Hii ndio nafasi yakuonyesha ulimwengu kuwa Muungano hatuutaki Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndio nafasi yakuonyesha ulimwengu kuwa Muungano hatuutaki Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, Jun 27, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by ole // 27/06/2011 // Habari // 1 Comment

  Na, B .OLE,
  Kwa Wazanzibar walio wengi leo hii ni kuona kwamba Zanzibar kama Nchi inajitawala wenyewe huku ikiongoza tawala zake kama vile historia ya kweli unavyotufahamisha, jinsi ya utawala halali wa kIzanzibar kabla ya kuja mapinduzi ambayo yamepelekea athari kubwa miongoni mwa Jamii ya Wazanzibar hadi leo hii.
  Huu sio wakati wa malumbano kwa Wazanzibar kwani siku zote mwenye macho haambiwii tazama wala mwenye masikio yake hahitaji kuhimizwa kusikia.Hii ndio nafasi pekee kwa Wazanzibar kushikamana na kuondoa tofauti zao kwani kinyume chake ni kuipoteza Zanzibar na vizazi vyake ambavyo hadi hivi leo vinahangaika bila kujua hatma yao.
  Wakati umefika kwa Wazanzibar kuchukua hatua zinazohitajika ili kuionesha dunia kwamba na sisi Wazanzibar sio wanyama ni binaadam ambao haki zetu za msingi lazima ziheshimiwe. Mifano mingi tumeiona leo hii imetokea Duniani na mpaka sasa Wanaukombozi bado hawajarudi nyuma, wapo na wanaendelea kudai haki zao, licha ya damu inayoendelea kumwagika, lakini leo lao ni ukombozi kwa kile wanachokiamini.
  Hatuna budi kuvishukuru vyama vya upinzani Zanzibar kwa kutoa muamsho na taswiira inayoonesha kwamba Wazanzibar wameporwa kile ambacho kilikuwa chao, wametoa msaada mkubwa hili hatuwezi kulikataa.
  Wakati umefika kwa Wazanzibar kuachana na mawazo mapotofu kwa kusema kwamba tunategemea chama fulani ili kituletee maendeleo na ukombozi, au fulani ndie pekee atatuokoa, tuelewe kwamba na huyu fulani ni binaadam na yeye pia anahitaji tumsaidie kufikia lengo lake, tusilaumu tu kwani ukombozi wa Nchi si wake peke yake bali ni jukumu la kila Mzanzibar awe ndani au nje ya nchi mchango wake unahitajika na taifa.
  Huu sio wakati tena wa kufikiria hayo, kwani kila kitu kina wakati wake, la msingi hivi ni kukaa chini kama Wazanzibar bila kujali huyu ni chama gani na anatoka wapi, bali uzanzibar uwe ndio mwega wa kulalia ukombozi wa mhimili wa nchi yetu kijikomboa kwa Madhalim na maadui zetu.
  Ikiwa Wazanzibar tutakaa kimya kwa kufikiria kusubiri rasimu ya katiba au vyenginevyo, hilo nikusema kwamba Zanzibar imeshapotea na haitorudi tena kwenye mikono ya Wazanzibar abadan.
  Njama za kuihujumu Zanzibar haikuanza jana wala leo, kwa wale wenye kujua na kufuatilia historia wataungana na mimi , kwamba tokea enzi za Mababu na Mabibi zetu mbinu na hila zilitumika kuiangamiza visiwa hivi mashughuri vya Zanzibar. Kwa vile Wazanzibar waliongozwa na dini yao pamoja na ukarimu wao hayo ndio yakawa chachu kwa Wazanzibar kutawaliwa hadi leo hii. Sasa basi mwiba unapoingia ndio unapotolewa wakati umefika kwa Wazanzibar kutumia dini yao kuikomboa nchi yetu.
  Mimi nahisi kwamba kwa sisi vijana wa Kizanzibar ingelikuwa ni vyema kama tungekuwa tunapigania Nchi yetu na kuuwawa kwa hilo kuliko kufa kwa madawa ya kulevya, kwani pindipo Zanzibar ikijikomboa basi ni kusema matunda yake yatakuwa kwa umma wote wa Kizanzibar.
  Nataka niweke wazi kwamba na iwe iwavyo na tufanye kila linalowezekena, Zanzibar haiwezi kupatikana kwa njia ya kidemokrasia abadani. Sina haja ya kulizungumzia hili kwani kila Mzanzibar anajua ni kitu gani kinachoendelea Zanzibar tokea kuasisiwa kwa vyama vingi.
  Watanganyika wako tayari kupigana vita ikibidi iwe hivyo ili kuhakikisha kwamba Zanzibar siku zote inakuwa katika miliki yake na hilo ndilo lengo la Watanganyika. Mbinu nyingi zinatumika ili kuwaziba macho Wazanzibar bila wao wenyewe kujitambua kwamba hizo ni mbinu za Watanganyika kuendelea kuwatawala Wazanzibar. Watanganyika huwachukua mamluki wachache pale Zanzibar na kuwapa vyeo ili Wazanzibar waone hawa ni wenzetu, kumbe hatujui kwamba kile ni chambo tu kwani viongozi wale hawazimi wala hawawashi kule Tanganyika, wapo pale kutumiliwa kuingamiza Dola ya Kizanzibar tu.
  Watanganyika wanatumia mbinu za kitoto kabisa kuidhibiti Zanzibar, kiasi ambacho ni aibu kwa Wazanzibar kutozitambua mbinu hizi. Iweje kila maamuzi makubwa ya Wazanzibar yafanywe na Watanganyika ? Hivi sisi Wazanzibar vichwa vyetu ni maji au ? Nasema wakati umefika kwa Vijana Wakizanzibar kuacha kupiga kelele ovyo bali tukae pamoja tuandae mbinu na mikakati ya kuikomboa Zanzibar yetu, kinyume chake itakuwa tunajidanganya wenyewe Watanganyika hawawezi kuitoa Zanzibar kwa bei yeyote isipokuwa kwa vita na mikakati maalum.
  NB:Ni maoni yangu tu.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Thread ya kihaini hii.....ndo maana umeileta usiku.......jitengen kesho asbui
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  duh mwana semeni hadharani
   
