Tangu rais Magufuli aingie madarakani 2015 amekuwa akithibitisha kwamba maamuzi waliyofanya watanzania ya kumchagua kuwa kiongozi wao hawakukosea, ni maamuzi ya hekima naye hatuangushi. Pia, anaendelea kututhibitishia kuwa kesho ya Tanzania ni nzuri kuliko jana. Kesho ya Tanzania imejaa mambo mazuri ya kufurahisha ambayo kila mtanzania anatamani kuwa mbele ya wakati kuona kesho ya Tanzania kuna nini.
Kama utakubaliana nami nina uhakika unaiona kesho ya Tanzania kama ninayoiona mimi. Mimi naiona kesho ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya watu kujifunza uongozi wa mfano na wa msimamo ambao Rais Magufuli anautumia katika kuletea nchi na wananchi wake maendeleo. Hii ndio kesho ya Tanzania ambayo rais wetu anataka iwe na naiona ikiwa hivyo.
Kesho ya Tanzania itakuwa ni hazina ya kudumu ya watanzania juu ya Amani, utu, umoja na mshikamano katika kuleta maendeleo. Kesho ambayo watanzania watakuwa waadilifu, watiifu na wazalendo kwa nchi yao inajengwa leo na rais Magufuli.
Kesho ambayo kutakuwa na siasa za kishindani na zisizofuata misingi ya ubaguzi wa rangi, dini, kabila na kanda. Hii ndio kesho ambayo rais wetu anataka iwe na tunaiona inavyokuwa kwa kasi na vyama vyenye misingi tajwa hapo juu tunaona vikipukutika na kupukutisha wanachama kama mti kipindi cha kiangazi.
Kesho ambayo huduma za kijamii kama elimu, maji, afya zitapatika kila sehemu katika nchi yetu na kwa gharama nafuu sana ndiyo inayotengenezwa na Rais Magufuli leo kwa damu na jasho ili itimie.
Kesho ambayo bajeti yetu itategemea wahisani kwa kiwango kidogo sana, uzalishaji kukua maradufu kutokana na kuwepo kwa wataalamu wengi kwa kila sekta, viwanda ndio kuwa nyenzo muhimu katika maendeleo yetu ndio naiona ikitengenezwa na rais Magufuli leo.
Kesho ambayo wafanyakazi watafurahi kwa ongezeko kubwa la mishahara, wakulima watafurahi kwa kuwepo kwa soko la uhakika la mazao yao,wavuvi, wafugaji nao hali kadhalika ndio itakuwa Tanzania.
Kesho ambayo mimi raia wa kawaida kabisa nitakuwa nasafiri kwa SGR ama ndege kwa gharama nafuu kabisa. Kesho ambayo miundombinu ya barabara, madaraja itakuwa kila sehemu nchini ndio ninayoiona.
Mimi naiona kesho ambayo kila mtanzania atakuwa na furaha sana na kuienzi jana ambayo ndio hii ya leo ambayo baadhi wanaidharau. Tuwe wamoja katika kuijenga kesho yetu kwa sababu tuna kiongozi ambayo yupo tayari kutuongoza kufika huko na kwa uweza wake Mungu tutafika. Hii ndio kesho ya Tanzania niionayo, je wewe waona kesho ya namna gani?