Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Wakuu,
Kabla sijatoa hoja yangu, hebu wote tutafakari yafuatayo:-
1. Hivi ni mwanachuo gani aliyekuwa anasomea ualimu wa arts ambaye mwaka 2015 angeweza kujua kuwa hadi 2017 hii atakuwa ana uhakika wa kukosa ajira angalau kwa 99'%?any way tuache hili,
2. Ni mtumishi gani wa umma ambaye mwaka jana alijua kuwa mpaka sasa atakuwa kashafukuzwa kazi kwa vyeti feki au sababu yeyote ile?
3.Ni wangapi ambao walikuwa wanajua kuwa mpaka sasa fao la kujitoa lingekuwa limefutwa?
4. Ni wangapi wanye uhakika kuwa kesho itafika wakiwa bado wako kazini? Nani ambaye ana uhakika kuwa kesho itamkuta kabla hajawa mlemavu?
Kuna mambo mengi ambayo tunapaswa kujiuliza lakini jambo la msingi la kuzingatia tu ni kwamba hakuna mwenye uhakika wa kesho yake hata uwe vizuri leo.
Kutokana na hali hiyo, hifadhi ya jamii pekee iliyobakia na ya kuaminika ni kujenga utamaduni wa kusaidiana sisi kwa sisi.Mtu anaweza kusema si viongozi wapo?ndio wapo ila na sisi kama jamii ni lazima tujenge utamaduni wa kusaidiana. Leo kwa mwenzako kesho kwako.
Hakuna namna ambayo mtu anaweza kuishi kwa furaha ikiwa waliomzunguka hawana furaha. Kutokana na mzunguko wa umasikini, kuna watu hawawezi kutoka kwenye mzunguko wa umasikini hadi wasaidiwe mitaji, lakini kama wakisaidiwa wanaweza kutoka nao kesho wakasaidia wengine.
Tuwasaidieni waliokosa ajira wajiajiri, tusaidianeni mitaji ili tuweze kufanikiwa kwa pamoja.Kwa kuanzia, humu jf mimi nshasaidia mtaji mdogo kwa watanzania wenzangu watatu. Sikusudii kujisifu bali kuhamasisha na wengine na baadae ikiwezekana tutengeneze mfumo wa kitaasisi wa kusaidiana.
Huo ndio udugu wa kitanzania tunaouzungumzia na wala si vingonevyo. Kweli nawaambia, hakuna atakayeishi kwa amani ya kweli ikiwa majirani wana njaa kali, unaweza ukawa na kiburi na dharau kwa kuwa leo umefanikiwa lakini kesho ukajikuta dhalili kuliko ulie mdharau leo. Wanadamu timeumbiwa changamoto na kwa namna zote tunategemeana. Ni lazima tutafute suluhu ya matatizo yetu wenyewe na kuyashughulikia kwa upande mmoja wakati tukiwaasa wanasiasa kutengeneza sera na mazingira rafiki kwa upande mwingine.