Orodha ya Wakurugenzi wa Usalama wa Taifa Tanzania "TISS" Tangu uhuru

Ile ndege "haikutekwa nyara" bali ilikuwa misled na waongoza ndege wa Nairobi alioiongoza kwenda Mwanza badala ya kwenda Entebbe. Shukurani zetu sana kwa serikali ya Kenya wakati huo ingawa Daniel alikuwa bado na msuguano wa ndani kuhusu madaraka baada ya kurithi kutoka kwa Jomo bila wakikuyu kupenda iwe hivyo, lakini bado aliamua kumsaidia Julius kwa hilo bila kujali kuwa Charles, ambaye alikuwa hasimu sana wa Julius wakati huo, angesema nini.
Siku zote mimi watu ambao huwa wanatumia akili kubwa namna hii huwa ninawaheshimu sana katika maisha yangu
 
June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".
waliomuua sidhani kama bado wapo hai, na kama wapo hai basi ni wazee sana !! wengi wao watakuwa wanatembea na vifuko vya mkojo tezi dume ikiwa inafanya yake.

Haya maisha ya duniani ukiwa mtu mkweli kabisa kabisa, huwezi kukatili maisha ya mwenzako kisa eti madaraka uliyonayo kwa muda huo.
 
Mbona hujasema kuhusu Dr. Hassy Kitine alivyofurushwa kutoka TISS.

Alivyotoka vitani uganda kumuondoa Idd Amini, alikuja na Pegout vijana wa TRA wakambana kodi mpakani akasema yeye ni Director General wa TISS hivyo hawezi kulipa kodi, habari zikamfikia Mzee Mchonga, akaomdolewa kesho yake tu!

Miaka mingi baadae Hassy Kitine mwenyewe alikiri kuwa alifanya kosa la kipuuzi sana!
 
Mmaaa!!!!
 
Back
Top Bottom