda wahusika na wabobezi katika sheria wanaweza toa ushauri wa kisheria.

Nafikiri ikiwezekana kuwa ivyo, Mdude atapata mileage kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje. Na dunia Nzima itaendelea kujua Tanzania ipo chini ya utawala wa aina gani.

Hakuna haja ya Mdude kuonesha kuwa hayupo Guilty. Dunia nzima ukweli tunaujua.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtego mkubwa sana kwa mtuhumiwa.mUkubwa wake ni kwamba akikubali kosa na kuhukumiwa jela zaidi ya miezi 6 ndio unakuwa mwisho wa ndoto zake kisiasa kushika nafasi za uwakiishi serikalini kama ubunge, udiwani n.k.
 
Kama watu "wamebatiziwa" kesi za uhujumu uchumi na wakashauriwa wakubali na walipe fine. Kwanini mdude asifanye ivyo?

Tuassume kama hii kesi anaweza kuhukumiwa kulipa fine. And if so, kwanini as plead guilty tu mapema ili asipoteze muda na "wazalendo" tumchangie atoke mapema iwezekanavyo?
Kwani umesikia wana shida na hela?? Nadhani hii ndiyo njia pekee ya kumuweka kando wakati huu wa vugu vugu la uchaguzi. Hivyo aangalie anavyo kubali hilo kosa. Asije ingia kichwa kichwa akala vyote viwili. Fine na jela miaka 5
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Mimi nilitegemea kusikia kwamba wamempima na wamebaini ni mtumiaji wa hayo madawa pia, maana picha inayotaka kutengenezwa hapa ni kwamba yeye ni mtumiaji ingawa hawajampima! Na ni ngumu kutaka kutuaminisha kwamba yeye hatumii hayo madawa ila wamemkuta nayo.

Mpaka sasa Hili tukio linaacha maswali mengi mno, ushahidi wa kimazingara unaonesha asilimia 90+% hii kesi ya kubambikiza..
 
CCM ya sasa imekuwa yaki mama sana.tuone watapambana na wapinzani wangapi wakumbuke upinzani hauwezi kuisha.

Naomba kuuliza. Hivi muuza dawa za kulevya sura yake inafananaje. Au je ukiwa CHadema automatically inakuwa huwezi kuwa mhalifu.

Hivi mtu aliyekuwa anatukana vile anawezaje kutofautiana na madawa ya kulevya. Mfano Bangi. Kuwa wakati migongo ya vyama isiwape uhalali wa ujinga.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani umesikia wana shida na hela?? Nadhani hii ndiyo njia pekee ya kumuweka kando wakati huu wa vugu vugu la uchaguzi. Hivyo aangalie anavyo kubali hilo kosa. Asije ingia kichwa kichwa akala vyote viwili. Fine na jela miaka 5
Ndyo maana nkasema huu mjadala unahitaji legal guidance. Wakina wemasepetu mbona walikutwa na madawa na walipimwa na kukutwa ni watumiaji ila walichomoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza. Hivi muuza dawa za kulevya sura yake inafananaje. Au je ukiwa CHadema automatically inakuwa huwezi kuwa mhalifu. Hivi mtu aliyekuwa anatukana vile anawezaje kutofautiana na madawa ya kulevya. Mfano Bangi. Kuwa wakati migongo ya vyama isiwape uhalali wa ujinga.


Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unauwakika kama anafanya biashara hiyo,kwani hawezi kubambikiwa kesi.Tuliza kwikwi hiyo mahakama italeta mrejesho.
 
kwa hakimu mkereketwa kama yule aliyemhukumu Sugu...

Mdude atalipa fine na kifungo juu yake
 
Back
Top Bottom