Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Pamoja na changamoto mbalimbali chaa hiki kilizozipitia, bado kimeendelea kuimarika kila uchao uchwao. Kuna wale wanaobeza kuimarika kwa chama hiki, na kukifananisha na vyama vingine vya CUF na NCCR - Mageuzi, wakidhani kuwa kama ilivyokuwa kwa vyama hivyo, Chadema pia kitaporomoka. Ila watu hawa wanashindwa kuelewa kuwa Chama hiki hakijawahi kupoteza umaarufu wake, na zaidi tu kimekuwa kikiuongeza.
Swala hili linathibitishwa na idadi ya viti vya udiwani na Ubunge ambavyo chama hiki kimekuwa kikivipata katika kila uchaguzi mkuu, tangu 1995. Leo tuangalie tu takwimu fupi za udiwani na ubunge kwa Chama hiki.
Kwa kuzitazama takwimu hizi rahisi, utajifunza kuwa pamoja na hujuma nyingi, wizi wa kura, na fitina mbalimbali kutoka vyama vingine vya siasa (vikiwemo CCM na CUF), pamoja na serikali kutumia vyombo vya dola kujaribu kukiporomosha, bado Chadema kimekuwa kikiendelea kujinyakulia viti vingi zaidi kila kiingiapo katika uchaguzi mkuuna zaidi sana, ongezeko limekuwa likiongezeka kila uchaguzi. Mfano, mwaka 2000 chadema kiliongeza kiti kimoja tu cha ubunge na mwaka 2005 kiliongeza viti sita vya ubunge na mwaka 2010 kiliongeza viti 38 (ukiongeza na vile vya viti maalum). Kwa mantiki hiyo, chadema kimekuwa kikikubalika zaidi kila miaka isogeapo. Wale wenye ndoto kuwa kitakufa, subirini kama hamtakiona kikiingia ikulu na nyie kubaki mnabung'aabung'aa tu.
Kwa wale mpendao grafu, takwimu hizi zinaweza kuonekana kama ifuatavyo. Chadema songeni mbele, hadi mfanikiwe kulikomboa taifa hili. Matumaini ya Watanzania wengi, hasa nguvu ya taifa (vijana), yako mikononi mwenu. Imarisheni umoja, mshikamano, maelewano na mapambano. Hatimaye mtalifikisha taifa letu pale ambapo CCM wameshindwa kwa zaidi ya miaka 50 sasa (nusu karne).

Mwaka | Madiwani | Wabunge |
1995 | 42 | 4 |
2000 | 75 | 5 |
2005 | 103 | 11 |
2010 | 467 | 49 |