Hii ndiyo hali ya mfumo wa afya Tanzania - Jionee tulivyo katika hali ngumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo hali ya mfumo wa afya Tanzania - Jionee tulivyo katika hali ngumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mawazo mbishi, Apr 3, 2012.

 1. mawazo mbishi

  mawazo mbishi Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Tz ina Madaktari wa upasuaji wa mfumo wa fahamu (neuro surgeons)-3
  Madaktari wa moyo ( cardiologists)-5
  Madaktari wa figo (nephrologists)-3
  Madaktari wa mfumo wa fahamu (neurologists)-2


  Nchi nzima ina machine 7 za Hemodialysis za kusafisha figo kwa watu wenye renal failure, na zinazofanya kazi ni 4 na hizo nne zinatumiwa na watu watatu au wanne tu. Nchi yetu inakadiriwa kuwa na wagonjwa zaidi ya laki moja wanaohitaji dialysis...maana yake ukipata tu renal failure maana yake we umeshakufa...

  leo hii ukipata renal failure, ambayo wengi wanapata kuafanyiwa dialysis mara moja tu ni sh 200,000 na unahitaji kufanyiwa mara tatu kwa wiki...!!!!

  Hospitali zote za mikoa hazina madaktari bingwa na zile ambazo wapo ni mmoja mmoja, nao ni viongozi hawatibu watu.

  Hebu niambieni hawa watanzania milioni 40 wanapata wapi hizi huduma, hivi tuna justification viongozi wetu kutembea na VX..!!!!!

  Inasikitisha kuona bado tuna mazingira kama haya, na tunatumia mamilioni ya pesa kuwapeleka vigogo wetu wakatibiwe nje ya nchi kwa hela zetu za kodi. Nadhani madaktari waliposema pamoja na mabo mengine wanapinga wagonjwa kupelekwa nje ya nchi walikuwa sahihi hasa ukizingatia wanaopata nafasi kwa kipaumbele ni viongozi wakifuatiwa na ndugu na jamaa zao, na wale wanaoweza kuilainisha machine nadhani hapa naeleweka, ila wewe mlalahoi ukiugua basi ndugu zako waanze tu taraibu za kukuaga....!!!

  Naona aibu kwamba tuna miaka 50 tangu uhuru..na tuna rasilimali nyingi kama Taifa...!!!!nimetafakari kwa kina taarifa hizi na nikaona wataalamu wetu walikuwa na hoja ya msingi walipoamua kuingia katika mgomo
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa hii. Lakini serikali imechaguluwa na wananchi hawa
   
 3. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nawafahamu baadhi ya madaktari wa moyo na madaktari wengine wa kitanzania wanaofanyia nje ambao wangekuwa msaada mkubwa sana kama wangeamua kurudi nyumbani.
  Lakini mkuu hizo data zako za madaktari specialists nadhani ni wale walioajiriwa serikalini tu,hukujumlisha na wale wa private,au?all in all hali ni mbaya na inasikitisha sana.Tatizo ni ubinafsi na kutojua vipaumbele vyetu kama nchi
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  That is frightening!
   
 5. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Safi serikali yetu haina wagonjwa ndio maana jaman madaktari hawana umuhimu
   
 6. m

  mubi JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Iam going to work on this though Iam not a politician. Not only this even O and gyenacology in villages. Nitakuja na mifano halisi inayoonekana.
   
 7. c

  collezione JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Madaktari walivyogoma. Si mliona vichekesho. Ngoja sasa muone mambo ya CCM.
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu, ambao wanapaswa kulaumiwa ni sisi wananchi kwa kuendelea kukubali kutawaliwa na awa majambazi.
  Jana nilishangaa sana ni kwa nini ccm walipata kura 26,000 hapa ndo utapiwa ujuwa wa wananchi...
   
 9. mawazo mbishi

  mawazo mbishi Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Hao ndiyo madaktari walioko TZ, hospitali binafsi zinaendeshwa na hawa hawa mkuu, leo nenda Ahga kaulize kama Neuro Surgeon pale kama hawajakuambia watamuita kutoka MOI.

  Tena ili kukuonyesha hiyo hali ilivyo zaidi hao wa moyo na figo wote wako Muhimbili, wa upasuaji wa mfumo wa fahamu wote wako MOI. kwa hiyo hata ukienda pale hospitali ya rufaa Mbeya hawapo.

  Wagonjwa wenye matatizo ya figo wanapata huduma ya dialysis Regency lakini hakuna daktari bingwa wa figo hapo, kwa hiyo wanakwenda kliniki muhimbili na kufanya dialysis regency, ukiwa na tatizo la figo Bugando hautapata msaada wowote kwa kuwa hakuna wataalamu wala machine za kukusaidia.

  That's how pathetic it is, nami nilikuwa nadahni hospitali za binafsi zina wataalamu, baadaye nikagundua hawapo kote huko.......!!!!
   
 10. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mie naona mganga aliyeturoga kafa....Otherwise ingebidi tu turudi tukampigie magoti. Maana unashindwa kuelewa kama tunatumia hata chembe moja ya ubongo wetu.
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Source? usije furaha baraza kwa mambo sensitive kumbe unafanya siasa za majitaka
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Imechaguliwa na wachache pia na kujilazimishia kuingia madarakani mfani hai ni uchaguzi wa mwaka 1995
   
 13. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Safi sana ccm buruza hao vilaza wanaokuweka madarakani,
  wanaoichagua ccm wanasumbuliwa na ubinafsi tu
   
 14. JS

  JS JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatari....a lot needs to be done kwenye health sector yetu...a lot
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Hata kama hajawajumuisha mkuu jiulize ni waTZ wangapi wanaweza kwenda kutibiwa hospital za private?
  ukichunguza sana utakuta wanawatibu hao hao viongozi wa serikali wenye uwezo na sio mtanzania wa kawaida
   
 16. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mpaka tumefika hapa, je kuna mtu anaweza kukumbuka mwaka gani tulipofanya makosa hadi leo kufikia kuyapata matokeo haya? Naogopa janga litakalo kuja kuifika Tanzania kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
   
 17. c

  collezione JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tatizo Tanzania tunaweka siasa hata kwenye mambo ya msingi.

  Tutapata wapi wataalamu, wakati kila siku muhimbili wanafunzi wanapigwa mabomu. Wanafunzi wetu kila siku wanagombana na serikali kutimiziwa mahitaji yao.

  Na badala ya serikali kutimizia watoto mahitaji, wameshafanya siasa...

  Wanafunzi waTanzania wanapoteza mda mwingi kulilia mahitaji yao. Kuliko ku_concentate kwenye masomo. Sasa katika hali kama hiyo unadhani tutapata wataalamu???

  Any way tunaweza piga kelele sana hapa. Wakati mkulu ameshasema yeye yuko na kilimo kwanza,. Mambo mengine yote upuuzu kwake. Ni bora ajisafirie akale upepo wa mbefele...haha
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wana kila wajibu wa kutufanya hivyo kwani wametunyanyasa live na bado tunakuwa hatujui kuwakataa wanapokuja kutuomba kura
   
 19. mawazo mbishi

  mawazo mbishi Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  OOhh, unauliza chanzo......hiyo rahisi tu hauhitaji hizo takwimu, we mwambie rafiki yako yoyote aliyeko Mwanza au Mbeya aende kwenye hizo hospitali za rufaa aseme ana tatizo la figo na anahitaji huduma ya dialysis, you will get your evidence....!!!

  We jua tu siku ikitokea umeugua ghafla ukiwa nje ya Dar, basi hali yako itakuwa ngumu iwapo utahitaji hizi huduma, nadhani huko ni mbali hata ukiwa hapa Dar bado itakuwa ngumu.

  Huduma ya dialysis gharama yake ni zaidi ya Sh laki mbili ni inapatikana hospitali binafsi, Muhimbili kuna watu wanne tu, ndiyo wanapata hii huduma, sasa kama una nafasi fuatilia ujue ni kina nai hao wanaopata hiyo huduma...!!!wengine wote wanapanga foleni Regency au Agha Khan. Uikwa na bahati ukawa mwanachama wa mfuko wa bima ya afya basi mfuko utalipia hayo matibabu, ila wale wasio wanachama wanalipa kutoka mfukoni, na hiyo huduma inahitajika mapaka utakapowekewa figo nyingine. kwa hiyo unahitaji laki 2 mara tatu kwa wiki mpaka utakafanyiwa upasuaji wa kuwekewa figo nyingine, na hiyo huduma ya kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa figo nyingine haipatikani Tz........!!!

  Na hali ni hivyo kwa wenye matatizo mengine mengi.....!!!!
   
 20. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aibu kwetu tunaoendelea kuichagua CCM. Hata kwa sisi tusioichagua, tunawajibu wa kujitolea kuwaelimisha wananchi ili wasiichague tena sisiemu.
   
Loading...