Hii ndiyo moja ya sababu Wakenya wako dakika 5 mbele yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo moja ya sababu Wakenya wako dakika 5 mbele yetu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Quemu, Oct 23, 2010.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kuna documentary moja naiandaa ambayo inahitaji video production.

  Sasa basi, niliwasiliana na kampuni maarufu za video production nne (sitozitaja) hapa nchini katika ku-shop moja ambayo itaifanya hiyo kazi kwa ufanisi. Tatu kati ya hizo zinamilikiwa na wabongo wenzetu. Moja na Mkenya.

  Mkurugenzi wa kampuni moja ya mbongo hakunipa nafasi hata ya kumtembelea ofisini kwake. Kwani kila nikiwasiliana naye kwenye simu ananiambia yupo “bize” kichizi, na kwamba atanitafuta atakapopata nafasi. Ieleweke kuwa toka nilipompigia simu ya kwanza kabisa, nilimweleza sababu ya kwa nini nahitaji kuonana naye.

  Nilipotembelea kampuni nyingine ya mbongo nilimkuta mkurugenzi amesafiri. Basi nikaongea na mhusika mwingine muhimu hapo na kumwelezea kilichonipeleka pale. Akanielewa vizuri na kuahidi kuwa pindi mkurugenzi atakaporudi (alikuwa arudi siku 3 baadaye) atamwelezea. Na kwamba mkurugenzi atani-contact ili tuonane. Wiki ikapita. Nikamwendea hewani yule mhusika, akanieleza kuwa alimwelezea mkurugenzi pindi aliporudi tu, mkurugenzi akaahidi kunitafuta. Basi nikasubiri siku kama 2 hivi, nikaibuka pale ofisini kwao tena. Stori niliyoipata hapo ikaniacha hoi….eti mkurugenzi amesafiri tena, amekwenda nje ya nchi kwa kama wiki 3 hivi, na kwamba hajaacha maagizo yoyote kuhusu kazi ambayo nimewapelekea. Nikagwaya!

  Kampuni ya 3 ya mbongo, nilifanikiwa kumwona mkurugenzi baada ya kujaribu kama mara 3 hivi. Tukaongea naye na akaniambia atajibu siku inayofuatia. Wiki imepita sijasikia chochote kutoka kwake.

  Pia, nilikwenda kwenye kampuni ambaye mkurugenzi wake ni mkenya. Kwanza attention aliyonipa huyo jamaa ilinitia moyo sana. Nilipokuwa namwelezea program yangu, jamaa alikuwa anathubutu mpaka kuchangia ideas zake (wabongo hawakufanya hivyo) ni vipi kampuni yake inavyoweza ku-shoot hii documentary kwa ufanisi wa hali ya juu. Jamaa akahidi kukutana na timu yake kesho yake, halafu tungeonana naye keshokutwa yake kwa majadiliano zaidi. Kesho yake asubuhi na mapema, mshikaji akanitumia sms kuniambia kuwa amepitia tena maelezo niliyompatia na kwamba amepata ideas nyingine mzuri za kuongezea. Na pia hakanihakikishia kuwa vifaa na uwezo wa ku-produce program yangu anavyo vya kutosha. Hakuishia hapo ! jioni yake akanipigia simu na kuniambia kuwa ameshajadili na timu yake, na kwamba tuonane siku inayofuatia saa 5 asubuhi kwa mazungumzo zaidi. Kwenye appointment yetu ya siku iliyofuatia, sio tu alizidi kunihakikishia kuwa anaweza kazi, bali pia alinionesha baadhi ya documentary walizowahi ku-shoot, na akaenda mbali zaidi kwa kunionesha vifaa vyote vya production alivyonavyo.

  Chagua langu likawa rahisi !!!!
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
  Wabongo wenzangu !

  Mchawi wetu ni nani – Wakenya au Sisi wenyewe?

  Yaani mtu unapeleka kazi kwenye haya makampuni, lakini wao wanataka uwafukuzie kana kwamba unaenda kuomba kazi au msaada ! Kha gademu!!
   
