Hii ndio tafsiri halisi ya siasa kwa mtu wa kawaida kama mimi

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Ukitaka kujua maana halisi ya siasa na uongozi na hasa unapokuelezea mtu anayekuwa na unafiki mwingi au wa kujipendekeza kujipendekeza muulize maswali haya machache

1. Swala la uchumi kukua
i. Miaka mitatu iliyopita bei ya cement, NONDO, sukari na mafuta ilikuwa kiasi gani. Je sasa iko kiasi gani?.
ii.Je thamani ya pesa yetu imeimarika kiasi gani kuleta unafuu kwenye kununua bidhaa tusizozalisha hapa nchni.
iii. Bei ya umeme na maji zina unafuu gani kwa mtanzania kuzimudu.
iv. Gharama za elimu inayompa mtu ujuzi hasa ufundi na vyuo zinaunafuu kiasi gani.
V. Kwenye swala la ajira rasmi na zisizo rasmi ni wangapi wamepewa au kujaengewa uwezo.

2. Kwenye afya
i. Je upo unafuu kwenye gharama za matibabu na makundi maalum
ii. Watoa huduma wa afya wanahudumia vipi. Wanasaidia kwa moyo.
iii. Vituo vipya vingapi vinafunguliwa na kuimarishwa.

3. Kwenye haki
i. Je mahakama zetu zina uhuru kiasi gani.
ii. Kesi za kubambikwa kwa wananchi vipi
iii.chaguzi zetu zinafanyika kwa kujibu wa sheria zetu na kiwango cha utosherevu wa haki ukoje.
4. Kwa watumishi wa umma.
i. Haki za watumishi zinazingatiwaje ikiwa pamoja na promotion na nyongeza ili kukabili ongezeko la gharama za maisha?
ii. Uwiano wa mishahara kwa watumishi wa kada moja na mwajiri mmoja na mlipaji mmoja ukoje.
iii. Watumishi wanajitoa vipi kutumika kutoka na mbinu za uongozi zilizopo.

5. Usalama
i. Usalama na utulivu upo kiasi gani ukilinganisha na awamu zingine?
ii. Maafisa usalama wanaheshimu vipi wananchi na kuzuia uhalifu?
6. Uhuru wa kujieleza.
i. Je uhuru wa kujieleza kwa mujibu wa katiba ukoje.
ii. Wananchi wana uwezo gani wa kuwawakilisha viongozi.

Katika haya ukiona kiongozi anapata asilimia zaidi ya hamsini mpe kura yako tena. Hiyo ndio tafsiri rahisi ya siasa na sio si hasa
 
Back
Top Bottom