Hii ndio komesha ya tatizo la ajira nchini, vinginevyo....

StudentTeacher

JF-Expert Member
Jan 30, 2019
3,679
3,718
Pamoja na yoooote lazima tuwe na Mfumo wa Elimu unaojali na kuthamini Uwezo na Vipaji asilia vya watoto mapema kabisa.Hii ni pamoja na kuwa na mfumo wa kubaini interest na uwezo asilia wa watoto na kisha kuwekeza katika ustawi wa vipaji vyao.Namaanisha elimu ifuate baada ya kubaini interest na vipaji asilia vya mtoto.Hii itasaidia;

(1)Kuepusha mkumbo na mlundikano wa watu wengi kwenye kada(fani) moja kisa tu eti hiyo kada inasemekana kwamba 'inalipa'.

Hapa kuna hatari ya fani husika kuvamiwa na watu wasio na interest wala uwezo nazo(nazungumzia uwezo wa asili ambao mtu kazaliwa nao siyo ule wa kubebeshwa).

Mfumo wa Elimu wenye kulenga kuwekeza kwenye vipaji vya watoto utafanya kila mtu akae kwenye eneo lake.Kila mtu atafanya la kwake.

Hakuna kubaka fani.Hakutakuwa na watu kulundikana eneo moja kwa mkumbo.

(2).Kuwa na wigo mpana wa kuajirika au kujiajiri popote duniani.Hii ni kutokana na ubora wa rasimaliwatu iliyonolewa vema katika fani husika kwa kuzingatia uwezo na vipaji asilia vya muhusika.

Mmesikia watu wa kale waliposena "Penzi kikohozi,halijifichi" bali Mimi TruthLover nasema "Kipaji kikohozi,hakijifichi" muhimu kitambuliwe,kichochewe, kistawishwe na kuboreshwa hapo automatically kitajiuza chenyewe.Mifano hai ipo,tena ya kutosha tu.

(3).Kuchochea Ustawi na Ubora wa huduma au bidhaa.Umewahi kujiuliza ubora wa huduma au bidhaa inayotolewa na mtu aliyesomea kitu ambacho hana interest wala uwezo nacho kwa asili?.

Jaribu tu kuvuta picha unahudumiwa huduma fulani na mtu ambaye kazi au huduma hiyo ama haipendi au hana uwezo nayo kwa asili.

(4).Kuchochea ubunifu,hivyo,kuzidi kupenya na kubamba kwenye soko la ushindani.Kipaji huzaa ubunifu.Na hapa kwenye ubunifu ndipo unapoweza kutofautisha kati ya mtu wa fani husika mwenye uwezo asilia na yule mwenye uwezo wa kupachikwa.

Ubunifu unawatofautisha.Ikumbukwe biashara yoyote bila ubunifu hasa kwa ushindani uliopo lazima ife kibudu.Kipaji kikohozi.

(5).Kila fani kupewa hadhi na heshima sawa.Tukiwa na Mfumo wa Elimu unaojali na kuthamini uwezo asilia wa watoto huji kusikia hizi bla bla za baadhi ya fani kuonekana zina hadhi ya juu kuliko nyingine kwa sababu kote kutakuwa na akina "Ronaldinho".

Anayemdharau Ronaldinho anyooshe mkono,ajifanye kama anajikuna hivi.Ukienda shuleni unakutana na akina ronaldinho-teachers,ukienda hospitali unakutana na akina ronaldinho-doctors.

Vivyo hivyo kwenye kilimo, siasa, sanaa, sayansi, habari n.k.Ni akina ronaldinho full.Haya niambie nani atamdharau nani. Mungu siyo mjinga.Kazi yake huwa anaimaliza ndani ya tumbo la kizazi.Wanaolitambua hili na kulifanyia kazi nchi zao zinameremeta.Kazi kwetu.
 
Nadhani pamajo na hayo, tunahitaji kifuata mfumo wanaofuata Marekani sasa hivi. Wanauita "The Gig Economy" unaweza google, umeongelewa sana. Kwa sisi Tanzania, tunaweza tumia www.ajiras.com kuelekea kwenye hiyo gig economy.
 
Back
Top Bottom