 2. BrainPower

  BrainPower Senior Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inanikumbusha 2005 nilipita pita Kenya, nilisoma gazeti mmoja - nadhani ilikuwa ni the standard kama sikosei. Nikakutana na ka-article ka-mmoja. Mwandishi kweli alikuwa anatupa live. Eti alisema kwenye kipengele kimoja unlike our neighbours, Tanzanians, We Kenyans do not wait for the Coconut to fall from the tree. We climb up the tree and pick up the Coconut. We! nilitoka na Hasira huko.

  Lakini busara baadaye ikanijia.., nikaelewa mwandishi alikuwa anajaribu kusema nini.. Subject hii ni very controversial, tunakasirika tukiambiwa (wa kwanza ni mimi). Lakini bora ukasirike alafu ujibadilishe in the process. Ofcourse kuna vijana (wazawa) ambao speed yao / creativity (kwenye biashara) ni ya kutisha hapa mjini -lakini bado wachache mno. Ninaongelea majority, kwasababu kwenye ushindani labour market na hii EAC -the best man/woman wins. Mwenyewe umeona...

  B.P (2010)
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo la wabongo tunabweteka haraka na sifa. Mtu akishapata umaarufu anasahau wateja.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  simple reasoning.....kama wakurugenzi wa makampuni ya kibongo walikuwa busy, sasa ulitegemea ungeonana nao vipi. it also means wapo busy. huyo mkenya alikuwa hana kazi!
   
 5. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante kwa maelezo yako. Kuna mambo mengi sasa sana wabongo wako mbele ya Kenya. Moja wapo ni property ownership. Wabongo wengi wana rasilimali (real property) zaidi ya wakenya. u should be happy for that. Hii mambo ya soko huria (free enterprises) sisi ndo tuko mwaka wa 24 kenya wamekua kwenye free market zaidi ya miaka hamsini (50 in the system). what is there to show. tell me right here. Kitu ambacho nimejifunza kutoka kwenye posti hii njema, inaonaka wabongo hawajaelewa uhusiano kati ya kastama keya na profitability. Kenya nawapa pongezi kwa hili. likini kumbuka hawa jamaa wamekua kwenye system ya free market for a very long time to be where they are. Probably instead of focusing on what they do better, let see what went wrong so we are not going to be on their situation or even worse the next tweny years. Asante kwa posti yako na nyingine zilizofuatia.
   
 6. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Also, we do not know what information led them to act adversely to this proposal. All business, the good, the bad, and the ugly makes descision based on the information at hand. I do not know any production company in Tanzania that would reject business. never. the whole thing could be a Kenyan marketing gimmick to potrays a doubtful accounts on tanzania business performance and incompetence, which will led to legally discrimate tanzanian demography from getting higher level management positions and challenging contracts. Legally, Tanzania will be required to have a suretybond a.k.a perfomance bond before a winning of a contracts. I am getting really sick of hearing this. it like no body know in Africa the people to watch is Nigerians and Kenyans in frauds and corraption. it is called NaiRoberry. Its like tz does not know other kapitalistic countries to take example but kenya. how about Uganda. I think they are successfull than kenyans on property ownerships. Actually, kenyans needs a lot of help from us. Acheni hii mambo ya malumbano. Africa ni kushirikiana. yani wakenya ni masikini sana kuliko wabongo, property ownership which is the credo of capitalism (by the way capitalism has many excepted styles.). Serikali yetu ilete tabia ya kupima performances. thats all, thank you

  Kenya is even behind of Congo katika utamaduni wa wananchi kumiliki mali. take it slowly gentlemen.
   
 7. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  S- say helo
  H- heads up
  O-offer related item
  p- prepare for success
  P-polite at all times
  I-introduce add ons
  E-every customer leaves happy

  follow that and u'll be on top of ya bussiness
   
 8. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Hebu nambie kunamtanzania gani atashindwa kufanya haya yalio andikwa na HashyKool. Watanzania tunafanya hivi kwa bure maishani mwetu humu bongo. Kuna namna ya kuwafundisha wajasirimali waelewe. lakini badala ya kuwe maneno machache kama haya. waandishi wetu huandika maneno alfu. wanadhani ndio kufundisha. acha nijaribu kutafsiri kama ntaweza: asante hashkul


  1. Msalimie mteja (mkaribishe vizuri) kwa tabasamu. lakini tabasamu sio lazima. muhimu mteja ajue unamthamini kama binadamu

  2. Innua kichwa, usikae kama mtoto anaekaripiwa. tizama watu mmacho.

  3. muonyeshe mteja bidhaa na huduma anazohitaji. au anaweza akahitaji (akinunua tumajani ya twa-chai, unamuonyesha na sukari ya zambia)

  4. tuwe na adabu, hata kama ni katoto au mteja sio muhindi, mzungu, muarabu au kabila yeyote. (watu wote wanahita heshima). usichanganyiwe ukajisahau uko kazini kuhudumia watu wote.

