Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

RaiaMbishi

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
252
124
Binafsi nimekuzwa na kulelewa na mzazi mmoja ambaye ni mama, sijawahi pata hata mapenzi ya baba nilipokuwa mwana.

Kulea mtoto binafsi bila msaada wowote ilikua ngumu sana kwa mzazi wangu lakini alijifunga shuka kiunoni na kutosalimu amri ya uvivu.

Kwakweli malezi ya mzazi mmoja pekee yana changamoto nyingi sana kwani kila jukumu la mtoto linasimamiwa na mzazi huyo huyo tu haswa haswa wakati ambapo mzazi huyo hana uwezo wa kumlea mwana huyo.

1580366135199.png

Mara nyingi huenda mzazi huyo akakumbwa na huzuni ambayo inaeza mwathiri mtoto wake kisaikologia. watoto huwa na tabia ya kufanya na kutii wanachokiona. Basi tabia ya mzazi inaeza mdhuru mwanawe.

Kwa sana mzazi yule anaenda kutoa hasira zake kwa mtoto, wakati mtoto huyo hana hatia. Hii huleta huzuni nyingi kwa mwana na kumpa mafikira ya kuwa hapendwi, ama hua anahisi kama yatima.

Wewe kama mzazi unayelea mwana wako ukiwa peke yako, mbali na sababu zake huna ruhusu kumfokea mwanao bila sababu au kumchapa ovyo ovyo. Na wakati huyo mtoto amefika umri wa kubalighi basi unaweza mweleza sababu zilizofanya akuwe mtoto wa kulelewa na mzazi mmoja tu.

Zaidi ya watoto milioni 320 ni watoto wa mzazi moja, hii inaonyesha kuwa wazazi wengi wanalea watoto wao peke yao, huenda ikawa ni sababu ya talaka ama kifo cha mzazi mmoja ama ni mwanaharamu(mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa).

Wala haimaanishi kuwa mtoto aliyekuzwa na mzazi mmoja hatapata malezi bora, La hasha, mtoto anaweza kukuzwa na malishe bora pia na maadili hata kushinda mwenye wazazi wake wawili. Jambo la kusikitisha ni kwamba, watoto wengi wa mzazi mmoja wanakuwa wakubwa bila kupata mapenzi ya baba… hii huenda pia ikafanya mtoto yule, iwapo ni wa kike awe mwenye mapenzi na wanaume wenye umri kumshinda kwa sana.

Sababu zinazopelekea mtoto kulelewa bila baba

1. Kufariki kwa baba
Hii hutokea pale ambapo mzazi wa kiume wa mtoto/watoto akafariki na mzazi aliyebaki kutofunga ndoa/ kuingia kwenye mahusiano tena au akaingia kwenye ndoa na mtu asiyekubali kubeba jukumu la kuwa baba kwa watoto hao.

2. Kutelekezwa
Hii hutokea mzazi wa kiume wa mtoto anapotelekeza familia na kuacha jukumu lote kwa mama.

3. Baba kukataa ujauzito
Mwanaume anaweza kukataa ujauzito kwa sababu mbalimbali kama kutokuwa tayari na malezi, kuwa na mahusiano mengine, kuhisi amesingiziwa ujauzito huo au kutotaka kuwa na mtoto na mwanamke husika.

4. Baba kufungwa
Uamuzi wa Mahakama unaweza kusababisha mzazi wa kike kubaki na jukumu la kulea watoto au mtoto peke yake.

5. Mama kubakwa
Vitendo vya ubakaji hususani kwa mabinti wadogo husababisha watoto kulelewa na mama pekee aidha kwa sababu ya kutomjua mhusika au kuogopa kumtaja au baada ya baba kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji

6. Maamuzi binafsi
Siku za karibuni kumekuwa na wimbi la wadada kutaka kulea watoto bila msaada wa wanaume kwa sababu ya nguvu ya kiuchumi hivyo kupelekea kufanya maamuzi ya kubeba ujauzito na kukataa kuendelea na mahusiano na mhusika au kumficha au kuamua kubeba ujauzito wa mume wa mtu akijua fika kuwa atakataa kuhusika na malezi.

Faida za mtoto kulelewa na baba na mama

Watoto huhitaji malezi ya pande zote mbili bila kujali wazazi wao wako pamoja au la. Wanaume wengi wamekuwa wakisahau hili na kuhisi mama ndie mwenye jukumu pekee la kulea watoto. Mara kadhaa hurudi usiku na kukuta watoto wamelala na hutoka asubuhi sana kabla hawajaamka pengine bila hata kujua wameamka vipi. Zifuatazo ni sababu kadhaa kwa nini watoto wanahitaji malezi ya baba:

Utashangaa lakini sehemu ya kwanza ya mtoto kujua mwanaume ni mtu gani, anaonekana vipi na tabia zake ni kupitia baba. Unavyoishi na familia yako ndio hivyo mtoto atajua wanaume wote wako hivyo!

Akina baba hucheza kwa namna tofauti kidogo na watu wengine

Mara kadhaa utasikia mama akigombana na baba pengine tu baba anatumia nguvu nyingi akiwa anacheza na mtoto akihisi atamuumiza! Akina baba hucheza kwa nguvu zaidi na hucheza na mtoto kwa muda mrefu zaidi hii humfanya mtoto ajihisi salama na mwenye furaha.

Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanaolelewa na baba huwa na tabia bora zaidi kuliko watoto wanaolelewa na mama pekee

Hakuna kitu mtoto huhitaji akiwa mdogo kama rafiki wa karibu. Watoto wadogo hasa wa kike hupenda sana kuwa karibu na baba yao, kwan huhisi salama zaidi akiwa na baba nan i mtu atakayemtetea kwa mama.

Uwepo wa baba katika maisha ya mtoto humfanya ajenge hali ya kujiamini kwani huhisi siku zote kuna mtu nyuma yake kwa ajili ya kumtetea.

Kujua namna ya kuwa baba bora/namna ya kuishi na mume

Zile tabia njema anazoziona kwa baba na mama ndio hivyo hivyo atafanya kwa mpenzi wake. Wazazi husahau kuwa Watoto hujiskia vizuri sana wanapoona hali ya mawasiliano mazuri kati ya wazazi wao hata wanapokua wametengana.


Mtoto anaelelewa na mama tu huwa na njia moja tu! Nayo ni ya mama, ni vema mtoto kupata upendo wa wazazi wote wawili ili ajue ni njia ipi sahihi kwake.

Kukaa na baba nyumbani humsaidia mtoto namna ya kuheshimu mamlaka mbalimbali za mahali husika. Mfano atajifunza kuwahi kurui nyumbani, kuvaa vizuri nk.

Wanaume wana uzoefu mwingi zaidi na maisha ya kawaida hasa kuishi na watu uvumilivu nk. Ni kawaida kumkanyaga bahati mbaya mwanaume, ukamuomba msamaha na akakuelewa, lakini kwa wanawake wengi hadithi huwa tofauti. Hapa utaona ni jinsi gani busara hii anavyoihitaji mtoto kuoka kwa baba.

Kufanya kazi kwa nguvu na bidii

Wanaume pia ni watu wanaofanya kazi kwa bidii sana hii humfundisha mtoto kutokata tamaa .


Madhara ayapatayo mtoto anayelelewa na mzazi mmoja

1. Chuki na kupunguza upendo kwa mzazi mmoja

Wazazi wanapoachana daima watoto hugawanyika, huenda wakaishi kwa baba au kwa mama, au mmoja akaishi kwa baba mwingine kwa mama, hii hupelekea chuki upande mwingine, wazazi wengi hupenda kushirikisha ugomvi wao na watoto hupenda kuzungumza kwa hasira na huenda mpaka kusema sababu ya kuachana kwao.
(mara nyingi sababu ya watu kuachana si nzuri na ni aibu kuiweka wazi hasa kwa watoto)

Baba huweza kumwambia mtoto mama yako mpuuzi sana, mama yako hana akili, mama yako malaya tabu unazopata hapa kwasababu ya umalaya wake au mama humwambia mtoto hasa anapokosea, yani unaakili kama za baba yako, usiwe chizi kama baba yako, usiwe mjinga kama baba yako.

Katika hali ya kawaida haya ni maneno machache lakini yenye ujumbe mzito na usio na busara mbele ya watoto , watoto huanza kujenga chuki kwa mzazi mmoja maana anayesema hayo ndio mzazi anayemuhudumia kwa kila kitu, mtoto lazima ataamini na kumfuata baba/mama kwa kauli zake hivi inapendeza mtoto kumuona baba/mama yake hana akili au malaya? si kauli au malezi ya kiuungwana kesho mtoto atakutusi wewe utaridhia?

