Orodha ya Wakurugenzi wa Usalama wa Taifa Tanzania "TISS" Tangu uhuru

Marehemu Balozi Dr. Augustine P. Mahiga.

Kwenye kesi ya uhaini iliyofunguliwa watu wiotaka kumpindua Nyerere urais miaka ya mwanzo ya themanini aliitwa "Mr. X" kama shahidi wa serikali.
kumbe sio Mabere Marando?
 
Hatujawahi kuwa na Usalama huru - usalama unaojali maslahi ya Taifa na si maslahi ya watawala na chama chao kilichoko madarakani.
 
Tupeni details kuhusu hiyo ndege ya makomando wa Libya kuingia 18 za mchonga wadau,
Walipojikuta wapo enemy land waligutukaje

Fungukeni sie wengine ndio kwanza tumejaliwa juzi na hayo mambo tunasikiaga juu juu tu!
😁😁😁
 
Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.

Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyepo kwa sasa

Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.

Wa pili ni Dr. Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Wa tatu ni Dr. Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr. Agustine Mahiga (PhD) - (Marehemu) ambaye alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na baadaye Waziri wa Sheria chini ya Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli - kuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TISS. Alikaimu nafasi hiyo hadi mwaka 1983, Nyerere alipomuondoa na kumteua Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.

Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha Kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.

June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".

Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.

Baada ya Kombe kuuawa alifuata Kanali Apson Mwang'onda. Huyu aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza Idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu. Cornel Mwang'onda anasifiwa kwa kuifanyia marekebisho makubwa idara ya TISS ya kimfumo na kiutendaji. Ndiye aliyewezesha muswada uliounda sheria ya TISS mwaka 1996.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alifanyiwa jaribio kubwa la kutaka kupinduliwa na baadhi askari wa JWTZ (akina Tamin, McGhee na Kepteni Maganga) . Hili lilikua jaribio la 3 kubwa la kumpindua Nyerere, lakini ni jaribio la 7 katika orodha ukijumlisha na mengine madogo. Cornel Apson Mwang'onda akiwa Mkurugenzi wa ndani wa TISS (DOI) alifanikiwa kuzima jaribio hilo. Historia hii ilimuongezea sifa ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa TISS mwaka 1995.

Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza Idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.

August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr. Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 8 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).

Mchungaji Dr. Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi September 12 mwaka 2019 alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.

#Kutoka maktaba#
Mchungaji Kipilimba akateuliwa kuwa balozi zimbabwe na kanisa lake mke ndiye mchungaji, Kipilimba ni TISS toka anasoma, akaenda BOT, CRDB na NIDA.
 
Back
Top Bottom