mpatto
JF-Expert Member
- Apr 28, 2017
- 766
- 1,027
Wana JF.
Basi, ikiwa zimebaki siku chache ili wanafunzi wa kidato cha sita waanze mitihani ya kumaliza elimu ya juu ya Sekondari, ni muhimu sasa kuwapa ushauri wakasome kozi ipi itakayowasaidia hapo baadaye.
Kipindi cha nyuma kidogo, watu walishauriwa kusoma masomo ya sayansi kwa sababu yalikuwa yana soko sana, yaani ajira zake zilikuwa zipo nyingi. Lakini tusidanganyane, kwa sasa hali ni tofauti, hata waliosoma Sayansi, bado wapo wengi tu mitaani hawajaajiriwa.
Kwa sasa naona kama wanaoajiriwa zaidi zaidi ni waalimu tena wa sayansi, au waalimu wale wa elimu maalum.
Sasa kutokana na kwamba si wote wanaopenda kuwa watumishi hasa katika fani ya ualimu wa elimu maalum, basi kwa hali iliyopo sasa ndugu zanguni ni hivi:
Nenda chuo, ukasome kozi ile unayoipenda, usifuate mkumbo wa kwamba kozi fulani ndio ina ajira, hilo kwa sikuhizi halipo. Bora ukasome kitu unachokipenda, ambacho unajua kabisa hata ukimaliza unaweza ukatoka na lolote la ziada linaloweza kukusaidia. Narudia tena, usichague kozi kishabiki. Mfano unachagua kishabiki, kozi ya Computer Security, lakini kumbe hata hobbie ya Linux huna, kisa tu uliambiwa ina mshahara mzuri utapopata ajira. Bora usome Bussiness Administration ambayo unajua una mpango wa kujiajiri mwenyewe hapo baadaye.
Mimi langu ni hilo tu ndugu zangu. Kama mtu una wazo tofauti basi unakaribishwa!!