2. Mawazo / Mgogoro wa nafsi

Umri wa mtoto ni tofauti na mkubwa, hakuna mtoto anayependa kuona wazazi wake wanakosana, kupigana mpaka kufikia hatua ya kuachana, hatua ambayo humuumiza zaidi mtoto kuliko wazazi, wazazi wanaamini kwamba kwakuwa wanapesa au wanauwezo wa kumuhudumi/kuhudumia mahitaji yote kwa mtoto basi anaweza kulea, (Wazazi wengi bado hawajui maana ya malezi na haki za mtoto).

Mgogoro wa nafsi unaweza ukawa wa nje au wa ndani, yani kama mzazi unaweza kumuona mwanao hana raha na akakuleza kinachomsibu au asikueleze( unaweza kumsaidia au usiweze) lakini watoto wengi huwezi kuwakuta wanakaa chini kuwaza ila yale mawazo yanawatafuna wakiwa wamelala, wanakuwa wanafikiria sana na kuumia nafsi, mtoto anaweza kula vizuri, kulala sehemu nzuri na unahakikisha unampa kila anachohitaji lakini humuoni akiwa na afya nje au kunenepa vizuri.

Hofu, mashaka na woga ndio unakuwa sehemu ya maisha yake, anaweza kuwa mjinga na asiwe mwenye kuhoji sana, hasa utakapozidi kutaka kuilazimisha furaha yake au kila atakapomuulizia baba/mama yake nawe kumpa majibu yasio faa, Akili yake inadumaa.

3. Mabadiliko ya kitabia

Tabia ya mtoto hujengwa na pande tatu, baba, mama na jamii inayowazunguka lakini tabia kuu ambayo mtoto ndio sura yake inatoka kwa baba na mama, wazazi wanapoachana na tabia za watoto pia hubadilika huenda zikawa nzuri au mbaya, lakini kwa asilimia kubwa tabia za watoto hao huegemea zaidi upande mmoja, upande ambao anapokea malezi, kwa mama au kwa baba.

Kama ni mtoto wakiume na anaishi na mama, kuna baadhi ya tabia za baba hasa za kiume anazikosa, kama vile ujasiri, uvumilivu njia za kutafuta pesa na hata baadhi ya mambo ya mahusiano na mabadiliko ya mwili, mama hawezi kuwa huru kumueleza mtoto wa kiume mambo ya kiume, na hata mtoto wa kiume akipatwa na ugonjwa wa siri hawezi kumueleza mama na hata kama atamueleza basi ni dhahiri amefikiria sana na amekosa msaada na ugonjwa tayari utakuwa umemtafuna

Vile vile kwa mtoto wa kike akiishi na baba ni hivyo hivyo, lakini pia huenda mtoto wa kiume akawa na tabia za kike kulingana na kuishi na mama yake muda mrefu, na mtoto wa kike akawa na tabia za kiume kulingana na kuishi na baba yake muda mrefu.

Kikubwa ni kushindwa na kudhitibi mihemko yao, kama mtoto wa kiume anaishi na mama yake, mara nyingi anajikuta huru kutoka na kufanya mambo mengine bila kujua anachokienda ni sahihi au si sahihi na kwa wakati husika au sio, na kwa mtoto wa kike ni rahisi kuwa huru maana baba ndio mtafutaji, muda mwingi anashinda kwenye mihangaiko au kazini muda wa kumchunga na kumlea mtoto anakosa.

Yote hayo ukijumuisha lazima tabia za watoto zibadilike na haziwezi kuwa sawa na walioishi na baba zao na mama zao pamoja mpaka wanakwenda kujitegema, huenda zikabadilika zikawa hasi au chanya tabia hizo inategemea na kujitambua kwa mzazi na mtoto husika.

4. Kukosa matunzo bora iwapo mzazi aliebeba jukumu la malezi hana uchumi imara

Hayo ni baadhi ya madhara tu ambayo mtoto humkumba baada ya wazazi kutengana ila yapo mengi zaidi kuliko hayo, ewe mzazi mambo ya kuzingatia,


Michango ya wadau

Lawama isitupwe kwa wanawake pekee

Kwani haya mambo ya kuwaponda single mothers yameanza leo?? Mbona wameanza kukanywa tangu karne iliyopita je kuna mabadiliko yoyote kwenye jamii?? Hakuna bali kila kukicha ndiyo wanazidi kuongezeka unajua kwanini?? Ni kwa sababu jamii imeyafumbia macho maovu ya wanaume na kuwatupia lawama zote wanawake kwamba wao ndiyo chanzo cha kila kitu!!

