Hii ndio mito mikubwa na hatari duniani

MTO KIWIRA sijauona nkale mbasa
Mto Kiwira ni kati ya mito ya mkoa wa Mbeya(Tanzania Kusini Magharibi) ambayo majiyake yanaishia katika bahari Hindi kupitia Ziwa Nyasa na mto Zambezi.
images.jpeg
 
Hivi chanzo cha maji ya ziwa huwa ni nini? kwanini hayaishi?mfano ziwa vicktoria linatoa maji mengi lakin hayaishi.
Ziwa hili linapata maji yake mengi kutokana na mvua (80%) na kutoka vijito vingi vidogo. Mto mkubwa unaoingia Viktoria ni Mto Kageraunaotiririka kutoka magharibi.
Na maji ya ziwa Viktoria yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea bahari ya Mediteraneakwa umbali wa maili 4,000.

Ziwa Viktoria ni miongoni mwa maziwa yenye visiwa vingi vidogovidogo.
Ziwa hili lina kina cha wastani cha mita 40 na mwambao wa urefu wa kilomita 4,828, visiwa vyake vikiwa vimechangia 3.7% ya urefu huu.
Eneo la maji ya ziwa limegawanywa 6% (4,100 km2) nchini Kenya, 45% (31,000 km2) nchini Uganda, na 49% (33,700 km2) nchini Tanzania
 
thanks
 
Kama hiyo mito ilikuwepo tangu dunia kuumbwa , hayo maji hayaishi ? Ni mzunguko gani huo ? Na bahari inapokea tu bila kujaa !!
 
Kama hiyo mito ilikuwepo tangu dunia kuumbwa , hayo maji hayaishi ? Ni mzunguko gani huo ? Na bahari inapokea tu bila kujaa !!
Try to be specific mkuu, ungeuliza mto upi ili tukuambie chanzo chake cha maji
 
Ningeuliza ni mto upi ili niambiwe chanzo chake . Ni elimu tu ya msingi kujua vianzio vya hiyo mito mikubwa duniani . Swali langu la msingi ! Bahari itajaa lini ?? Mito yote hiyo inamwaga baharini .
 
Umesaha mto nail misri
Jinja, Uganda kwenye kingo ya mashariki ya Mto Nile, hapo ndipo sehemu ambapo mto unaanza kutiririka kutoka Ziwa Viktoria (chanzo cha Nile) kuelekea kwenye Bahari ya Mediterranean. Inachukuwa miezi mitatu kwa maji kumaliza safari ya maili 4,000 (kilomita 6,400).
Lakini swali la kujiuliza hapa ni..... ikiwa Ziwa Viktoria linapokea maji kutoka mito mbali mbali ya nchi za Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Mto Mara wa Tanzania, na Mto Kagera unaopita Rwanda, Burundi, na Tanzania. Maji yote haya kutoka mito kadhaa yanachangia maji yanayoingia kwenye Mto Nile. Itakuwaje chanzo kiwe Jinja tu?
Labda ingekuwa sahihi kusema kuwa kuna vyanzo vingi vya Mto Nile ambavyo vimetapakaa kwenye nchi za Afrika Mashariki.
 
Ningeuliza ni mto upi ili niambiwe chanzo chake . Ni elimu tu ya msingi kujua vianzio vya hiyo mito mikubwa duniani . Swali langu la msingi ! Bahari itajaa lini ?? Mito yote hiyo inamwaga baharini .
Mkuu, jibu ni kwamba... pamoja na mito mingi kumwaga maji yake baharini, lakini kamwe bahari haziwezi zikajaa kutokana na mabadiliko yanasabishwa na nguvu ya gravitiya mwezi na jua inayovuta dunia yetu. Sehemu ya dunia iliyo tazama mwezi ni karibu zaidi kwake na inaathiriwa zaidi na nguvu ya graviti. Maji ya bahari ni gimba moja kubwa la kiowevu na hivyo sehemu yake iliyoathiriwa zaidi inavutwa kuelekea mwezini. Ilhali mwezi unazunguka dunia katika muda wa takriban siku moja (halihalisi kidogo zaidi ya siku moja ya hesabu yetu) kuna kilele cha maji yanayovutwa kuelekea mwezini. Mzunguko wa mwezi ni masaa 24 na dakika 50 kwa hiyo saa ya maji kupaa na kupwa hubadilika hizi dakika 50 kila siku.

Kuna athira nyingine zinazovuta uso wa maji ya bahari pia; hii ni hasa kani nje kutokana na mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake na graviti ya jua. Kila mwezi wakati jua iko nyuma ya mwezi kwenye mstari nyoofu nguvu za graviti hizi mbili zinaungana na kusababisha bamvua inayomaanisha maji kujaa sana yaani uso wa maji wa bahari hupanda juu zaidi kuliko kawaida.

Kimsingi mabadiliko ya graviti ya mwezi huathiri kila kitu duniani na pia magimba madogo kama mto, bwawa na maji katika bakuli. Lakini kama gimba la maji ni dogo tofauti hazionekani ingawa zinapimika kwa mitambo.

Nadhani nimejaribu kukujibu kutokana na uelewa wangu mdogo...
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom