Jef Kirhiku
Member
- Dec 10, 2016
- 39
- 76
"Elimu ni silaha yenye nguvu katika kuleta maendeleo kuanzia ngazi ya familia mpaka katika jamii kwa ujumla ".
Tathmini ya matokeo ya kidato cha nne Singida mjini
Na Japhari Saidi Mtoro.
Nimejaribu kufanya tathmini ya hali ya elimu Singida mjini kupitia matokeo ya kidato cha nne na kugundua hali ni mbaya na hivyo ni vigumu kupata maendeleo ya haraka na endelevu .
Jumla ya wanafunzi 1,296 walifanya mtihani katika shule 16 za kata Wilayani Singida mjini .
Kati ya hao wanafunzi 7(0.54%) wamepata div one ,65(5.02%) wamepata div two,154(11.88%) wamepata div three ,590(45.52%) wamepata div four na 480(37.04%) wamepata div Zero .
Waliopata kati ya div I-III ni wanafunzi 226(17.44%) huku waliopata kati ya div IV-O ni 1,070(82.56%).
Div one nyingi zaidi(6) zimejitokeza Katika shule ya Dr Salmin ikifuatiwa na chief Senge (1) huku shule 14 zilizobaki hakuna div one hata moja .
Zero nyingi Zaidi zimeonekana katika shule ya Chief Senge (57) ikifuatiwa na mungumaji(55) pamoja na Ipembe (55). Hakuna shule yeyote ambayo haina Zero.
Tafsiri yake ni kwamba tunaingiza vijana wengi zaidi wenye ufaulu hafifu au waliofeli kabisa katika ushindani wa kupata fursa za kujiendeleza kitaaluma au soko la ajira na uchumi kwa ujumla .
Hatuwezi kupata maendeleo ya haraka na endelevu kwa hali hii ya elimu na sifa hizi za vijana wetu wanaoingia nazo katika soko la ajira na uchumi pamoja na ushindani wa fursa za kujiendeleza kitaaluma.
Hii ni changamoto kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali ,wazazi na wakazi wote wa Singida mjini.
Ni muhimu kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kubadili hali hii kama Sharti muhimu la kupata maendeleo ya haraka na endelevu .
Tunapaswa kuwekeza zaidi katika elimu ya vijana wetu .
Mwisho wa mtihani mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya mtihani mwingine .
Tutakiane kila la kheri katika kukabiliana na changamoto hii .