Imagine mtu anasema mwanaume kuzalisha bila ndoa ni sawa ila mwanamke kuzalishwa bila ndoa ni kosa hivyo wanaume wasijitunze wanawake ndiyo wajitunze!! Mtu kama huyu hajui tu ni jinsi gani anavyozidi kuwapa kichwa wanaume na kuwafanya wajione hawana hatia kwa mambo wanayoyafanya eti kwa sababu tu hawapati madhara mwisho wa siku hata wanawake wakisema wajitunze wanaume hawawezi kuacha kuendelea kuwatongoza kwa nia ovu kwa sababu wameshaambiwa wao kufanya hivyo siyo kosa na hawapati madhara

Kwahiyo lazima watatumia kila mbinu kuendelea kuwashawishi hao wanawake wakubali na kumbuka wanawake nao ni binadamu kama ninyi hawawezi kuchomoa kwenye vishawishi vyote kama ambavyo hata ninyi wanaume hamuwezi kufanya hivyo!! Tatizo haya mambo tukisema jaribuni kuzionya jinsia zote mbili ziache maovu hamtaki mnasema tunataka haki sawa (kana kwamba kuna jinsia iliyoruhusiwa kutenda dhambi) yaani mnaleta maswala ya haki sawa hadi kwenye maovu!!

Basi sawa mimi naomba jamii iendelee kumshikia bango mwanamke peke yake huku ikimsifia mwanaume kwa ubaharia wake na kumuambia kuwa aendelee kufanya anavyojisikia kwa sababu yeye ndiye mwenye ndoa na yeye ndiye anayemiliki dunia (utadhani kajiumba mwenyewe)!! Halafu tuone labda ipo siku hizi juhudi zitakuja kuzaa matunda mimi huo unafiki ulishanishinda kwa kweli siwezi kushikia bango jinsia moja kwenye maovu ambayo jinsia zote mbili zinahusika ila tatizo ukisema hivyo ndiyo utaambiwa unataka haki sawa (maana ndiyo utetezi uliobaki kwa wanaume)!! Okay mimi kwani nina tatizo basi ninyi endeleeni kuwaponda single mothers hivyo hivyo ipo siku wataisha wote yaani wanaume waacheni kabisa msiwaguse kwenye hayo mambo maana hawahusiki na hawapati madhara!!

--------------------

Weekend tulivu kabisa ikianza.
Pia poleni na shughuli za week nzima.

Kuna watu waajabu sana ambao ukiwatazama unabaki kushangaa. Hivi unapata wapi ujasiri wa kumtukana/kushambulia single mother?

Jaribu kufanya utafiti binafsi usio rasmi kuchunguza huyo single mother anayesemwa kwenye mada na uhalisia uliopo.


Mwanamke huyu anapambana sana fahamu vizuri kuna jamaa kakimbia majukumu hapa na huyu mwanamke kayachukua kama yalivyo na kusonga nayo mbele.

Atapambana mwanae aishi vizuri kabisa na atajitahidi kwa hali na mali mtoto hasijisikie vibaya wala kuhisi kama hana baba.
Kama mtoto ataugua mwanamke huyu atapambana mtoto apate matibabu bora kabisa kwa gharama zozote zile.

Kama ni elimu, mtoto akifikisha umri wa shule atapelekwa vyema kabisa. Swala la sare na mahitaji ya mtoto ya kila siku atampambania mwanae.

Kama ni chakula na malazi, mtoto atapata vyote hivyo bila kupepesa macho japo mama anajikakamua kweli kweli maana kuna mbwa mmoja kakimbia majukumu.

Sasa wewe unaetoa maneno makali juu ya single mother hivi haya yote huwa unayaangalia kabla ya kumtukana na kumsimanga?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Kumbuka kabla ya yote hayo kuna mtu aliona tayari kaharibu na hana alternative ndio maana kakimbia ila mwanamke huyu yeye kajifunga kilemba na kuanza kupambana na njia imeanza kuonekana wewe huku unakuja kutoa maneno machafu juu yake na kuwaanzishia nyuzi za kuwaandama.

Inaumiza sana kuwashambulia single mother kiasi hicho.


