Hii ndio serikali ya ubungo mataa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndio serikali ya ubungo mataa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 20, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  SERIKALI YA UBUNGO MATAA

  Nilikuwa kwenye kituo cha basi ( standi ya mkoa ) asubuhi nikasimamisha taxi ambayo ilikuwa inatokea ubungo kwenda shekilango , nilipoingia ndani ya gari mara vijana 2 wakaja , mmoja akaaa nyuma ya gari yule wa mbele akamfuata dereva akamlazimisha ampe shilingi 500 za kupakia , dereva akabishana nae lakini mwisho akampa , tulienda na gari mpaka magomeni ndio dereva akashituka tairi la nyuma moja halina upepo .

  Wakati anabishana na wale vijana mmoja alaingiza spoku kwenye tairi moja ya gari kama adhabu yake ya kubishana wakati wa kutoa pesa , kama wasipofanikiwa kutoa upepo basi kiongozi wao mmoja anaweza kuja kumchapa makofi dereva , pamoja na unyanyasaji mwingine .

  Hapo hapo wale wanaopanda dala dala wanajua vituko wanavyokutana navyo kama vijana wengine wanaokaa kituoni hapo zaidi ya masaa 2 kusubiri gari wanapopata hilo gari anaweza kwenda kushuka kituo kinachofuatia zaidi wanapenda kushuka mahakama ya ndizi au manzese tiptop , wakishafanya hivyo ujue ndani ya ya gari lazima kuna mtu atakuwa kaibiwa mali yake .
  Kuanzia Asubuhi na mapema kuna kuwa na wafanyabiashara mbali mbali eneo la ubungo mataa , muda wa asubuhi wengi wa wafanya biashara ni wale wa magazeti na vifaa vidogo vya magari ambavyo ni rahisi kubebeka pindi askari wa jiji wanapovamia eneo hilo , kuna wengine wanaouza vocha za simu , kuna matapeli na kila aina ya wafanyakazi .

  Wale wote wanaofanya kazi za kuuza magazeti wenye vibanda vyao , wale wanaotembeza njiani , hutakiwa kulipa karo Fulani , sio kwa serikali bali ni kwa watu wengine ambao wachukua wajibu huo wa kukusanya hayo mapato bila ridhaa ya serikali , mfano mwenye kibanda cha magazeti huwa analipa kuanzia 500 mpaka 800 kwa siku .

  Madereva wa taxi ambao hupaki magari yao karibu na eneo hilo nao hutakiwa kulipa karo kwa siku , vile vile hao wanaochukuwa makato hao ni wababe wa maeneo hayo ambao wakishafanya uhalifu huo wanaenda kujificha katika mto ambao uko karibu na njia panda ya chuo au nyumba za karibu na mataa .
  Vijana pamoja na madereva wakikataa kutoa hizo pesa ni kupigwa , wanapopeleka malalamiko yao kituo cha karibu yaani ubungo standi , wahalifu hawa huwa wanakamatwa na kuachiwa baada ya dakika chake na tatizo huja kwa Yule ambaye alimpeleka mhalifu kutuo cha polisi atakuwa hana amani na eneo hilo tena ni kupigwa na kufanyiwa visa vingine .
  Kundi hili la vijana linaongozwa na watu 2 mmoja anaitwa Hemedi pamoja Tembo , hemedi ni mwenyeji wa maeneo hayo ya mataa inasemekana baba yake ana nyumba eneo hilo , na yeye ndio kiongozi wa kuendesha vipigo kwa wale ambao hawalipi hizi pesa .

  Kama nilivyosema huko juu hawa wanaopigwa na kulipishwa pesa hawadiriki kwenda tena kutuo cha polisi kwa sababu ya usalama wao , basi pale pale kituoni kuna maaskari ambao wanapokuwa na njaa huenda kwa vijana wengine ambao kazi yao ni kuuza vipande vya sabuni vilivyo mfano wa simu .
  Hawa askari kanzu wanajua kabisa sasa hivi Fulani ameshauza simu nae anaenda kupata mgao wake , na ndio hawa hawa unapouziwa simu bandia unapeleka kesi kwao .

  Biashara ya simu za sabuni mara nyingi zinakuwa na watu zaidi ya 3 , kuna mmoja ndio mwenye simu halali na ndio mmiliki wa simu , huyo ukimwona ni mtanashati amependeza anaishi mjini kwa shuguli hizo kukodisha simu yake kwa hawa vijana , halafu kuna wengine kazi yao kuangalia kama kuna yeyote anayewaona wanaitwa site mirror , halafu kuna Yule ambaye ndio ameshika simu bandia ni watu wenye uelewano mkubwa sana .

  Kama wamekuuzia ukafanikiwa kuondoka ukashituka mbeleni bahati yako mbaya au nzuri ila kama wamekuuzia ukawapa hela ukashituka pale pale manaa yake unaweza kugeuziwa kibao wewe , ukapigwa na kuitwa mwizi , unaweza hata kuchomwa moto .

  Hii ndio serikali mpya ya ubungo mataa – wahusika wachukue hatua dhidi ya makundi haya yanayozidi kuchipuka kila mara
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Magari ya kwenda Kijiwe Samli kule Kiwalani huwa yanakumbana na adha ya vijana wa namna hiyo pale Bom Bom. Cha ajabu makonda wa magari hayo wameshaona ni kawaida kutoa 'ushuru' kwa mateja wa pale, na ukiwauliza dereva/konda kwa nini mnawapa hela hao jamaa bila ya wao kufanya kazi yoyote, jibu utakalopewa ni kwamba heri kutoa sh. 200/= kila route kuliko kuchomwa na bisibisi !!
   
 3. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2009
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mungiki huwa wanaanzishwa kwa namna hii,hawa wahalifu wanaanza kama mateja ila baadaye watu wenye nguvu na ushawishi hujiunga na kufanya uhalifu mkubwa zaidi. kuna mahali hawa jamaa huwa wanakuahidi ulinzi kama utashirikiana nao vizuri,kwa maana hakuna kundi lingine la uhalifu litakalokubugudhi.....hatua hii ikifikiwa walipa kodi wataongezeka na makundi haya yatamiliki silaha na kama wanashirikiana na polisi then ukienda polisi unaumia zaidi...viongozi wetu hawana sababu ya kupuuza uhalifu huu wa kimakundi athari zake ni kubwa sana mbeleni kama utaachwa uendelee....
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nahisi kova anajua haya lakini pia inabibi ktk mitaa tuwe na walinzi wanaolipwa na serikali za mitaa kwa michango ya wananchi.
   
 5. G

  Gofu Zulu Member

  #5
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwakweli hali ni mbaya sana.Nilikuwa Ubungo nasubiri foleni,natokea Riverside nakwenda Shekilango. Wakatokea hao wazee unaowasema wakachukua Site Mirror zangu zote kwakweli ikanibidi nibaki nawaangalia tu maana kama ulivyoeleza walikuwa na hizo dispisi ukithubutu kutoa kichwa chako wanakuchoma ya tumbo.

  Serikali yetu inayajua haya yote na polisi wanajua sana ila kwakuwa wanachukua 10% zao basi hawawezi kukupa msaada wowote ule.Sijui tufanyeje Wazee hebu tusaidie tutatue hili tatizo kwakweli.

  Tchao.
   
Loading...