Hii Ndiyo mifuko mbadala kuanzia tarehe 01.06.2019

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,191
USHINDI KWENYE MAZINGIRA.

Tunapenda kuipongeza serikali kupitia kauli ya Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye kuhitimisha bajeti ya ofisi yake bungeni hapo jana tarehe 09.04.2019 kwa kuweka ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki.

Taasisi ya Waandishi wa Habari Marafiki wa Mazingira na Urithi wa Asili JFW-NH tunapongeza juhudi hizi za serikali ambazo taasisi yetu imekuwa ikijitahidi kutoa elimu na kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi kuepukana na matumizi ya mifuko hiyo.

Sehemu tofauti kumewahi kutukia magonjwa, vifo na madhara mbalimbali yatokanayo na mifuko hiyo, hivyo kupigwa marufuku mifuko hiyo kwetu sisi ni ushindi mkubwa kuelekea kuifanya dunia sehemu salama na rafiki kwa binadamu kuishi.
Aluta Continual.
JFW-NH
Hakuna ufafanuzi unaopatikana wa picha.
 
Back
Top Bottom