Wanajamvi kwanza niwasalimie maana, ni kitambo kidogo sijaingia humu lakini yote ni mema naona mambo yanaenda sawa humu. Kama kawaida great thinkers wanaendelea kupasua vichwa na kuelimisha jamii kwa jumbe zao zenye ujazo, lakini pia na wale fwata mkumbo tusiwasahau nao wanaumuhimu wao.
Basi baada ya salamu hizo niende moja kwa moja kwenye mada iliyonisukuma kuingia humu leo na naamini kwa gt watanielewa tu na wale wengine watanielewa ila kama kawaida hawataacha kubisha.
Hoja yangu leo imejikita katika umuhimu wa bunge kuonyeshwa live. Hili jambo limejadiliwa na watu wengi sana na kumekua na kutofautiana sana ki fikra na mitazamo lakini leo naomba wote tuliangalie hili jambo kwa mtazamo mpana zaidi.
Wabunge tukiachilia mbali hoja kwamba ni watunga sheria na wana wajibu wa kuiwajibisha serikali.......
''Hawa watu ni wawakilishi wa wananchi''. sasa kuna kuna mtua atauliza kwahiyo wakiwa wawakilishi wawananchi ndo waonekane live?
Mbunge anawajibu wa kuhakikisha kwamba, anawasilisha bungeni matatizo na kerio zinazomkabili mwananchi wake ili serikali izifanyie kazi kwa kumuwezesha huyu mbunge yale yanayohitajika katika kukidhi matakwa ya mwananchi aliyemtuma kule bungeni.
Sasa kwanini aonekane live? sababu kubwa ambayo mimi nimeiona ni kwamba, kama mwananchi hatoruhusuiwa kumuona huyu mbunge live ni rahisi sana kwa serikali kutokutimiza yale aliyoiomba kama alivyotumwa na wananchi alafu matokeo yake kwakua mwananchi hakumuona akitoa hoja akaaminishwa kwamba, mbunge wako ni mzembe na hatendei haki unachomtuma.
Madhara ya hii kitu ni kwamba serikali itakapoamua kuwawezesha wabunge wa chama tawala na kuwaminya wale wa upinzani inawezekana kabisa uchaguzi ujao wabunge kutoka upinzani wakawa wachache kuliko tudhaniavyo sasa.
Mbunge ili afanikiwe katika jimbo lake mambo mawili yanahitajika; juhudi binafsi na lakini pia serikali.
Hivyo basi hili swala la bunge linaweza likawa ni mkakati kabisa wa kuudhofisha upinzani hasa kwa serikali kuhakikisha kwamba, maeneo yote ambayo upinzani umeshikilia hayapewi kipaombele cha maendeleo na hii itakua fimbo kipindi cha kampeni. Lakini wananchi wakipewa uhuru wa kuona ninini wabunge wao wanawasilisha bungeni watahukumu kwa haki siku ya mwisho.
''Usipoona kwa macho kila utakachoambiwa utasema ni sawa''Ni mtazamo wangu sijui wewe unaona nini