Hii ndio jinsi siasa za matukio zinavyozorotesha upatikanaji wa Ben Saanane

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Kama tujuavyo Beni amepotea sasa ni takribani miezi sita haifahamiki ni upi mustakabali wake na kinachosikitisha si tu vyombo vya dola kutokupata majibu kwa haraka,ama raia wenye mapenzi mema bali hata viongozi wa chama ambacho Beni alikiwa ni miongoni mwa kiongozi mwenzeo wanalifuatilia jambo hili kwa mtindo wa siasa za matukio.

Ndugu wanachadema mchezo wa kuwa busy kwenye siasa za matukio kunasababisha sakata la Beni kusahaulika kila itokeapo agenda mpya ionekanayo kama mtaji wa kisiasa.

Nafahamu mtasema kwamba CDM sio chombo cha Dola ila ifahamike sakata la Roma ni kama hili la beni lakini nadiriki kusema wasanii wameonesha mfano mzuri kuliko CDM kwani walisimama imara mpaka Roma akapatikana.

Juzi sakata hili lilionesha kufufuliwa na wanasiasa kama ZZK,Lissu na Mbowe lakini inasikitisha jambo hili kusahaulika kwa kuibuka isue ya Bashite.

Hivi ni sawa kuhangaika na kutumia nguvu kubwa kwa isue ya Bashite kuliko mustabali wa wapi alipo Beni Saanane?

Siku chache hapo nyuma kila mtu ni lazima kila aandikapo aweke#Tunamtaka Beni saanane akiwa hai,lakini kwa sasa watu wameshasahau kabisa.

Ni lazima CDM wakajifunza kupendana si tu wakati wa siasa bali hata wakati wa matatizo
 
Kwenye suala la Ben,viongozi wa chadema hawana utashi wa kisiasa ili kulisukuma.Viongozi ni kama vile wanaongea kuridhisha wananchama tu
 
Maskini miezi sita, si ajabu alishatangulia mbele ya haki!!!. Kama alitekwa apate maumivu Na vidonda kama Roma kwa siku2 hawezi kuwa hai huyu! Huyu Ben ananiumiza Roho kuliko kawaida. Alikosa nini hapa duniani hadi apotezwe bila kuona mwili wake? Yaani mtu anapotea tangu December anatafutwa April tena kwa matukio! Nguvu kubwa ilitakiwa ile December sasa hivi tujisemee tu RIP Ben saa8.
 
Na bado kuna mpango wa kuendelea kuteka watu na kuwapoteza, hata baadhi ya members wa JF wapo kwenye list Kwa Sababu ya michango yao humu
 
Kwenye suala la Ben,viongozi wa chadema hawana utashi wa kisiasa ili kulisukuma.Viongozi ni kama vile wanaongea kuridhisha wananchama tu
Baba wa beni alikuwa sahihi kumweleza Lema kwamba beni ni mtoto wake sio mbuzi wake
 
Kama tujuavyo Beni amepotea sasa ni takribani miezi sita haifahamiki ni upi mustakabali wake na kinachosikitisha si tu vyombo vya dola kutokupata majibu kwa haraka,ama raia wenye mapenzi mema bali hata viongozi wa chama ambacho Beni alikiwa ni miongoni mwa kiongozi mwenzeo wanalifuatilia jambo hili kwa mtindo wa siasa za matukio.

Ndugu wanachadema mchezo wa kuwa busy kwenye siasa za matukio kunasababisha sakata la Beni kusahaulika kila itokeapo agenda mpya ionekanayo kama mtaji wa kisiasa.

Nafahamu mtasema kwamba CDM sio chombo cha Dola ila ifahamike sakata la Roma ni kama hili la beni lakini nadiriki kusema wasanii wameonesha mfano mzuri kuliko CDM kwani walisimama imara mpaka Roma akapatikana.

Juzi sakata hili lilionesha kufufuliwa na wanasiasa kama ZZK,Lissu na Mbowe lakini inasikitisha jambo hili kusahaulika kwa kuibuka isue ya Bashite.