=====================

Changamoto wanazopata wanaume walio kwenye mahusiano na single mothers

Nina mwanamke ambae tuna mtoto, ila hatukuweza kuoana kutokana matatizo yaliyojitokeza wakati huo. Baadae alioolewa na sasa ni zaidi ya miaka mitano tangu aolewe, mtoto alimwaacha nyumbani kwao, nilimuomba baada ya kuolewa tukatishe mawasiliano kwa afya ya mahusiano yetu, tukawa hatusiwasiliani tena, mawasiliano pekee yakabaki kwa mamaake mzazi na mdogo wake wa kike.

Baadae nilimchukua mtoto nikampeleka Kenya kusoma, ikawa wakati wa likizo nampeleka kwa bibi yake maana ndiko alikokuzoea, sasa hivi karibuni nilimfuata mtoto nimpeleke shule, nikamkuta huyu mzazi mwenzangu yupo kwao, akaniambia kuwa alikuwa ananisubiria mimi ana mambo muhimu ya kuniambia. Akasema mazungumzo hayo yatafanyika mjini na vile vile alitaka kumfanyia mtoto wake shopping, tukaondoka mpaka mjini, lakini cha ajabu alitupeleka kwenye nyumba ambayo amejenga akasema amemjengea akanipa na documents zote, baadae akanionesha dukani ambalo amefungua na faida ataiweka kwenye akaunti ya mtoto.

Baadae tukaenda kupata chakula ili tuendelee na safari ya shule, tukiwa kwenye chakula nilimuuliza amewezaje kujenga na kufungua duka kubwa vile, akaniambia anamuibia mme wake, kwamba yeye ndie msimamizi wa biashara za mme wake na pesa zote anachukua, alinionesha akaunti yake imenona.

Mbaya zaidi kilichonifanya niandike hapa aliniomba usiku huo tuwe pamoja na kesho yake ndio tuendelee na safari, baada ya ombi hilo, nikamfikria jamaangu (simfahamu) jinsi anavyoibiwa na huyu mwanamke halafu na mimi nimuibie? Nikaona nikikataa moja kwa moja angejisikia vibaya, nikamdanganya nimeisha kanyaga miwaya, akaishia kunishukru na kunipongeza kwa kumuokoa.

Baada ya hapo nimefikria sana kuhusu hawa single mothers, hivi wanakwama wapi? Wanakumbuka nini kwa wanaume waliowazalisha?
---------------------------
Habarini watu wa Mungu

Utangulizi:
Kuna kaka yangu alioa (miaka kama mitano iliyopita) mwanamke aliyezaa na mwanaume tofauti na yeye hawajafunga ndoa na pia hawaishi pamoja kutokana na mambo ya kazi kwa pande zote mbili walishatambulishana kwa wazazi pande zote mbili na mahusiano yao ni ya uwazi na jamii inajua.

Pia mwanamke anaishi na mtoto aliyezaa na mwanaume kabla hajaanza kuishi na kaka na huyo mtoto anasoma darasa la 2 sasa(7yrs) kawaida kaka huenda kwa huyo mke kila ijumaa na kurudi jumapili jioni au jumatatu asubuhi sana na kupitiliza kazini kwake.

Tatizo lilipo
Ni kwamba mpaka leo mwanamke (shemeji) anawasiliana na mzazi wa mtoto wake (akiulizwa husema anawasiliana nae kwa sababu ya mtoto na kutuma matumizi na sio kimapenzi), na mara nyingine huja kumwona mwanae anapopata nafasi na kila anapokuja hamshirikishi kaka na akimuuliza hujibu tu alikuja bila taarifa kumwona mwanae na kwasababu anaishi mikoa ya mbali lazima alale hata siku 2 au 3 na akimuuliza analalaje hapo na ataaminije kuwa hawafanyi mapenzi? shemeji husema analala chumba cha housegirl na yeye analala na h/g.

Nimeandika hivi kwa sababu bro hii wiki hajaenda kwa mke kwa sababu kasikia yupo mzazi mwenzie na mke wake, na anakosaga sana amani, wikiendi yote kaishia kulewa tu mpaka sasa mwanaume bado yupo na kaka akitaka kuongea na mwanamke hana shida anaongea nae kwa uhuru lakini mi naona ni maigizo.

Kaniomba jana ushauri na anampenda kweli, nimeshindwa kutoa jibu ila nimemwambia amwambie mwanamke ampeleke mtoto kwa baba yake ili hiyo shida iishe kasema alishamwambia lakini shemeji anadai mtoto wake hawezi kuishi kwa mama wa kambo na kaka mpaka sasa hajazaa nae.