 4. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hawa wamesahau zile ndinga za washa washa! We waache walete ujinga wakati wanajua fika wao wenyewe ndo wameyataka kwa kujidai wahafidhina eti CCM! Haya mzimu wa ccm huo unawatafuna!
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Unafikiri tunashangaa? Ufisadi umo ndani ya damu za watu na hizi harakati za maandamano ni kugombania ulaji tu. Kama kweli lengo la harakati hizi ni kuona kuondowa dhuluma basi mgeliungana na Wazanzibari kwa haki yao. Haki mnaitaka nyie lakini wenzenu wakiitaka mnacharuka. Unajuwa nyie uzandiki unawasumbua lakini ukweli ni ukweli na haki ni haki iko siku mtatambuwa kuwa unapodai haki basi uwe tayari kutowa haki.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  duh.......
   
 7. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Hawa wazenj waduanz kweli,wanadhan wakijtoa cc watanganyika 2tatetereka,wao ndo watakao umia as wenyewe ndo wana2tegemea sisi watanganyika 2pge mzigo tuwalishe na wao!wenyewe kutwa kazi kukaa kwenye vijiwe vya kahawa kupga umbea 2!jitoeni hata leo muone ka tanganyika itayumba kwa lolote.
   
 8. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Hivi Tanganyika iliivamia Zanzibar? Huyo Karume wenu alikuwa amelala usingizi? Mimi nakereka sana na hizi kelele za kuonewa na Watanganyika. Ebu tuambieni faida kubwa tunayoipata kutoka Zanzibar? Huku bara vimejaa vi-Pemba chungu mzima na viduka vyao. Kila kiongozi wa juu wa Zanzibar ana bangalow huku bara. Chakula chenu kwa kiasi kikubwa kinatoka bara. Bila kusahau umeme wa bure. Mtoto akililia embe mpe umkate ....................... Tanganzeni kujitenga hata leo.
   
 9. f

  fazili JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  ni mtanganyika nitafurani sana kusikia muungano unavunjika manake hauna faida yoyote na watanganyika. sisi ndio tunaopoteza in terms of bajeti yetu inakwenda zanzibar na uchumi wetu unamiminikia zanzibar. tuvune muungano kwa faida ya watanganyika kama wazanzibar nao itawafaidisha basi sawa kabisa
   
 10. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkivunja muungano bara nafuu yetu. Maana tumewabeba kwa miaka zaidi ya arobaini na hambebeki, hamna kumbukumbu wala shukrani marhuni nyie. Mkivunja muungano mtapata wapi pa kuzalia hovyo kama inzi? Vunjeni hata leo mkome. Mkienda Kenya kwa wakola ndiyo mtajua sie waungwana ati. Vunjeni muone cha moto. Mtapinduana hadi jasho liwatoke. Angalieni Comoros pale. Nani anamhitaji mwenzake kati ya bara na zenj kama si zenj kupata pa kupatia japo mlo wa dezo na vyeo lukuki bila stahiki.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwanini mnaandikia mate na wino upo. Vunjeni kisha muone nani ni nani
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..njia rahisi ya kuuvunja muungano ni Wazanzibari kususia shughuli zote za serikali ya muungano.

  ..pia Wazanzibar wawa-recall wabunge wao walioko ktk bunge la muungano.

  ..watumishi wa Kizanzibar walioajiriwa ktk serikali ya muungano nao waache kazi na kurudi Zanzibar.

  ..hayo yakitokea muungano utakuwa umefikia mwisho wake.

  ..kinachofuatia baada ya hapo ni kutafutwa msuluhishi wa kimataifa aje ku-sort out masuala ya mgawanyo wa mali za iliyokuwa serikali ya muungano.
   
 13. Sailor Boy

  Sailor Boy Senior Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haha ntafurai kuna mpemba analoga watu mtaani kw2 bora arudi zenji akakutane na walimu wake wa kulogo. Cjui atalogo wajukuu zake?
   
 14. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
Loading...