  Mengine naona waendelee kutafsiri.
  4. Muheshimu mteja wakati wote (mpe wadhifa wake tafadhal)
   
 9. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Birigita,

  Nitakupa issue nyingine inayofanana kidogo na hiyo, kudhihirisha ni jinsi gani siyo suala la ubize, bali ni kutojua au kudharau misingi ya biashara (angalia SHOPPIE kutoka kwa Hashycool) ambayo inasababisha tuzidiwe kete na Wakenya.

  Nina wasanii wa Bongo Fleva Kadhaa ambao nina wa-manage.

  Kunako mwanzoni mwa mwezi wa 7, Kuna shooter mmoja mbongo maarufu sana hapa nchini (maarufu wako 2 tu.......yes you guessed right.....mmoja wao), nilimpatia kazi ya kushoot video ya wimbo mpya wa mmoja wa wasanii wangu. Tukakubaliana kazi ya editing itakuwa tayari imemalizika wiki moja baadaye. Amini usiamini, wiki moja baadaye jamaa akaanza kuleta story. Haikupita muda mrefu akaacha kupokea simu zangu, sms akawahajibu, ofisini kwake haonekani, na vitimbwi vingine kibao. Kwa kifupi tu, ile video ilishutiwa July 10, sikupata video mpaka Oct 6. Yaani mpaka tukaanza kutishiana kupigia simu advocate and all that...ndipo alipofanya kazi.

  Katika kufanya uchunguzi, nikaja kugundua kuwa huyu shooter hii ndiyo tabia yake. Amekuwa anachelewesha kazi za wasanii wengi tu. Kuna waliompeleka polisi, kuna waliomwendea nyumbani/ofisini kwake na rungu, kuna waliomjia na machizi wa kitaa, na kuendelea. Jamaa huwa anatabia ya kurundika kazi za watu, halafu anasikia uvivu kuzi-edit. Yaani akivuta mkwanja wa kazi tu, anapotea.

  Sasa ubize huko wapi hapo ndugu? Kwa hali hii, majirani zetu wakenya wakija wanakamata kazi kirahisi mno. Sisi hatujali wateja wala muda. Tunalewa sifa haraka mno na kusahau shughuli zinazopeleka mkono kinywani. Tunaangalia leo, na kusahau kuwa kuna kesho, keshokutwa, na mtondogoo..

  If we don't change our entrepreneurship tactics, we gonna get whipped by EA common market pretty bad!!!
   
 10. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nakunga mkono kwa hilo wabongo wengi hawajui walifanyalo wamezoea njia za mkato,ujanjaujanja kila sehemu na sio wakweli badala ya kukukwambia kitu hiki sikiwezi yeye atakwambia ah njoo kesho mara oh muhusika kasafiri ,wabongo hatujui timelines na hatujui kuwa unaposema uongo husimamisha shughuli za watu kibao ambao ndio wahusika wa shughuli inayotakiwa kufanywa
   
 11. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  You are right. Wabongo wako slow, angalia hata wanavyotembea barabarani, kama wanaumwa.
   
 12. Cathy Duncan

  Cathy Duncan Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sorry to bother you guys, I don’t really think that Tanzanians are sick of anything. I’m just saying this because I really had a great time trading with them, in the past.
   