Hivi ni sawa kuhangaika na kutumia nguvu kubwa kwa isue ya Bashite kuliko mustabali wa wapi alipo Beni Saanane?

Siku chache hapo nyuma kila mtu ni lazima kila aandikapo aweke#Tunamtaka Beni saanane akiwa hai,lakini kwa sasa watu wameshasahau kabisa.

Ni lazima CDM wakajifunza kupendana si tu wakati wa siasa bali hata wakati wa matatizo

"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Serikali ya CCM, Yapewa Onyo la "Mwanagutu"-" Siku Yake Ipo!, Utapogeuka Upepo, Wasije Kulia!.

Nimemkumbuka Ben Saanane siku ya leo ya Uhuru wa Habari, Japo Ben sii mwandishi rasmi wa habari, lakini katika dunia hii ya kijiji kimoja, kila mpashaji habari ni mwandishi wa habari, hata Mange Kimambi ni mpashaji wa habari, taarifa yake inasomwa kuliko gazeti lolote la Tanzania, hivyo siku kama ya leo tuwakumbuke watu kama hawa!.
Paskali
 
Ni aibu kwa vyombo vya dola kufanya kazi kwa msukumo wa wana siasa!Ndicho ulichokiri,hapa ninachoona ni incompetence ya vyombo vya ulizi na usalama!
 
Kupotea kwake kumehusishwa na makala alizo andika kuhusu mkubwa Fulani serikalini. Baada ya tukio serikali ilipaswa kutumia nguvu zote kumtafuta ili kujisafisha. Kuilaumu Chadema ni wazo LA kijinga kabisa kwani haiwezi kuingilia uchunguzi wa kipolisi maana ni kosa
 
Mbowe ndio amemteka Ben

Hahahhahahahahha,pole sana sana nakuonea huruma,maana akili yako ni ndogo inatosha kisoda tu.Mtekaji wa wapinzani wa CCM ni Bashite aka fafaffafafafafaffafa na akitumika na Baba yake
 
Kupotea kwake kumehusishwa na makala alizo andika kuhusu mkubwa Fulani serikalini. Baada ya tukio serikali ilipaswa kutumia nguvu zote kumtafuta ili kujisafisha. Kuilaumu Chadema ni wazo LA kijinga kabisa kwani haiwezi kuingilia uchunguzi wa kipolisi maana ni kosa
ushahidi wote unaonyesha Mbowe ndio amemteka Ben
 
Sijui mleta hoja anamtafuta mwingine wa kumtanguliza mbele za haki au vipi? Kuna kiranja mmoja mkubwa niliwahi kumsikia kwenye mjengo fulani akitangaza kuwa "mwenzetu aliyetangulia mbele za haki" Sikumwelewa alikuwa ana maanisha nini. Mpk Leo ninatafakari sijapata jibu
 
Na bado kuna mpango wa kuendelea kuteka watu na kuwapoteza, hata baadhi ya members wa JF wapo kwenye list Kwa Sababu ya michango yao humu
Ukiitwa kutoa ushahidi juu ya hili unalolisema upo tayari? Kwn inavyoonekana tayari kumbe wewe unawajua watekaji na hata waliomteka ben saanane unawajua.na inawezekana unajua pia yuko wapi km watekaji unawajua.
 
Hii serikali ya tanzania mie naishangaa sn.km kuna watu humu jf wanaonyesha wazi kuwajua watekaji wa ben saaane.kw nn upelelezi usianzie kwao ili kuutafuta ukweli?
 
Mungu wetu ni mwenye kutenda haki.Naamini haki itatendeka kwa wote waliohusika kumteka BEN.Mungu wetu kila aliyeshiriki kwa namna yoyote kumteka BEN onyesha uwezo wako .Wapo wengi wanaomlilia BEN lakini hawana uwezo wa kumtafuta na wenye mamlaka wako kimya.Mungu wetu tenda miujiza juu ya jambo hili.
 
Back
Top Bottom