hii ndiyo maana ya msanii kioo cha jamii???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hii ndiyo maana ya msanii kioo cha jamii????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mapambazuko, Oct 8, 2010.

 1. m

  mapambazuko Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani leo katika pitia pitia yangu ya gazeti la michezo la bingwa kuna makala moja imeandikwa na mwandishi mmoja anaitwa ojuku abrahamu anazungumzia kuhusu wasanii anawashangaa hivi kwa meseji yao kwa jamii hivi au kutambua kwao nini jamii inahitaji kwa wakati gani ingawa mimi ningelipenda awapake kabisa,

  unajua hawa wasanii wa bongo fleva na hip hop ya kibongo ambao wengi huwa wanajifanya ni wanaharakati wa mapinduzi ya fikra lakini cha kushangaza sijui huwa hawajui nini maana ya usanii kioo cha jamii!! hebu mchukulie mtu kama joseph haule "profesa j" mzee wa mitulinga kwa nyimbo zake nzuri za kuelimisha jamii juu ya utambuzi wa nani anayestahili kupigiwa kura za kupata uongozi hasa ile nyimbo yake ya ndiyo mzee aliyofanya na na afande sele juma nature na nyimbo nyingine inayozungumzia ahaadi hewa za wagombea lakini leo hii yeye ndiyo wa kwanza kwenye majukwaa yanayokweda kinyume na meseji yake tumweleweje ni haki kumwita mwanamapinzduzi wa fikra au yeye kweli ni kioo cha jamii??? mimi kwa mtazamo wangu heshima ni zaidi ya pesa!!! jamaa kachemka sanaa
  yaani yule bwana mdogo wa kigamboni Roma kesho tumkute kwenye majukwaa ya siasa nahamasisha kinyume na ujumbe wa kwenye single zake hivi jamii itamwelewa kweli? au hawa wasanii wetu bado kujielewa?? namsikitiakia sana j wenzangu mnasemaje juu ya hili??
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Njaaa,unafiki, kujikomba, n.k ndo vinamsumbua j
   
Loading...