 13. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,061
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Nasikitishwa sana na baadhi ya mijitu humu wakati maudhui muhimu ikijadiliwa, badala ya kufikiria na kutoa mchango wa mantiki, wakimbilia kujihami kwa utaifa na the so-called uzalendo. Hayo mambo yamekwisha. Dunia inakwenda kwenye one global government na watu bado wanajivunia u-inchi, kha! Hivi si kweli kwamba Wakenya wana maisha bora kuliko sisi? Hivi si kweli kuwa Wakenya ni wachapa kazi zaidi yetu?
  Wengine wanataka kutoa excuses ooh, Wakenya wako kwenye system miaka mingi.....kha! Kwani inapasa kuwa kwenye system miaka mingi kujua kwamba ili uendeshe biashara yenye faida ni lazima uwathamini wateja wako? Ni lazima uwe na miadi? Haya pia yapasa kuwa kwenye thythtem kwa miaka 50? Wabongo...bureeeeeeeee, kichwa maji. Halafu nime-note kila kikizungumziwa kitu kizuri cha Mkenya kinawakera Wabongo....inferiority complex!
   
 14. Zneba

  Zneba Senior Member

  #14
  Nov 10, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe na ww umeliona hivyo halfu kama hujastukia wabongo tunapenda kutetea ujinga inshu siyo miaka hamsini hata miaka miwili tu tungeweza kufanya mabadiliko tukafanana na hao wa miaka hamsini,tatizo hatujitumi na ni wakata tamaa mno
   
 15. k

  kirongaya Member

  #15
  Nov 10, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni tatizo kubwa sana lakini hii economic intergaration itatunyoosha sana, maringo na uvivu vitatuisha bila kupenda wenzetu wanajua kazi maana yake nini mfano halisi mkoa wetu jirani unoongoza kwa utaliii na hoteli yaani Arusha nafasi za hotelia na utalii zimechukuliwa na jirani zetu wakenya sababu kubwa unaijua? jibu lake ni WACHAPA KAZI
   
 16. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  All well said wakuu, wabongo tubadilike, if we are relatively better we can be best
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ongezea mtu akishaona bank acc inasoma dola 10000 anajihesabu milionea kula bata kwenda mbele!
   
 18. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,546
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  wabongo wanapenda starehe kuliko kazi , tunamaneno mengii sana ambayo hayasaidii . ni kweli arusha viongozi kwenye hoteli nyingi za kitalii ni wakenya maana wengi wawa bongo ni wavivu, wezi , wanamajungu na wazembe . mungu atusaidie ili tubadilike maana huko tuendako si mchezo .
   
 19. S

  Somi JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  watanzania hawataweza kuwapita wakenya na nchi nyingine kwa maendeleo , sababu ni

  1.wavivu hawapendi kuwajibika nenda maofisini n.k. utashuhudia nayosema
  2.wanaridhika mapema hawataki mafanikio ya kuendelea
  3.wanapenda mafanikio ya short cut bila kuumia na kuvumilia kwa muda mrefu na hii kupelekea nchi kuwa na ufisadi kila mahali pa kazi ili mradi wajipatie ela za wizi
  4.ni matapeli
  5.hawapendi kuumiza kichwa kwa ajili ya kupata majibu ya vikwazo mbali mbali na hivyo kukata tamaa mapema

  kuna jamaa kadhaa wenye maeneo ya uchimbaji wa madini ambao waliniomba niwaunganishe na wafadhili wawasaidie kuwapa vifaa vya uchimbaji ili wazalishe madini kwa masharti mali inayopatikana watagawana na hao wazungu kwa asilimia ya makubaliano kulingana na masharti ya mkataba
  wa kwanza akataka apewe ela kama kianzio kwa sharti la kuingia mkataba alionyesha tamaa ya kupata ela mapema bila kuangalia mafanikio ya muda mrefu mzungu akasema "bull shit"
  wa pili akapewa mkataba hadithi ndio ikawa ya kutafutana kwenye simu mpaka nikachoka ,kila siku sababu anatoa mara leo nilikuwa hapa mara juzi nilikuwa nafanya hivi nikawa namtafuta mimi kila wakati basi nikachoka nikamuacha na sababu zake
  halafu wa tanzania wanakiburi fulani kama anakitu basi atataka umtafute yeye kwakuwa anakitu hajui hicho kitu kinatakiwa kizalishe ela lasivyo atakosa ela na faida ya hicho kitu alichonacho itakuwa zero maana kila bidhaa duniani lengo ni kuzalisha ela.
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  si kweli aisee hakikisha watejawako unawapa appointment za kukamilika bwana! mi sitetei ujinga wa wabongo wengi!
   
Loading...