Hii ndio democracy tunayoihitaji tanzania-vyombo vya dola vijifunze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndio democracy tunayoihitaji tanzania-vyombo vya dola vijifunze

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Nov 8, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu kulinganisha hili tukio la CHADEMA kukesha NMC and demonstrators ambao wapo st Pauls Cathedral London kwa wiki kadhaa sasa na hakuna polisi wanaowavuruga wala kuwatimua kama walivyofanyiwa CHADEMA (Angalia picha attached au nenda Cameron lashes out at 'comatose' St Paul's protesters .


  [​IMG]  Madai ya hawa jamaa yana fanana na ambayo yanapiganiwa Tanzania na watu wengi wenye hali duni. Wao wanasema kuwa their protest is about "social justice, real democracy and challenging the unsustainable financial system that punishes the many and privileges the few" (Samahani habari yenye imeandikwa kizungu ndo maana nimenukuu kwa kizungu hicho hicho nisije nikatafsiri nikaharibu maana). Kwa muda wote huu waliokaa hawa jamaa mpaka wameweka mahema hakuna aliyewabugudhi ingawa serikali haikubaliani nao kukesha katika eneo hilo. Na mbaya zaidi jamaa wameweka hadi tents wakati mtu anaye andamana au kuprotest anatakiwa awe amesimama!

  Kwanini Tanzania isijifunze aina hii ya Democracy (Ingawa kwa wao wanaona bado hawana real democracy). Kwanini ukawatimue watu walioamua kukesha kwa ajili ya kudai haki zao hasa kama wamekesha kwa amani. Nafikiri cha msingi ilikua ni kuimarisha ulinzi hapo NMC ili watu wasiondoke kuelekea maeneo mengine kufanya fujo.

  Jamani, Tanzania ifahamu kuwa kadiri polisi wanavyo wapiga na kuwanyanyasa wananchi ndivyo hasira za wananchi zinapozidi. Serikali ijifunze kutumia busara na itumie polisi kutuliza fujo na sio kuanzisha vurugu kwa watu ambao wamekusanyika kwa amani. Nafikiri vyombo vyetu vya dola vinatakiwa vijifunze njia ya busara zaidi ya jinsi ya kuwashughulia watu wenye hasira. Sio nao kukurupuka tu.
   
Loading...