Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,445
Disemba 12 2018 Serikali ya Tanzania chini ya utawala wa Dkt John Pombe Magufuli na kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri zilitilia saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme lkatika mto Rujifi (Stiegler's Gorge) utakaotekelezwa kwa muda wa miezi 42 kuanzia sasa.
Katika halfa hiyo ya kutia saini iliyohudhuriwa na Rais wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mustafa Madbouly,kwa upande wa Tanzania aliyetia aini ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la umeme Tanzania(TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka huku upande wa Misri ukiwakilishwa na Mwenyekkiti wa kampuni ya Arabs Contractors Bwana Mohamed Mohsen Salaheldin na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Elsewedy Bwana Ahmed Sadek Elsewedy.
Kampuni ya Arab Contractors iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo mkubwa utakaozalisha megawati 2,115 utakapokamilika ni kampuni ya ujenzi kutoka Misri iliyoanzishwa mwaka 1955 yenye makao yake makuu jijini Cairo.
Mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Bwana Osman Ahmed Osman ambaye aloikuwa ni mjasiriamali na mwanasiasa nchini humo na pia aliwahi kuwa Waziri wa Makzi wa Misri chini ya utawala wa Rais kipenzi cha watu Anwar Saadat aliyeongoza kuanza 1971 hadi 1980.
Osman Ahmed Osman alifahamika zaidi kama El-mo;alim alifariki Mei Mosi 1999 jijini Cairo.
Kampuni hiyo ilitaifishwa na kuwa mali ya serikali baada ya kutokea mapinduzi nchini humo.
Kampuni hiyo pia ilishiriki katika ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme nchini humo la Aswan ambalo lilionekana na njia ya kuleta mapinduzi ya Viwanda nchini humo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuzalisha umeme.
Ujenzi wa bwaa la Awan ulianza mwaka 1960 na kufungulia rasmi mwaka 1970 yaani miaka 10 baadae.Bwawa hilo lina urefu wa kina cha futi 364 urefu wa kilometa 3.83 na upana wa mita 980.
Kampuni hiyo pia imehusika na ujenzi wa majengo mbalimbali ya nchini humo na nje ya nchi.Hadi sasa kampuni hiyo ya Arab Contractors ina miradi katika nchi 29 duniani kote.
Mbali na ujenzi kampuni hiyo inamiliki klabu ya mpira wa miguu ya El Mokawloon SC inayoshiriki ligi kuu ya nchini Misri.
Katika michuano ya klabu bingwa ya Afrika mwaka 1996 klabu hiyo inayomilikiwa na kampuni hii ilikutana na Simba SC ya Tanzania katika mzunguko wa pili ambapo katika mchezo wa kwanza klabu ya El Mokawloon SC ilikubali kipigo cha 3-1 kutoka kwa Simba SC.Na katika marudiano klabu ya Simba SC ilifungwa 2-0 na hivyo klabu ya El Mokawloon iliingia robo fainali kwa faida ya goli la ugenini.
Katika fainali hizo klabu ya El Mokawloon ilifanikiwa kutinga fainali kwa kuifunga klabu ya Sodigraf ya Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo(DRC) kwa magoli 4-0 na kufanikiwa kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika.
Hapo chini ni baadhi ya miradi iliyowahi kutekelezwa na kampuni hiyo
Bibliotheca Alexandrina
Uwanja wa mpira wa Borg El Arab
Bwawa la Aswan
Cairo Regional Ring Road
Uwanja wa ndee wa kimataifa wa Luxor