Hii ndiyo heshima ya ng'ombe pamoja na upumbavu wa kuku

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Ng'ombe, akishatoa maziwa ya kulisha familia nzima, hurejea katika malisho yake taratibu. Lakini kuku, akishataga yai moja hupiga kelele ili kila mtu ajue. Je! Yai hilo alilotaga laweza kutosha hata kwa mlo wa mtu mmoja? Jibu ni hapana.

Katika maisha kuna watu wa aina 2 kuna wale wanaofanana na Ng'ombe na wale wanaofanana na Kuku.

Mtu afananaye na kuku akikusaidia jambo hata kama ni dogo sana atasema kila mahali ili watu wote wajue jambo hilo. Kama ni kazini/msikitini, nyumbani etc atahakikisha anajisifu sana na kuisambaza ile habari kwa wengi. Kuna watu walisaidiwa na watu hawa wenye tabia ya kuku baadaye wakaishia kuumizwa mioyo yao baada ya kusambaa kwa habari hiyo.

Mtu mwenye tabia ya kuku akitoa msaada hata kwenye kituo cha watoto yatima, au akisaidia maskini anatamani aje na waandishi wa habari.

Kuna watu wenye tabia ya ng'ombe. Akikusaidia hata kama ni jambo kubwa sana kiasi cha kushindwa kumlipa fadhila, hawezi kukusema na hataki watu wajue. Furaha yake ni kukuona unavuka salama na unafanikiwa. Watu wa namna hii hupata thawabu kubwa. Tamani kuwa na tabia kama hii ya kusaidia bila kujitafutia utukufu.

Muwe na jioni njema*
 
jamani za asubuhi naomba kwa mwenye kuku mbegu nzuri yakienyeji tuwasiliane awe maeneo ya tabata nahitaji mbegu kubwa ya kienyeji
 
Back
Top Bottom