Naombeni pia mawazo yenu, hali ya kaka sio nzuri kwa sasa

(Hanaga mpango na mitandao ya kijamii zaidi ya whatsapp so naamini hawezi kuona huu uzi).


Changamoto wanazopata single mothers walio kwenye mahusiano na wanaume wengine / ndoa na wanaume wengine

Kuolewa au kuingia kwenye mahusiano mapya hali ya kuwa ulishawahi kuzaa mtoto au watoto kuna changamoto nyingi sana mwanamke hupitia akiwa ndani ya hayo mahusiano mapya, nitaelezea baadhi ya changamoto hizo
  • Mwanaume kukataa kubeba jukumu la ubaba kwa watoto wasio wa kwake, kama kuwaonesha upendo kama watoto wake au kuwapa huduma stahiki kama elimu bora na mahitaji muhimu, hali hii hujitokeza hasa kwa kuona anamsaidia mwenye jukumu ambaye ni baba wa mtoto hivyo kutokuwa tayari kufanya hivyo.
  • Wanawake kuwa na hofu ya watoto wao kufanyiwa vitendo vya kikatili na baba zao wa kufikia hasa kulingana na kuongezeka kwa matukio kama hayo katika jamii
  • Mama kuona kama baba wa kufikia hutoa adhabu kali kwa watoto wake hasa wanapokuwa wamekosea, na mama kutotamani mtoto kupata adhabu ya kiwango hicho na kuhisi anampa adhabu hiyo kwa kuwa si mtoto wake wa kumzaa
  • Wanaume kukataa kuishi na mtoto aliomkuta naye mwanamke, hivyo kumlazimu kuwapeleka kwa ndugu zake na kusababisha mtoto kuishi bila upendo wa wazazi

Ni nini Mama anaelea mtoto peke yake anatakiwa kufanya

Kulea mtoto bila baba sio jambo la ajabu, japo mama unatakiwa kuwa imara ili uweze kuhakikisha mwanao anapata malezi bora na elimu inayomstahili.

1. Epuka kuhamisha machungu yako kwa mtoto.
Mama unatakiwa kuwa na furaha na mwanao ili uweze kumlea vyema, basi yale machungu unayopitia juu ya kutelekezwa, hasira chuki za mzazi mwenzako usizihamishe kwa mtoto kwani hahusiki, yeye natakiwa kupewa malezi bora na upendo kutoka kwako.

2. Kumtafutia/ kuhakikisha mtoto ana baba mlezi (father figure)
Mfano wewe ni mama unaelea peke yako, unaweza kumuomba mwanaume yoyote unaemuamini anakuwa kama baba kwa mtoto wako kwa kuongea nae n.k unamuomba muda fulani anakuwa anakaa na mtoto au watoto wako ili apate mfano wa malezi ya baba na mafunzo ya kiume kutoka kwa baba huyo.

3. Usimueleze mtoto chanzo cha kutengana au yeye kupata malezi ya upande mmoja akiwa bado mdogo.
Mtoto akiwa bado mdogo akili yake haiwezi kubeba vitu vizito, hivyo usimueleze matatizo yaliyosababisha uktengana na baba yake au kma baba yake alimkataa au kama ulibakwa, kwani kufanya hivyo utamharibu kisaikolojia na kumfanya ajione hana thamani.

4. Usimpandikize chuki mtoto dhidi ya baba yake mzazi kwani ugomvi wenu haumuhusu mtoto.
Wazazi wa kike wengi walioachiwa watoto hupandikiza chuki kwa watoto kwa kuwaeleza kuwa baba zao ni watu wabaya na haafai kuwa baba. Hivyo mtoto hukua akiwa na kisasi dhidi ya baba yake na hata akikua huanza kutafuta jinsi ya kulipa kisasi na huenda akaja lipa kisasi hicho hata kwa watu wasiohusik kwani tayari ameshajeruhiwa akiwa mdogo.

5, Usimtupe wala kumdhuru mtoto iwapo utaona huwezi kumlea.
Kulea kuna changamoto nyingi na hasa kama unalea peke yako na huna chanzo cha kuaminika kukuingizia kipato. Hivyo kama huwezi kumlea usimdhuru bali mpeleke Ustawi wa jamii, serikali ya kijiji/ kata au nenda kwenye taasisi za kidini watakupa ushauri au msaada kama wataweza na pia watakuongoza ni jinsi gani mtoto anaweza kupata msaada wa watoto walio katika mazingira magumu au hata kupelekwa kwenye vituo maalamu vya watoto.

