hii ndiyo kampuni ya Abdulrahman Kinana

Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,173
708
Wandugu naomba msome hii taarifa ndio mjue nchi yetu imeoza

KAMPUNI ya uwakala iliyosafirisha kontena lililokuwa na meno ya tembo ambayo yalikamatwa nchini Vietnam, inamilikiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM na ambaye sasa ndiyo katibu mkuu Abdulrahman Kinana, imefahamika.
Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam.
Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussen anamiliki hisa 2,500 zenye thamani ya shilingi 1,000 kila moja.
Kwamujibu wa taarifa za usajili, wamiliki wote wawili, Kinana na Rahma wanapatikana kwa S.L.P 10910, Kiwanja Na. 403 Mtaa wa Tosamaganga, Msasani Peninsular, Dar es Salaam.
Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
Sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali zilizosafirishwa na kampuni ya Sharaf Shipping Agency liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
Hati ya kusafirisha makontena hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni pembe za ndovu ilisainiwa na mfanyakazi mwenye asili ya India wa kampuni hiyo Samir Hemani.
Nyaraka zote zilionyesha kuwa kilichokuwa ndani ni plastiki zilizorudufiwa, wakati baada ya makontena kukamatwa, walikuta yamesheheni pembe za ndovu.
Taarifa zinasema kibali cha kusafirishwa kontena hilo kilisainiwa 13 Novemba 2008 na Meneja wa Fedha na Utawala wa Kampuni hiyo.
Wakati Hemani anasaini nyaraka hizo, kibali chake cha kuishi nchini tayari kilikuwa kimeshaisha. Kibali cha Hemani kiliisha 7 Mei 2008.
Makontena yalikamtwa nchini China yakisafirishwa kwenda Hong Kong.
Akichangia makadirio ya bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.
Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Phillipines, China, Singapore na Hong Kong.
Kutokana na kutopatikana kwa Kinana juzi kuzungumzia suala hilo, haikufahamika iwapo kampuni ya spika huyo wa zamani wa Afrika Mashariki au yeye mwenyewe, walijua kilichokuwamo katika makontena hayo.
Lakini afisa mwandamizi katika wizara ya Viwanda na Biashara alisema kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Alisema wanaowajibika kusitisha mzigo kusafirishwa pindi wanapoutilia mashaka ni TRA.
"TRA ndio wanakagua na baada ya kujiridhisha kama kilichomo ndani ndicho kilichotamkwa kwenye nyaraka na ni halali, ndipo wanaweka muhuri (seal) wa mwisho," alisema afisa huyo.
"Ukitamka kwa mfano, kuwa katika nyaraka ndani ya kontena kuna matairi 40 ya magari, lazima TRA wafungue na kukagua kuona kama kweli yako matairi 40 au kitu kingine. Baada ya hapo wanaweka seal; sasa kuna kila sababu ya kujenga mashaka,” alieleza.
Alisema, "Wakala wa meli kazi yake ni kusafirisha mzigo wa mteja wake. Hata mteja akija na kontena tupu na kusema anataka liende nchi fulani, kazi yake ni kulipeleka kunakohusika na si kuhoji kilichomo.”
Alifafanua kuwa watu muhimu wa kuhojiwa na ambao wanaweza kuwa wanajua mchezo wote, kama upo, ni wafanyakazi wa TRA.
Hadi juzi Jumatatu hakukuwa na taarifa zozote za maofisa wa TRA kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo.
 
Kama huna ushahidi wa kutosha utaambiwa wakati yanakamatwa kampuni ilikuwa ilishauzwa kwa watu wengine!
 
Bei ya hisa 1000 jumla ya hisa 10000 hivyo mtaji ni 10,000,000/=
Mzigo uliokamatwa ni 1.4bil
Does this sound?
 
Khaaaaaa CCM oyeeeeeeee sisi wote wasafi hakuna haja ya kuonyesheena vidole ndio maana tumechaguana kurudi mwenye NEC...Thithiem Bhana
 
Asante kwa taarifa, ingawa tayari kuna nyuzi humu za siku za nyuma zilikuwa na taarifa nene zaidi. Kifupi ni kuwa Kinana, kama EL, JK, RA, AC, NK na wengine wengi ni mafisadi wazoefu.

Kinana alifanya ufisadi toka enzi za Mwinyi na kwa sehemu kashfa alizozipata zilimnyong'nyeza na ndio maana akaamua kujikita kwenye ngome salama yaani chamani.

Kwa hulka na wasifu Kinana ni mbunifu na pia ni msomi mzuri tu, na ndio maana hata mikakati mingi ya CCM amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wazalishaji wake. Lakini hana sifa ya uadilifu na misingi ya uzalendo. Suala la Wasomali na uhamiaji/biashara haramu naye ni mmoja wa wafadhili wake. Kifupi Kinana haifai Tanzania ya leo wala Tanzania tunayoitaka kesho.
 
Inaonekana ni marufuku kwa TRA kukagua mizigo inayopitia Sharaf Shipping.
 
Hawa huwa hawaitiji Source labda ingekuwa habari inawahusu Chadema ndio watu wangeomba Source.
hivi Ritz wakati mnampa kinana wadhifa wa kichama hamkujua uchafu alionao?
Au mliamua liwalo na liwe?
 
Bei ya hisa 1000 jumla ya hisa 10000 hivyo mtaji ni 10,000,000/=
Mzigo uliokamatwa ni 1.4bil
Does this sound?
It does. Sio lazima hisa ziwe reflected kama working capital au business networth. Ndio maana kuna financial facilities kama bank overdraft, invoice credit, loans etc.

Badala yake naomba tujiulize yafuatayo:-

- Kwa vile yeye anamiliki kampuni au chombo kama kile ili-hali ni ofisa wa ngazi ya juu ktk uongozi wa nchi hii (kupitia CCM) je maadili ya uongozi hapo yako wapi? Hasa kwenye kubeba nyara za Taifa?

- Huo mgongano na mkanganyiko wa maslahi ni kwa faida ya nani? Na ni kwa hasara ya nani?

- Je Rais na M/kiti wa CCM alipomchagua majuzi kuwa party GS (hasa tukizingaitia ushiriki wa wazi wazi wa TISS ktk siasa za CCM), hakuwa anayajua haya na mengine? Je kwanini Kinana leo ni Katibu Mkuu wa CCM katikati ya yote haya?

- Je ni nini hatima ya nchi katika mazingira na uhalisia kama ulivyo?
 
Wacha unafiki na umbea kijana.Source yenyewe hujaweka unapayuka tu mdomo.Na isitoshe pembe za ndovu zilizokamatwa huko zote zimetoka Congo.
 
Sasa jamani investigation za namna hii zinatoa hint tu ila huwezi kum-pin mtu down to earth

1. Je haruhusiwi kuwa na kampuni..............????

2. Mzigo ulisafirishwa na kampuni yake..........cha msingi wakala huwajibika kukagua mzigo kabla ya kuukubali.....wadau wa hii sekta mtupe maujuzi plz...????

3. Umesema TRA ndo wanaweka seal ya mwisho .........implication ni kwamba umemtoa kwenye kosa la msingi atasema mpaka mzigo unaondoka kulikuwa na plastic na TRA walithibitisha hilo ??? Vp kama nyara ziliwekwa melini kabla ya upakiaji halafu safarini watu wakapiga maujanja na kurudishia seals????

4. Mfanyakazi wa kampuni yake hana kibali cha kufanya kazi.......kuna HR officer hapo so yeye atakubali collective responsibility na kutoa uamuzi hata wa kumfukuza kazi.....kampuni ikiwa sued itaweka wakili na yeye atabaki huru kama AK.........bado simpati mkononi......tusaidiane kumkamata.

Mytake; Heading ilivyowekwa ni kama kampuni ya huyu mtajwa ipo moja kwa moja ready handed kumbe ni mlolongo wa matukio na ubovu katika usimamizi wa kutoa mizigo nje ya nchi....ambayo inatia hasara kwa taifa kuliko the fact kwamba kampuni ni ya nani

Sasa motive ilikuwa;
1. Ku highlight weakness ya utaratibu wa kusafirisha mizigo???
2. Kumuhusisha mmiliki na mzigo???
3. Hasara inayopatikana kwa uzembe huu???
4. Ku doubt integrity ya muhusika???
5. Au bora kuna jina la mkubwa basi ni habari???

Sina nia ya kutetea uovu ila ni vema kujenga tabia ya kuwa na uandishi ambao mwisho wa habari kila kitu kinakuwa kimejipambanua na unaweka facts basi mtu anabaki kweupeee mchana wa jua kali then tunajua ukweli wake na
kumuweka kundi husika...Imagine uandishi wa Kubenea ......tujitahidi kufika katika level ile.....then tutakuwa tumeapata silaha nzuri na ya kudumu juu ya kadhia nyingi sana..............

S
 
Mnataka source gani hapa nyie? Kashasema Anne Kilango akiongea bungeni manake maelezo yapo kwenye hansard na kuhakikisha kuwa kampuni ni ya kinana ametaja source kuwa ni brela kawapa na certificate no. Mnataka nini? Ndugu yangu Ritz atakuwa anaota Chadema
 
Back
Top Bottom