Hii ndiyo Agenda ya ACT-Wazalendo kumuombea Mbowe msamaha kwa Rais

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Shabaha kubwa na ya Makusudi ya ACT-WAZALENDO kumuombea Mhe Freeman Mbowe msamaha kwa Rais amsamehe kuhusu kesi yake ya tuhuma za ugaidi inaonekana chama hiki kwa kujua au kutokujua kinataka kutumika kuisafisha serikali ya awamu ya 6 baada ya kuona kua hii kesi inalitia taifa aibu.

Sasa ACT-WAZALENDO wanatumika kuisafisha serikali ili Mbowe aombe msamaha kwa Rais ionekane kuwa alikosa na hivyo ionekane ni kweli alishiriki kula njama za kufanya Ugaidi. Wanajua kabisa kua mbele ya maamuzi ya kisheria hakuna kesi hapo, ushahidi wote mpaka sasa ni shahidi wa 12 hakuna popote panathibisha ugaidi wa Mbowe. Yaani wanataka Mbowe akirinkosa ambalo hakukifanya ili wamgeuke kubwa alifanya makosa ya ugaidi waanze kukiandama chama chake kwa kukipaka matope.CHADEMA wasikubali mtego huu ambao ACT-WAZALENDO ni chanzo tu.

Lengo la ACT ni Mhe Mbowe akubali kuomba msamaha ili aonekane kweli alikuwa Gaidi, hawa hawa ACT-WAZALENDO na CCM watakigeuka CHADEMA na kukiita Chama cha magaidi, watakipaka matope na mwisho wa siku ACT kionekane chama safi na kiweze kuwa chama kikuu cha upinzani.Hii ndiyo Shabaha kuu ya ACT-WAZALENDO.

Naamini CHADEMA ni taasisi imara na ni chama kikubwa ambacho kinaifanya mambo yake kwa weledi na unafiki huu wa ACT wanaielewa vyema.

Alianza Zitto wazi wazi akamuombea msamaha Mhe Mbowe mbele za Rais kitu ambacho CHADEMA wakistuka na kumwakia juu, juzi kafiata mzee Duni bila haya anadai angewa nafasi ya kumuombea Mhe Mbowe msamaha angefanya hivyo kuliko kuendelea kukaa jela. Huu mpango si wa bahati mbaya, CHADEMA wameshaustukia. Wanachofanya ACT-WAZALENDO ni unafki ambao kesho wataujutia mbele za wananchi kwani wao ni chama kichanga sana.

Zitto Kabwe ameamua kuendesha taasisi yake kwa kujipendekeza,kutumika na kujikweza akidhani kuwa wanaweza kufika mbali. Kuwa chama kwa misingi ya uongo na unafki hakuwezi kukufikisha chama chao mbali. Wao badala hata ya kuwaongezea CHADEMA mawakili ili iwe kama kuwatia moyo leo wao wanamuombea Mtuhumiwa Msamaha wa kesi ya Kubumba ili tu apewe jina jipya la Gaidi kisha wao wanufaike.
 
Zitto Kabwe ameamua kuendesha taasisi yake kwa kujipendekeza,kutumika na kujikweza akidhani kuwa wanaweza kufika mbali. Kuwa chama kwa misingi ya uongo na unafki hakuwezi kukufikisha chama chao mbali. Wao badala hata ya kuwaongezea CHADEMA mawakili ili iwe kama kuwatia moyo leo wao wanamuombea Mtuhumiwa Msamaha wa kesi ya Kubumba ili tu apewe jina jipya la Gaidi kisha wao wanufaike
 
Uzuri ni kwamba kamanda Mbowe alishaweka wazi kuwa hata omba msamaha kwa sababu yeye hana kosa

Pia ni udhaifu mkubwa kuomba msamaha wakati huna kosa, na ni kumpa bichwa (credits) Bi. Mikopo; kisa cha Speaker Job Ndugai ni mfano tosha

Baada ya Speaker Job Ndugai kujichanganya kwa kuomba msamaha Bi. Mikopo akapata nguvu na kujitokeza hadharani kumsema Speaker na kufanya aliyofanya ya kumuondoa kwenye nafasi ya u-speaker
 
Shabaha kubwa na ya Makusudi ya ACT-WAZALENDO kumuombea Mhe Freeman Mbowe msamaha kwa Rais amsamehe kuhusu kesi yake ya tuhuma za ugaidi inaonekana chama hiki kwa kujua au kutokujua kinataka kutumika kuisafisha serikali ya awamu ya 6 baada ya kuona kua hii kesi inalitia taifa aibu...
Hakuna cha msamaha hapo, kipute kinaunguruma mahakamani, wacha kiendelee hadi mwisho ili wote tushuhudie ukweli wa mambo!
 
Kwa tunaomfahamu ZZK, yupo hivyo. Na uzuri hana uwezo wa kujificha.
ccm = act.
Bila shaka ZZK alijua mashtaka dhidi ya Mbowe yataisambaratisha CDM na yeye angevuna wanachama wapya!
#MunguFundiSana!

NB: Kwa mwenendo wa kesi ulivyo Mbowe akiomba msamaha nitajiona mjinga sana!
Kesi mwanzoni ilidhaniwa kuwa ni ya kigaidi. Ilivuta hisia toka pande zote za dunia na wabobezi.
Ikakolezwa na IGP na Bi Mchele!
Kwa sasa imebainika ni ujinga wa scripts za Kingai, Urio na Sabaya!
Hivi how comes ujinga huu ulipenyezwa hadi Ikulu kwa Bi Mchele na mahakamani??
 
Ushahidi kaja nao Luten Urio na umeomba mahakama ipokee kielelezo chake kama kwa utambzi.

Amefichua siri ovu ya Freeman A. Mbowe ya kutaka kuleta taharuki nchi nzima na kutaka kuchukua dola vyovyote vile. Alienda mbali zaidi kwa kufichua hila na njama za Mbowe za kutaka kudhuru na kushambulia viongozi wa serikali,kukata miti Morogoro to Iringa na kuchoma moto vituo vya mafuta(sheli).

Serikali imempongeza sana kwa uzalendo wake kwani ukiachilia waliopigania taifa letu dhidi ya adui yetu Amin Nduli Dada,basi huyu ndio mfano mwingine wa uzalendo wa kuigwa. Pamoja na kuwa promoted kutoka Koplo wa VV hadi Luten wa ** hii ni zawadi ndogo kati ya zile kubwa atakazotunikiwa endapo tukio hilo litazimwa na wahusika kuishi maisha ya jela katika kipindi chao chote kilicho bakia cha maisha.
 
Ushahidi kaja nao Luten Urio na umeomba mahakama ipokee kielelezo chake kama kwa utambzi.
Amefichua siri ovu ya Freeman A. Mbowe ya kutaka kuleta taharuki nchi nzima na kutaka kuchukua dola vyovyote vile...
Unatumia makalio kufikiri, mzalendo anaweza kusafiri kwenda mpka Morogoro akawakusanye magaidi awape hela na kuwasafirisha ili hali yeye asiwepo ktk njama hizo za kuufanisha huo Ugaidi?

Hivi umejiuliza Kama kweli wale ni magaidi kabla ya kwenda huko Arusha wangelipua mabomu hayo maeneo ya soko hapo
Morogoro au ktk magari waliyo safiria?

Urio anawezaje awe shahidi badala ya kuwa mtuhumiwa namba moja? Yeye ndiye aliye wapa fedha na kwa maana nyingine hao watuhumiwa wasinge kamatwa Kama Ulio asinge watafuta na kuwaeleza kuwa Kuna kazi na wala hakuwaambia wanaenda kufanya Ugaidi.

Usiwe Kama kasuku wewe Kibwetele.
 
Unatumia makalio kufikiri, mzalendo anaweza kusafiri kwenda mpka Morogoro akawakusanye magaidi awape hela na kuwasafirisha ili hali yeye asiwepo ktk njama hizo za kuufanisha huo Ugaidi...
Mimi nimefupisha ya jana kwani kosa langu lipi hapo? Kumlaumu wakili wa serikali na mwendesha mashtaka maana wao ndio mastermind wa haya yote. Usipende saana kumshambulia mtu bila kumwelewa anamainisha nn,soma uelewe na uanze kule niliko quote
 
ACT wazalendo kwa sasa ni skin tight ya kuficha aibu za Serikali zisionekane.
MhtaG.jpg
 
Naamini CHADEMA ni taasisi imara na ni chama kikubwa ambacho kinaifanya mambo yake kwa weledi na unafiki huu wa ACT wanaielewa vyema.
CHADEMA Ina akili kuliko chama chochote Cha siasa Tanzania na nje ya Tanzania. What Chadema can see seated, CCM can not see standing
 
Acheni kuipaka matope Act na kiongozi wake ndugu Zitto.

Zitto alifanya hayo kwa nia njema ila kiongozi mwenzake wa upinzani awe huru maana hata yeye anaamini hii kesi ni ya kumkomoa tu Mbowe.
 
Unatumia makalio kufikiri, mzalendo anaweza kusafiri kwenda mpka Morogoro akawakusanye magaidi awape hela na kuwasafirisha ili hali yeye asiwepo ktk njama hizo za kuufanisha huo Ugaidi...
Hakika umenena,Urio ni mshitakiwa No 1 yeye ndiye alikuwa anawalipa pesa magaidi,Mbowe alitakiwa awe shahidi wa serikali kumtumia pesa Urio kwa matumizi ya walinzi lakini Urio alizitumia kuwapa mafunzo magaidi.

Urio wakuu wako wakikosi walijua kuwa umesafiri kwa kazi za Mbowe? au za DCI
 
Acheni kuipaka matope Act na kiongozi wake ndugu Zitto.

Zitto alifanya hayo kwa nia njema ila kiongozi mwenzake wa upinzani awe huru maana hata yeye anaamini hii kesi ni ya kumkomoa tu Mbowe.
Yaani gaidi anaachiwa kwa kuomba msamaha?
 
Shabaha kubwa na ya Makusudi ya ACT-WAZALENDO kumuombea Mhe Freeman Mbowe msamaha kwa Rais amsamehe kuhusu kesi yake ya tuhuma za ugaidi inaonekana chama hiki kwa kujua au kutokujua kinataka kutumika kuisafisha serikali ya awamu ya 6 baada ya kuona kua hii kesi inalitia taifa aibu...
Hebu tusiwahukumu ACT
 
Mm nimefupisha ya jana kwani kosa langu lipi hapo? Kumlaumu wakili wa serikali na mwendesha mashtaka maana wao ndio mastermind wa haya yote. Usipende saana kumshambulia mtu bila kumwelewa anamainisha nn,soma uelewe na uanze kule niliko quote
Hajakuelewa. Mpotezee tu
 
Back
Top Bottom