6. Iwapo utapata watoto au mtoto mwingine kwa baba mwingine wafanye wanao wawe wamoja.
Iwapo utaanzisha mahusiano mapya na kupata watoto wengine, basi wafanye watoto wako wawe kitu kimoja, wasimbague mwanao mmoja kwa kigezo cha kuwa yeye hana baba, hicho kitamfanya awe na msononeko wa moyo.

7. Ikiwa amejitambua yaani kakomaa kiakili waweza kumweleza kuhusu baba yake kwa lugha rafiki.
Unapo mweleza kuhusu yeye na baba yake epuka kutumia lugha au maneno yatakayoibua maumivu au chuki dhidi ya baba yake au wewe mwenyewe, hapa inatakiwa uwe na hekima ili kumweleza kuhusu jambo hili na kama hajui ukoo wake waweza mwambia kama unaufahamu au hata bb kama hamhui pia.
 
Why should you be a priority ?

Mama, mchumba, partner/mke.., hizi zote zina mapenzi tofauti, hata akiwa partner wako bado watoto wana nafasi ya mapenzi ya mama yao ambayo ni tofauti na mapenzi anayokupa wewe.. would you rather date a mother who care less about her kids...

Mapenzi ya mama kwa mtoto ni natural ikiwa tofauti kuna walakini.., wewe vumilia kiasi cha mapenzi unachopewa na usitake kuleta competition au kuingilia kati ya mtoto na mama yake
 
sijakuelewa vzr. Naomba nifafanulie niweze kuelewa.


Kwa kifupi - kwanza, ushauri wa mwanaume kuhusu mwanae unakuwa na mipaka kwani ukizidisha inakuwa kama unamuona shes not a good mother hata kama hoja ni za msingi na za wazi kabisa na mjadala unageuka kuwa ugomvi.

Pili, attention yake kubwa ni kwa mwanae whether yupo au hayupo (ni mkubwa, miaka kumi wa kike), na mwanaume ukiwa na attention sana kwa familia hasa mama na dada, inakuwa ni full kununa. Huyu sio mwanamke wa kwanza single mother kutoka nae, ni wa pili na wote tabia zao zinafanana katika haya.

copy sun wu
 
RaiaMbishi,

Kuhusu kuwa na attention kwa mwanae sioni tatizo sana sababu kama na wewe utazaa nae na mtaongeza watoto nina uhakika atawapa mapenzi tosha pia kama anayompa huyo mwingine.

Kuhusu malezi ya mtoto kama hataki ushauri hapo kuna walakini inabidi kama unatoa issue za maana kuhusu mtoto akusikilize na kama hafanyi hivyo ni kumweleza anayofanya sio poa, kwako wala kwa mtoto nyie kama wazazi inabidi kushauriana kwenye malezi, lakini as a mother ni vema kuwamchia awe na final say.

Kuhusu kununa kwake wewe ukiwa karibu na ndugu zako nadhani hao ulikutana nao wana matatizo na ni selfish unless kama mama yako na dada yako hawakupenda uhusiano wako na huyu single mother hivyo wamejenga uadui baina yao (ila kununa sio solution inabidi aweke wazi tatizo ni nini)
 
We ujawajulia tu Single Mums! Jifanye unampenda yule mtoto! Weeeeeeee! Atakupendaje hai ku sweep the ocean for you!

1.Rule LOVE THE KID
2.Rule Muunge mkono kuwa the baby dady ni ingrorious batsard! Ila yeye huyo mama hana makosa na si wakulaumiwa!
3.Rule muahidi Mtoto wenu atazaliwa ndani ya ndoa!

Hapo utapiga hadi basi!
 
Pole ila punguza wivu. Usiwe na wivu wa kupitiliza namna hiyo mpaka kwa mtoto/watoto.

Hata ungekutana na huyo mwanamke akiwa hana mtoto na ukazaa nae wewe bado ungejisikia hivyo hivyo mama akimjali mwanae kwahiyo stop competing with a child. You will never win.Kwanza unatakiwa kufurahi kuwa umepata mtu anaemjali mwanae hivyo unajua kama mtafika mbali atakuwa mama mzuri kwa mwanao pia.

Mimi binafsi nimewahi kuwa single mom hivyo najua hamna mwanaume anaeweza kushindana na watoto wangu. Ntampenda na kumjali ila watoto comes before anyone/anything else.

Kwahiyo wewe ridhika na hayo mapenzi anayokupa as long as anakujali vya kutosha compare to other people (isipokuwa watoto). Na ukitaka kum-WIN jumla jali sana mtoto/watoto.wako kama vile ni wakwako.

Ila kwenye kujali jitahidi kutokukosoa na kutoa sana ushauri ambao hujaombwa. Uwezekano wa yeye kudhani unakosoa aina yake ya malezi kana kwamba hayafai upo hata kama sio nia yako kwahiyo kwepa hilo.

Kila la kheri.
 
lara 1, kirachacha na sun wu, ushauri wenu mzuri sana, shukrani. Kongosho, je una maana kwamba single men and single mothers ni kama jua na nyota - ni vigumu kuendana?
 
1. usichukue nafasi ya baba wa mtoto wake,yaani usijifanye wewe ndio baba yake - baki kuwa mjomba mwema
2. kamwe usimlaumu au kumshutumu kuhusu malezi ya mtoto wake, msaidie tu pale anapohitaji msaada/maoni
3. hata mara moja usimweke katika mtanzuko wa kulazimika kukuchagua wewe au mtoto wake, msimgombanie
 
1) You cannot be her top priority simply because you are dating. You aren't her husband. Umemkuta na watoto kwahiyo huwezi ukategemea watoto washushwe rank sababu yuko kwenye relationship.

2) Huwezi kumwambia jinsi ya kulea watoto wake sababu you're just the boyfriend. Kama ukimuoa then you are the head of the house. Mkishazaa then taratibu unaweza ukawa na input kwenye mambo ya malezi, hasahasa discipline ya watoto.

3) Attention ya mama kwa watoto ni tofauti na attention ya mwanamme mzima aliyekomaa na attention kwa mama au dada zake. Hii attention ya pili unaweza ukaonekana wewe ni mama's boy, hauna msimamo. You can love you mother and care for her, lakini kama kila kitu mama yako akisema unaitika NDIO then you are a mama's boy, and no woman likes a mama's boy.

That said, hongera kwa kuwa open-minded kutaka kuwa na uhusiano na single mom.
 
Na wanawake je? Tusijifanye mama za watoto wa waume zetu???? Na kuwa mama/baba una maanisha nini? Tuwaachie kazi ya kuwakanya watoto bio-parent? Inachanganya kwa kweli.
1. usichukue nafasi ya baba wa mtoto wake,yaani usijifanye wewe ndio baba yake - baki kuwa mjomba mwema
2. kamwe usimlaumu au kumshutumu kuhusu malezi ya mtoto wake, msaidie tu pale anapohitaji msaada/maoni
3. hata mara moja usimweke katika mtanzuko wa kulazimika kukuchagua wewe au mtoto wake, msimgombanie
 
You were not supposed to show them our weak spots you know. LOL
We ujawajulia tu Single Mums! Jifanye unampenda yule mtoto! Weeeeeeee! Atakupendaje hai ku sweep the ocean for you!

1.Rule LOVE THE KID
2.Rule Muunge mkono kuwa the baby dady ni ingrorious batsard! Ila yeye huyo mama hana makosa na si wakulaumiwa!
3.Rule muahidi Mtoto wenu atazaliwa ndani ya ndoa!

Hapo utapiga hadi basi!
 
Na wanawake je? Tusijifanye mama za watoto wa waume zetu???? Na kuwa mama/baba una maanisha nini? Tuwaachie kazi ya kuwakanya watoto bio-parent? Inachanganya kwa kweli.

namaanisha usiwe kimbelembele kana kwamba wewe ndio baba/mama mzazi wa mtoto/watoto husika, kuwa mpole tu - toa ushauri unapoombwa, fanya vitu unavyotakiwa kufanya na kamwe usijifanye wewe ni zaidi ya baba/mama mzazi.
 
sasa kwa nini u-date matatizo wakati wanawake wasio na watoto ni wengi sana?

Siongle mama for single baba, angalau wana common story ya kuongelea.


That's my word....

Nakuaminia dada mkuu ingawa wakati mwingine bhangi inakupeleka speed...!!

Kwani wasio na watoto hawaoni??

Babu DC!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom