Hii ndio CHADEMA niliyoitaka inayoweza kukabiliana na Magufuli

Ok! Umeliweka vyema japo kwa swali
Kwa hiyo kipaumbele ni kupiga hela kwa mlango wa Operations, Movement miaka zaidi ya 20?
Yerico unaijua vizuri Chadema yako ilikotokea au ni kijana umeibukia ktk hujui mtokako?
Teh teh. Au ujengewe masela wengine km wa milembe mkapumzike na kufurahi? Kutokuw ana office kwa chadema ni strategy ambayo imeimaliza sana ccm.
 
Upanuzi wa mradi wa maji unaosambazwa dar es salaam ambao umeongeza upatikanaji wa maji safi
mradi wa jk huo,ila sio mbaya akiendeleza alipoishia mwenzake...kwemye maji kwa dar upatikanaji umeongezeka kweli..sijui huko vijijini.
 
nimesikia wimbo mmoja unaimba freshfresh umo ndani katajwa mkulu msishangae mkaona mkulu kashiriki kama ili kututoa mchezoni
 
Baada ya Uchaguzi mkuu 2015, Chadema ilionekana kukosa staili na midundo ya kwenda na Rais Maguli, Nasema hivyo kwakuwa mwelekeo wa siasa za kiafrika maranyingi huakisi aina na staili ya utawala ulio madarakani kwa kipindi hicho. Kwa namna fulani nilijaribu kutoa maoni humu mitandaoni na katika njia stahiki za chama changu Chadema lakini ilionekana tunakwama namna ya kutembea na chaki na Magufuli,

Naaam, sasa Chadema kama taasisi yenye watu weledi mziki umeingia damuni, ni kiguu na njia na Magufuli, akitoa unyayo, unawekwa unyayo. Hii ndio siasa za hoja zilivyo hasa katika uwanja ambao kuna siasa za jela.

Juzi nimekutana na Mh Sumaye katika mkutano wa Wilaya ya Kigamboni yeye akiwa mgeni rasmi ambapo ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, mimi ni kiwa mjumbe wa kamati tendaji Wilaya ya Kigamboni na Mjumbe wa Mkutano mkuu Chadema taifa, pembeni ya mkutano tuling'atana sikio la kikada, Kwahakika wale wanaofikiri Sumaye yule wa ccm, wanajidanganya, huyu ni sumaye aliyedhamiria kuhakikisha ccm inaondoka madarakani hata wampore kila mali aliyonayo na ikiwezekana hata uhai wake, aliongea neno zito sana alisema,

"Hivi mnadhani mimi nimekosa nini mpaka nipo hapa? Ningeweza kupumzika nyumbani tu lakini siwezi kuona taifa linaangamia, nimeungana nanyi ili tulikomboe taifa hili ili vizazi vyetu vije kuliishi salama, wameninyang'anya mashamba kisa nipo upinzani, mnadhani sikulijua kabla sijaja kuwa wataninyang'anya? Nilijua na nipo tayari, tunahitaji umoja kuliko vyeo"

Hii ilikuwa kauli nzito na yenye tafakuri pana sana toka kwa kiongozi mstaafu wa ngazi ya juu kama Waziri Mkuu.

Naaam baada ya utangulizi wa udambwidambwi huo sasa nije kwenye mada husika, Maendeleo yoyote ni matokeo ya msuguano wa kifikra chokonozi ama chochezi na kinzani ulimwenguni. Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani, faida zao za binafsi kwaamaana ya itikadi na faida za taifa na watu wake. Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao.

Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali kuu dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti, tafsiri yake ni kuwa chama kilichoshika madaraka kinachoua vyama vingine vya siasa katika nchi ya mfumo wa vyama vingi, ni chama kinachounda na kuongoza dola la kidikteta.

Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa programu au mipango.

Naaam, baada ya somo hilo fupi sasa nirejee kwenye siasa zetu za ubwa. Nipongeze chama cha Chadema na Ukawa kwakushiriki uchaguzi na kushinda kwa kura nyingi japo hakikushinda kutangazwa kushika serikali "urais". Hilo ni mchakato mrefu nitalieliza leo kwa kiasi chake,

Yote yamepita lakini siasa haijapita, bado safari ni ndefu kuelekea kushika dola kwa ridhaa ya umma bila kuruhusu damu ya Mtanzania awaye yeyote kumwagika kisa madaraka, kwa hili hongera Lowasa, Mbowe, Mbatia na Maalim Seif.

Nimezifuatilia siasa za Afrika, karibu zote zinalingana kwa kila kitu, lakini siasa za Asia hazilingani na siasa za Latini Amerika, wala siasa za Amerika hazilingani na siasa za Mashariki ya Mbali. Bali siasa za Afrika kwa namna moja zinafanana na tofauti yake ni ndogo sana ambayo inabebwa na alama tunu ya Uhuru Kenyatta anayeonyesha kwa namna moja kuiheshimu na kuiishi demokrasia walau kwa vitendo.

Ninashawikisha kuchagiza mwendo ulioanzishwa na Chadema chini ya Mwanasheria wake mkuu Tundu Lissu la kucheza na siasa za "masuala" na kuibua vuguvugu la fikra mpya za aina ya siasa nchini ambapo sasa mwelekeo wake umeruhusu AGENDA kuu ziwe mbele, itikadi ifuate kuelekea LENGO kuu la kushika dola. Tofauti na hapo nyuma vyama vinashughulika na harakati nyepesinyepesa zinazoisha muda wake mapema na kimsingi hazitupa mwangaza wakutimiza malengo yetu ya kushika dola.

Tukubaliane kuwa MALENGO makuu yetu ni kushika madaraka, hili halihitaji mjadala. Ninachojaribu kusema ni zile njia ndogo kuu za kuendea kuyashika madaraka yaani AGENDA KUU, yaani kuikosoa serikali na kuonyesha njia mbadala, hapa umma wote tumefanikiwa upo kwetu, hili hata Magufuli analijua. Kukabiliana na aina ya utawala wa Magufuli sio lelemama kama watu wengine wanavyofikiri, inatakiwa ujikane kuanzia mwili na nafsi kama walivyojikana Lissu, Mbowe, Sumaye na makada wa Chadema wengine...

Aina hii ya siasa ninayoihuisha ndio inayofanywa Amerika na Ulaya ya kati na baadhi ya Asia na Moscow. Japo hapa Afrika siasa zake ni za uchawi zaidi kuliko sayansi ya maandishi.
Ni aina nzuri ya siasa, watu wanazifia agenda badala ya vyama kwanza au matukio, watu walipende taifa kwanza na agenda kabla hawajampenda mtu au chama.

Tuuondoe mfumo ambao umewafanya watanzania kuwa na uchama badala ya agenda na utaifa.
Tujenge taasisi ambayo wanachama wake wanapotoka kwenda kuongea na wananchi wasiende na uchama ambao kimsingi uchama huo huonwa kirahisi kwa sare na bendera bali watembee na Agenda na utaifa. Unaweza kuona, kwa muda mfupi ambao amejitoa mhanga kuikabili serikali kwa hoja nzitonzito, serikali imekuwa mtumwa wakujibu, na kila inapojibu ndio inaharibu kabisaaaa na watu wanazidi kumwamini Lissu kuliko akina Zamaradi Kawawa na Abas Abdalah ambao huwezi hata kuelewa kama wanaelewa wanachokijibu au wapo gizani tu. Ukiangalia mashambulizi ya Chadema yanapangwa vizuri sana, yanaelekezwa kwenye lengo kuu ambako ni ikulu na yanafika hasaa....jambo hili linafanya kwamba mashambulizi haya yasijibiwe na ccm kama chama na kuwaacha akina Hamphrey Polepole wakishinda steshenari kughushi matamko ya serikali kumjibu Lissu hasa wakibaini wasemaji wa serikali wameshindwa kujibu vizuri.

Vikwazo vya vyama vya siasa kushika madaraka vipo vipo vinne ambavyo ni vikubwa,

1. Sheria ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo inavifanya vombo hivyo kuwa sehemu ya chama tawala ccm.

2. Tume ya uchaguzi ambayo kimsingi ni tume ya chama tawala kwasababu inachaguliwa na mwenyekiti wa ccm kuanzia mwenyekiti wake hadi karani wake na mfagia ofisi, pia katika ngazi ya majimbo tume ya uchaguzi huwa haisimamii kwa 100% kabisa uchaguzi huo na badala yake mkurugenzi wa wilaya/manispaa ndie husimamia, zingatia mkurugenzi huyo ni kada wa ccm aliyeshindwa kura za maoni za ubunge. Vivyo hivyo udiwani na uenyekiti wa mitaa husimamia na afisa mtendaji wa kata na afisa mtendaji wa mtaa ambao ni makada kindaki ndakindaki wa ccm.

3. Matokeo ya urais yathibitishwe ama yahojiwe mahakamani.

4. Katiba iweke utaratibu wa namna ya kukabidhiana madaraka.

Ninakipongeza Chadema na muungano wake wa Ukawa kuachana na matukio na agenda ndogondogo ambazo kimsingi zinaweza kusimamiwa vizuri na wanaharakati wa kawaida kama akina Mange Kimambi, Sungusia, Maria Sarungi, Kijo Bisimba nk, waachiwe ccm waendelee na viroja vya viwanda kwakuwa hawana fikra mbadala, Chadema na ukawa kwasasa iendelee kwenye maswala nyeti makubwa yanayogusa ikulu moja kwa moja kama hivi afanyavyo mwanasheria Mh Tundu Lissu, kisha ijikite katika kudai mabadiliko ya katiba mpya, Tume huru ya Uchaguzi, na kwakuwa ccm haitaleta mchakato wa katiba mpya, basi wabunge wa upinzani waanze mara moja kuandaa hoja za mabadiliko/marekebisho ya ya katiba ya 1977 katika vipengele nilivyovianisha hapo juu. Kimsingi hata kwa katiba na tume hii hii lazima tuingie katika uchaguzi, kwakuwa kuisusia ccm uchaguzi ni kuachia fisi bucha, tujifunze ya Cuf Zanzibar,

Hili ni zito ndani ya ccm na serikali yake kukubalika kwasababu linahusu itikadi ambayo ni sawa na dini kwa mtu, lakini tukilijaribu na kulihubiri kwa namna ambayo tunataka watu walielewe kuwa agenda ya Chadema ni kupambana na uovu serikalini au mapungufu yanayoanzia Ikulu, katiba mpya ya Tanzania iwe mbele, bila shaka wataelewa. Na wakibana zaidi , njooni kwa wananchi, umma haunaga majadiliano bali nguvu tu ambayo sheria na amri za kirais hazitawazuia.

Nimejaribu kupitia vitabu na machapisho mengi yanayohusu agenda na utaifa ambapo mambo kama unuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, ununuzi wa vivuko, miradi mingine ambayo inaharufu ya kutofuata taratibu za manunuzi ya nchi, hakika nimeona inaweza kuvuta kada zote zikatuelewa hata zile kada zinazozuiwa na serikali kwa minajiri ya kisiasa.

Kwakifupi tuanze kama alivyoamua Mwalimu Nyerere kuachia nyadhifa za Chama na kurudi vijijini kueneza chama kwa agenda ya uhuru bila kuvaa uchama wake. Alikwenda kama mwanautanganyika.

Lumumba imepasuka, kuna lumba ya chato na kuna lumba ya chamwino, tuachane na mambo mepesimepesi tumuunge mkono Mh Lissu na tuiunge mkono Chadema, na sasa imebaki miaka miwili na nusu tu uchaguzi mwingine! Tunataka wabunge wa upinzani waje na hoja bungeni zinazotoa mwelekeo wa kutusaidia kushinda 2020.

Upepo unazidi kuvuma huko Lumumba, uchi wa kuku unakaribia kuonekana!

Na Yericko Nyerere

Hivi kweli mtu unayefikiri vizuri unaweza kudanganywa na Lowassa na Sumaye ambao kama mnasema CCM imeleta matatizo (kama kweli) walikuwa huko kitambo. Wana jipya gani linaloweza kuleta mabadiliko chanya kama mnasema CCM ina matatizo. Sumaye alikuwepo zilipouzwa nyumba za Serikali na Lowassa pia. Mbona hamuwahoji kuhusu uamuzi huo?
 
Sisi Chadema adui yetu ni CCM ya Magufuli hivyo Magufuli ni adui yetu, tutapambana nae mchana na usiku, ardhini, angani na majini
Duh, hii vision kiboko! ......such is newest political opposition philosophy a la Chadema...na kwa tunaojua mnaelekea kumalizia kushindwa kwenu. Vinginevyo, na kwa kuwa Lissu ameachiwa kamba ajinyonge pamoja na Chadema sawia, soon or later, kwa nia ya kuokoa Chama, wenye chama (wako kimya kwa sasa) watam-ditch Lissu (political liability) na hapo ndipo Chadema kitaibuka upya kikiongozwa na Lowasa. Tusubiri.
 
Mkuu mimi naamini kuwa hata 2020 Urais unawezekana. Kwanza ujue kwa utendaji huu wa Magufuli wa one man show huku akibeza na kutukana wenzake ndani ya huu mwaka mmoja na miezi kadhaa ndio angamizo lake.
Nimemsikia waziri mmoja mwandamizi kwa masikio yangu akiongea kuwa hana hamu na kazi afanyayo na sio yeye tuu na wenzake. Lakini wanaogopa kujiuzulu kwani nikujitafutia visasi vya bure tuu. Bora kusubiri kama anatumbuliwa hiyo itakuwa furaha kwao.
Sasa msaidizi na mshauri wa ngazi hiyo anatamka hayo kweli hapo kuna timu ya mapambano 2020? Tatizo la Magu ni kuwa anatengeneza uadui sio na wapinzani tuu (ambao huo hauna shida maana ni dhahiri) bali hata ccm kaibomoa. Ukiangalia mahusiano yake na Katibu wake mkuu ni ya mashaka sana, wazee wa chama na master minders hawana uhusiano mzuri na mahusiano yao yako kwenye misingi ya kinafiki kabisa au uchumia tumbo.
Kama alivyosema Yericko, ona sasa kwa vile yeye anataka one man show basi wapinzani wameacha kutengeneza hoja za kuishambulia ccm bali mashambulizi yanaenda kwake direct na mbaya ni kuwa watetezi wake wamekuwa wale wasio na ujuzi wa propaganda hivyo wanamchafua zaidi kwa majibu yao. Hii miaka mitatu iliyobaki itafika wakati hata wanaccm watabaki kuipenda ccm yao na kumchukia yeye binafsi kwani kila shida waipatayo imani itakuwa imesababishwa na yeye binafsi.
Akimaliza 10 tunamuongezea nyie mtaendelea na uchambuzi wenu feki kuja kushtuka mshazeeka na nchi inasonga.
 
Baada ya Uchaguzi mkuu 2015, CHADEMA ilionekana kukosa staili na midundo ya kwenda na Rais Magufuli, Nasema hivyo kwakuwa mwelekeo wa siasa za kiafrika maranyingi huakisi aina na staili ya utawala ulio madarakani kwa kipindi hicho. Kwa namna fulani nilijaribu kutoa maoni humu mitandaoni na katika njia stahiki za chama changu CHADEMA lakini ilionekana tunakwama namna ya kutembea na chaki na Rais Magufuli.

Naaam, sasa CHADEMA kama taasisi yenye watu weledi mziki umeingia damuni, ni kiguu na njia na Rais Magufuli, akitoa unyayo, unawekwa unyayo. Hii ndio siasa za hoja zilivyo hasa katika uwanja ambao kuna siasa za jela.

Juzi nimekutana na Mh Sumaye katika mkutano wa Wilaya ya Kigamboni yeye akiwa mgeni rasmi ambapo ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, mimi ni kiwa mjumbe wa kamati tendaji Wilaya ya Kigamboni na Mjumbe wa Mkutano mkuu CHADEMA taifa, pembeni ya mkutano tuling'atana sikio la kikada, Kwahakika wale wanaofikiri Sumaye yule wa CCM, wanajidanganya, huyu ni Sumaye aliyedhamiria kuhakikisha CCM inaondoka madarakani hata wampore kila mali aliyonayo na ikiwezekana hata uhai wake, aliongea neno zito sana alisema,

"Hivi mnadhani mimi nimekosa nini mpaka nipo hapa? Ningeweza kupumzika nyumbani tu lakini siwezi kuona taifa linaangamia, nimeungana nanyi ili tulikomboe taifa hili ili vizazi vyetu vije kuliishi salama, wameninyang'anya mashamba kisa nipo upinzani, mnadhani sikulijua kabla sijaja kuwa wataninyang'anya? Nilijua na nipo tayari, tunahitaji umoja kuliko vyeo"

Hii ilikuwa kauli nzito na yenye tafakuri pana sana toka kwa kiongozi mstaafu wa ngazi ya juu kama Waziri Mkuu.

Naaam baada ya utangulizi wa udambwidambwi huo sasa nije kwenye mada husika, Maendeleo yoyote ni matokeo ya msuguano wa kifikra chokonozi ama chochezi na kinzani ulimwenguni. Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani, faida zao za binafsi kwaamaana ya itikadi na faida za taifa na watu wake. Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao.

Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali kuu dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti, tafsiri yake ni kuwa chama kilichoshika madaraka kinachoua vyama vingine vya siasa katika nchi ya mfumo wa vyama vingi, ni chama kinachounda na kuongoza dola la kidikteta.

Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa programu au mipango.

Naaam, baada ya somo hilo fupi sasa nirejee kwenye siasa zetu za ubwa. Nipongeze chama cha CHADEMA na UKAWA kwakushiriki uchaguzi na kushinda kwa kura nyingi japo hakikushinda kutangazwa kushika serikali "urais". Hilo ni mchakato mrefu nitalieliza leo kwa kiasi chake,

Yote yamepita lakini siasa haijapita, bado safari ni ndefu kuelekea kushika dola kwa ridhaa ya umma bila kuruhusu damu ya Mtanzania awaye yeyote kumwagika kisa madaraka, kwa hili hongera Lowassa, Mbowe, Mbatia na Maalim Seif.

Nimezifuatilia siasa za Afrika, karibu zote zinalingana kwa kila kitu, lakini siasa za Asia hazilingani na siasa za Latini Amerika, wala siasa za Amerika hazilingani na siasa za Mashariki ya Mbali. Bali siasa za Afrika kwa namna moja zinafanana na tofauti yake ni ndogo sana ambayo inabebwa na alama tunu ya Rais Uhuru Kenyatta anayeonyesha kwa namna moja kuiheshimu na kuiishi demokrasia walau kwa vitendo.

Ninashawikisha kuchagiza mwendo ulioanzishwa na CHADEMA chini ya Mwanasheria wake mkuu Tundu Lissu la kucheza na siasa za "masuala" na kuibua vuguvugu la fikra mpya za aina ya siasa nchini ambapo sasa mwelekeo wake umeruhusu AGENDA kuu ziwe mbele, itikadi ifuate kuelekea LENGO kuu la kushika dola. Tofauti na hapo nyuma vyama vinashughulika na harakati nyepesinyepesa zinazoisha muda wake mapema na kimsingi hazitupa mwangaza wakutimiza malengo yetu ya kushika dola.

Tukubaliane kuwa MALENGO makuu yetu ni kushika madaraka, hili halihitaji mjadala. Ninachojaribu kusema ni zile njia ndogo kuu za kuendea kuyashika madaraka yaani AGENDA KUU, yaani kuikosoa serikali na kuonyesha njia mbadala, hapa umma wote tumefanikiwa upo kwetu, hili hata Rais Magufuli analijua. Kukabiliana na aina ya utawala wa Magufuli sio lelemama kama watu wengine wanavyofikiri, inatakiwa ujikane kuanzia mwili na nafsi kama walivyojikana Lissu, Mbowe, Sumaye na makada wa CHADEMA wengine.

Aina hii ya siasa ninayoihuisha ndio inayofanywa Amerika na Ulaya ya kati na baadhi ya Asia na Moscow. Japo hapa Afrika siasa zake ni za uchawi zaidi kuliko sayansi ya maandishi. Ni aina nzuri ya siasa, watu wanazifia agenda badala ya vyama kwanza au matukio, watu walipende taifa kwanza na agenda kabla hawajampenda mtu au chama.

Tuuondoe mfumo ambao umewafanya watanzania kuwa na uchama badala ya agenda na utaifa. Tujenge taasisi ambayo wanachama wake wanapotoka kwenda kuongea na wananchi wasiende na uchama ambao kimsingi uchama huo huonwa kirahisi kwa sare na bendera bali watembee na Agenda na utaifa.

Unaweza kuona, kwa muda mfupi ambao amejitoa mhanga kuikabili serikali kwa hoja nzitonzito, serikali imekuwa mtumwa wakujibu, na kila inapojibu ndio inaharibu kabisaaaa na watu wanazidi kumwamini Lissu kuliko akina Zamaradi Kawawa na Abas Abdalah ambao huwezi hata kuelewa kama wanaelewa wanachokijibu au wapo gizani tu.

Ukiangalia mashambulizi ya CHADEMA yanapangwa vizuri sana, yanaelekezwa kwenye lengo kuu ambako ni ikulu na yanafika hasa jambo hili linafanya kwamba mashambulizi haya yasijibiwe na CCM kama chama na kuwaacha akina Hamphrey Polepole wakishinda steshenari kughushi matamko ya serikali kumjibu Lissu hasa wakibaini wasemaji wa serikali wameshindwa kujibu vizuri.

Vikwazo vya vyama vya siasa kushika madaraka vipo vipo vinne ambavyo ni vikubwa,

1. Sheria ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo inavifanya vombo hivyo kuwa sehemu ya chama tawala CCM.

2. Tume ya uchaguzi ambayo kimsingi ni tume ya chama tawala kwasababu inachaguliwa na mwenyekiti wa CCM kuanzia mwenyekiti wake hadi karani wake na mfagia ofisi, pia katika ngazi ya majimbo tume ya uchaguzi huwa haisimamii kwa 100% kabisa uchaguzi huo na badala yake mkurugenzi wa wilaya/manispaa ndie husimamia, zingatia mkurugenzi huyo ni kada wa CCM aliyeshindwa kura za maoni za ubunge. Vivyo hivyo udiwani na uenyekiti wa mitaa husimamia na afisa mtendaji wa kata na afisa mtendaji wa mtaa ambao ni makada kindaki ndakindaki wa CCM.

3. Matokeo ya urais yathibitishwe ama yahojiwe mahakamani.

4. Katiba iweke utaratibu wa namna ya kukabidhiana madaraka.

Ninakipongeza CHADEMA na muungano wake wa UKAWA kuachana na matukio na agenda ndogondogo ambazo kimsingi zinaweza kusimamiwa vizuri na wanaharakati wa kawaida kama akina Mange Kimambi, Sungusia, Maria Sarungi, Kijo Bisimba nk, waachiwe CCM waendelee na viroja vya viwanda kwakuwa hawana fikra mbadala, CHADEMA na ukawa kwasasa iendelee kwenye maswala nyeti makubwa yanayogusa ikulu moja kwa moja kama hivi afanyavyo mwanasheria Mh Tundu Lissu, kisha ijikite katika kudai mabadiliko ya katiba mpya, Tume huru ya Uchaguzi, na kwakuwa CCM haitaleta mchakato wa katiba mpya, basi wabunge wa upinzani waanze mara moja kuandaa hoja za mabadiliko/marekebisho ya ya katiba ya 1977 katika vipengele nilivyovianisha hapo juu. Kimsingi hata kwa katiba na tume hii hii lazima tuingie katika uchaguzi, kwakuwa kuisusia CCM uchaguzi ni kuachia fisi bucha, tujifunze ya CUF Zanzibar,

Hili ni zito ndani ya CCM na serikali yake kukubalika kwasababu linahusu itikadi ambayo ni sawa na dini kwa mtu, lakini tukilijaribu na kulihubiri kwa namna ambayo tunataka watu walielewe kuwa agenda ya CHADEMA ni kupambana na uovu serikalini au mapungufu yanayoanzia Ikulu, katiba mpya ya Tanzania iwe mbele, bila shaka wataelewa. Na wakibana zaidi, njooni kwa wananchi, umma haunaga majadiliano bali nguvu tu ambayo sheria na amri za kirais hazitawazuia.

Nimejaribu kupitia vitabu na machapisho mengi yanayohusu agenda na utaifa ambapo mambo kama unuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, ununuzi wa vivuko, miradi mingine ambayo inaharufu ya kutofuata taratibu za manunuzi ya nchi, hakika nimeona inaweza kuvuta kada zote zikatuelewa hata zile kada zinazozuiwa na serikali kwa minajiri ya kisiasa.

Kwakifupi tuanze kama alivyoamua Mwalimu Nyerere kuachia nyadhifa za Chama na kurudi vijijini kueneza chama kwa agenda ya uhuru bila kuvaa uchama wake. Alikwenda kama mwanautanganyika.

Lumumba imepasuka, kuna lumba ya chato na kuna lumba ya Chamwino, tuachane na mambo mepesimepesi tumuunge mkono Mh. Lissu na tuiunge mkono, CHADEMA na sasa imebaki miaka miwili na nusu tu uchaguzi mwingine! Tunataka wabunge wa upinzani waje na hoja bungeni zinazotoa mwelekeo wa kutusaidia kushinda 2020.

Upepo unazidi kuvuma huko Lumumba, uchi wa kuku unakaribia kuonekana!

Na Yericko Nyerere

Mkuu huu msemo unanifurahisha sana "Upepo unazidi kuvuma huko Lumumba, uchi wa kuku unakaribia kuonekana!"
 
Usichokijua ni kwamba hakuna mtu mwenye nia thabiti na maendeleo ya taifa letu,kila mtu ana maslahi yake mbele...kilichitokea 2015 kwa bwana sumaye kuhamia upinzani ni mistake tu kama ilivyo kwenye betting, kwamba unaamini Man U anashinda afu inatokea anapigwa,kwa joto la uchaguzi ule,ndugu yetu aliona upande salama kwa maslahi yake hapo baadae ni upinzani sababu aliona wanamwelekeo wa kuchukua nchi,akabeti kiasi chake chote na mambo yakawa ndivyo sivyo....hizi hadithi nyingine zote ni unafiki tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom