Hii ndio maana halisi ya "Sisi ni Tanzania mpya"

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Emmanuel J. Shilatu

1. Tanzania Leo hii ni nchi ya 7 kwa uwekezaji Afrika.

2. Tanzania ya Leo imepanda kwa nafasi 13 katika Mwaka 2016 na Mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

3. Tanzania ya Leo uchumi umekuwa hadi kufikia asilimia 7.2 toka asilimia 5.1 ya hapo awali.

4. Tanzania ya Leo Elimu kuanzia ya Msingi hadi ya Sekondari ni bure. Hapa adui ujinga anapigwa Vita kwa vitendo.

5. Tanzania ya Leo ina miliki ndege zake takribani 7 na hivyo kuifungua Tanzania kiutalii Duniani, kuongeza mapato na kuleta ufanisi na ubora wa usafiri wa anga nchini.

6. Tanzania ya Leo kuanza kutumia usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme toka ule wa kikoloni uliokuwa unatumia dizeli. Hii itasaidia Watu na mizigo kusafiri kwa haraka, kwa unafuu na hivyo itasaidia ukuaji wa uchumi kwa Kasi.

7. Tanzania ya Leo kesi Mpya zaidi ya 41 za makosa ya ufisadi na uhujumu uchumi zimefunguliwa; Kesi Mpya za rushwa zipatazo 495 zilifunguliwa na Kati ya hizo asilimia 60.14 walifungwa. Pia jumla ya Tsh. Bilioni 127.9 kuokolewa kutokana na matendo ya rushwa.

8. Tanzania ya Leo nidhamu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma imeimarika sana; Uonevu dhidi ya Mtanzania mnyonge umepungua.

9. Tanzania ya Leo Kuna upatikanaji wa dawa za kutosha mpaka ngazi za Vijiji; Vifaa tiba na upasuaji wa kibingwa unafanyika nchini. Suala la Wagonjwa kupelekwa nje ya nchi kutibiwa limepungua Sana.

10. Tanzania ya Leo inanufaika na rasilimali madini yake kwani Sasa nchi inapata gawio sawia la faida za madini (50/50) huku Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji madini.

*Shilatu E.J*
CCM%20FREE%20MINDS%20(CFM)%F0%9F%92%AA%F0%9F%8F%BE%2020190216_140928.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No.2 Tanzania ya leo inapiga vita rushwa na ufisadi??!!!
1. Sio magufuli aliyehonga wabunge na madiwani wa CHADEMA&CUF ili wahame vyama vyao na kuiingiza nchi kwenye gharama za kutisha za chaguzi za marudio??!! Hiyo kwako sio rushwa na ufisadi.
2. Sio magufuli huyu huyu aliyekwapua trilioni 2.4, rejea ripoti ya C.A.G
3. Sio ufisadi na ubinafsi kujenga uwanja wa ndege Chato n kuweka taa za kuoongozea magari wakati zinapita punda tu?
4.Huo uchumi uliokuwa uko wapi wakati watu hawana ajira, biashara zinakufa na wawekezaji wanaondoka.
5. Utawala bora ni kumtumbua Nape aliyemkemea Bashite kwa kuvamia studio na mabunduki???!!
6. Utawala bora ni kumteka MO dewji na kumkamua hela za kutosha kisha kumuachia kwa masharti mazito.
Nitaendelea....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Emmanuel J. Shilatu

1. Tanzania Leo hii ni nchi ya 7 kwa uwekezaji Afrika.

2. Tanzania ya Leo imepanda kwa nafasi 13 katika Mwaka 2016 na Mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

3. Tanzania ya Leo uchumi umekuwa hadi kufikia asilimia 7.2 toka asilimia 5.1 ya hapo awali.

4. Tanzania ya Leo Elimu kuanzia ya Msingi hadi ya Sekondari ni bure. Hapa adui ujinga anapigwa Vita kwa vitendo.

5. Tanzania ya Leo ina miliki ndege zake takribani 7 na hivyo kuifungua Tanzania kiutalii Duniani, kuongeza mapato na kuleta ufanisi na ubora wa usafiri wa anga nchini.

6. Tanzania ya Leo kuanza kutumia usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme toka ule wa kikoloni uliokuwa unatumia dizeli. Hii itasaidia Watu na mizigo kusafiri kwa haraka, kwa unafuu na hivyo itasaidia ukuaji wa uchumi kwa Kasi.

7. Tanzania ya Leo kesi Mpya zaidi ya 41 za makosa ya ufisadi na uhujumu uchumi zimefunguliwa; Kesi Mpya za rushwa zipatazo 495 zilifunguliwa na Kati ya hizo asilimia 60.14 walifungwa. Pia jumla ya Tsh. Bilioni 127.9 kuokolewa kutokana na matendo ya rushwa.

8. Tanzania ya Leo nidhamu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma imeimarika sana; Uonevu dhidi ya Mtanzania mnyonge umepungua.

9. Tanzania ya Leo Kuna upatikanaji wa dawa za kutosha mpaka ngazi za Vijiji; Vifaa tiba na upasuaji wa kibingwa unafanyika nchini. Suala la Wagonjwa kupelekwa nje ya nchi kutibiwa limepungua Sana.

10. Tanzania ya Leo inanufaika na rasilimali madini yake kwani Sasa nchi inapata gawio sawia la faida za madini (50/50) huku Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji madini.

*Shilatu E.J*View attachment 1024079

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti Emanuel shilatu

Kazi kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom