Hii ndiyo dawa ya asili iliyotibu muwasho sehemu za siri ulionisumbua kwa takribani mwaka na nusu.

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
3,030
3,324
Wakuu habari,

Mnamo mwaka 2016 April, nilianza kusumbuliwa na tatizo la muwasho katika korodani zangu.

Niliona ni jambo la kawaida but nikaona linadumu mwezi mzima, ikanibidi niende Hospital ya magomeni. Nilipewa cream ya kupaka pamoja na dawa nyingine za kumeza. Dozi ilikua ni ya siku saba. Baada ya dozi kuisha, tatizo lilipungua na baada ya wiki moja likarudi tena.

Nikakwenda zahanati moja sinza. Nikapewa dawa tena ya kupaka na kumeza. Dozi ya wiki mbili. Bado mchezo ukawa uleule. Linapungua na kurudi.

Tatizo liliendelea kunisumbua miezi na miezi. Niliamua kwenda Hospital ya Kairuki, nikapewa dozi ya mwezi mzima, sikupona, nikarudi wakanjrudishia dozi ya mwezi mzima sikupona. Kimsingi Kairuki nilikwenda mara nyingi mno bila mafanikio na huku nikiwa nimepewa dozi ya kila aina.

Nikaanza safari ya kwenda Muhimbili Hospital, kule nilipimwa FBP(full blood picture), HIV na vipimo vingine vingi. Nikapewa dozi pia sikupona. Nikahuduria pale miezi kadhaa pia sikupona. Nikashauriwa nimwone daktari wa ngozi.

Yaani korodani zilivyokua zinawasha, nilikosa amani. Zilibadilika rangi nakuwa na weupe fulani hivi.

Nikarudi tena Kairuki Hospital kwa daktari bingwa wa ngozi, naye akanipa dawa hizo hizo za kupaka na kumeza. Kimsingi nilipiga routes kwa miezi kadhaa pia kwenda kwa daktari wa ngozi Muhimbili bila mafanikio.

Wakati nilipokua nakwenda Hospital, nilipitia thread kadhaa humu na sehemu nyingine mitandaoni kupata ushauri na namna ya kutibu hili suala. Kimsingi ushauri ni mwingi. Nilijiweka katika hali ya usafi na bila kuruhusu Nywele ziote sehem za siri maana zikianza tu kuota ni balaha. Nawashwa hatari.

Kama ni dawa na cream za mahosipitalini, nilitumia nyingi mno hata sikumbuki idadi bila mafanikio, nikawa nimekata tamaa kabisa nikaona ndo siponi tena kabisa maana ni mwaka karibu na nusu nateseka.

Ikumbukwe kuwa, nilishapandisha pia uzi hapa jamvini kuomba ushauri Msaada: Tatizo la korodani kuwasha kwa karibu mwaka. Kuna mdau mmoja alinishauri kwenye uzi huo nipulizie ile dawa ya kuulia mbu ile ya Rungu au Hit. Kusema kweli nilijaribu na sikupona. But yeye anasema alipona kwa kufanya hivyo.

Sasa mwezi wa saba mwishoni nikawa na search YouTube namna ya kutibu muwasho wa korodani, nikakutana na suggestions ya dawa nyingi mno. Moja ya dawa hizo ilikua ni kupaka Asali Mbichi sehemu yenye inayowasha.

Hapa ndani nilikua nimenunua asali mbichi ya nyuki wakubwa kutoka Tabora. Nilianza kupaka, na ndani ya wiki moja tu, muwasho ulianza kupotea, na sasa haupo tena.

Kwaiyo kama na wewe unasumbuliwa na tatizo kama hili, paka Asali mbichi hakika utapona.

Kuwashwa korodani kunakosesha amani sana.

............
Ngoja nipate chai ya mdalasini na Tangawizi plus asali ndani yake kisha narudi.
 
Kwahyo mkuu ukiwa unawashwa unaweza ukashindwa ata kutiana?

Power of forgiveness
 
Hili tangazo la biashara limekuja kivingine kabisa.
Tangazo hili la biashara linatangaza biashara gani?
Asali? Yeye atanufaikaje kwa mfano iwapo hiyo asali utaiagiza kwa babu yako kijijini aliyovuna kutoka ktk mizinga ya nyuki aliyoirithi?

Acha kuwavunja moyo watu wenye moyo wa kutoa ushauri,
Sio kila mtu anaroho mbaya kama ya kwako...shwaaaiin!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli inashangaza mtu kaleta mrejesho wanadai tangazo
 
Tangazo hili la biashara linatangaza biashara gani?
Asali? Yeye atanufaikaje kwa mfano iwapo hiyo asali utaiagiza kwa babu yako kijijini aliyovuna kutoka ktk mizinga ya nyuki aliyoirithi?

Acha kuwavunja moyo watu wenye moyo wa kutoa ushauri,
Sio kila mtu anaroho mbaya kama ya kwako...shwaaaiin!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukran kwa maelezo mazuri mkuu
 
Wakuu habari,

Mnamo mwaka 2016 April, nilianza kusumbuliwa na tatizo la muwasho katika korodani zangu.

Niliona ni jambo la kawaida but nikaona linadumu mwezi mzima, ikanibidi niende Hospital ya magomeni. Nilipewa cream ya kupaka pamoja na dawa nyingine za kumeza. Dozi ilikua ni ya siku saba. Baada ya dozi kuisha, tatizo lilipungua na baada ya wiki moja likarudi tena.

Nikakwenda zahanati moja sinza. Nikapewa dawa tena ya kupaka na kumeza. Dozi ya wiki mbili. Bado mchezo ukawa uleule. Linapungua na kurudi.

Tatizo liliendelea kunisumbua miezi na miezi. Niliamua kwenda Hospital ya Kairuki, nikapewa dozi ya mwezi mzima, sikupona, nikarudi wakanjrudishia dozi ya mwezi mzima sikupona. Kimsingi Kairuki nilikwenda mara nyingi mno bila mafanikio na huku nikiwa nimepewa dozi ya kila aina.

Nikaanza safari ya kwenda Muhimbili Hospital, kule nilipimwa FBP(full blood picture), HIV na vipimo vingine vingi. Nikapewa dozi pia sikupona. Nikahuduria pale miezi kadhaa pia sikupona. Nikashauriwa nimwone daktari wa ngozi.

Yaani korodani zilivyokua zinawasha, nilikosa amani. Zilibadilika rangi nakuwa na weupe fulani hivi.

Nikarudi tena Kairuki Hospital kwa daktari bingwa wa ngozi, naye akanipa dawa hizo hizo za kupaka na kumeza. Kimsingi nilipiga routes kwa miezi kadhaa pia kwenda kwa daktari wa ngozi Muhimbili bila mafanikio.

Wakati nilipokua nakwenda Hospital, nilipitia thread kadhaa humu na sehemu nyingine mitandaoni kupata ushauri na namna ya kutibu hili suala. Kimsingi ushauri ni mwingi. Nilijiweka katika hali ya usafi na bila kuruhusu Nywele ziote sehem za siri maana zikianza tu kuota ni balaha. Nawashwa hatari.

Kama ni dawa na cream za mahosipitalini, nilitumia nyingi mno hata sikumbuki idadi bila mafanikio, nikawa nimekata tamaa kabisa nikaona ndo siponi tena kabisa maana ni mwaka karibu na nusu nateseka.

Ikumbukwe kuwa, nilishapandisha pia uzi hapa jamvini kuomba ushauri Msaada: Tatizo la korodani kuwasha kwa karibu mwaka. Kuna mdau mmoja alinishauri kwenye uzi huo nipulizie ile dawa ya kuulia mbu ile ya Rungu au Hit. Kusema kweli nilijaribu na sikupona. But yeye anasema alipona kwa kufanya hivyo.

Sasa mwezi wa saba mwishoni nikawa na search YouTube namna ya kutibu muwasho wa korodani, nikakutana na suggestions ya dawa nyingi mno. Moja ya dawa hizo ilikua ni kupaka Asali Mbichi sehemu yenye inayowasha.

Hapa ndani nilikua nimenunua asali mbichi ya nyuki wakubwa kutoka Tabora. Nilianza kupaka, na ndani ya wiki moja tu, muwasho ulianza kupotea, na sasa haupo tena.

Kwaiyo kama na wewe unasumbuliwa na tatizo kama hili, paka Asali mbichi hakika utapona.

Kuwashwa korodani kunakosesha amani sana.

............
Ngoja nipate chai ya mdalasini na Tangawizi plus asali ndani yake kisha narudi.
Ahsante kwa mrejesho. Hongera kwa huo uponyaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom