Hii ndio CCM kimetoka chuma kimeingia chuma siyo kama CHADEMA kaondoka Dkt. Slaa imepoteza mwelekeo

Chuma kilichotoka ndiyo hicho kimebainika kuleta hasara kubwa mno kwenye ATCL??
Huyu anatafuta njia ya kuchutama...walikua wanaamini serikali haijawahi kuibiwa wala kupoteza hata mia ndani ya miaka 5...sasa hivi wanaoa aibu..wanajifanya ooo chuma mwingine kaingia. Wkt kaanza kuonyesha madudu wa aliyepita.
 
Miradi mikubwa huanza kutengeneza faida baada ya miaka zaidi ya 10 bwashee!
Na ile bil 28 iliyotengenezwa hata mwaka haujafika ile haijahesabiwa?? Au umesahau bwana mkubwa alisema wametengeneza faida ndani ya miezi 6, sasa wewe tena unaleta story ya miaka 10? Kwahiyo ije hasara ya bil 60 kila mwaka mpk ifike miaka 10 ndo tuanze faida...hivi hii bil 60 hainunui ndege kweli
 
Huyo aliyeondoka alikuwa anafuga wezi unamwitaje chuma bwashe? Haijapita wiki kumbe DG bandari kaiba 3.6 Bilioni kwanini meko hakumgusa ?
 
Mama very soon atathibitisha serikali ya meko ilikuwa ya kifisadi kuliko zota hapa Tanzania tangu tupate uhuru.
Majizi yalikuwa yanajificha kwenye kichaka cha uzalendo...
Itafahamika tu hata tusiyoyajua.
Kikubwa watanzania wote vyama vyote vishaelekea kibla.
Twende na Rais Samia mpaka kieleweke.
 
Kuna wakati wanaccm, muwe na staha kidogo lakini pia ujiangalie marazote Kama upo sahihi na like unachotaka kusema kina maana au unajidhalilisha mwenyewe.

Ufisadi wote serikalini umetokana na serikali za wanaccm, upinzani wanaingiaje? Kama jembe alikuwepo na wakapiga je alistahili sifa alizokuwa anapewa?

Hongera Mama Samia Suluhu Hassani mwanzo mzuri.
 
Magufuli alikuwa anaongoza serikali iliyojaa majizi
Kwasasa twenda na serikali ya Rais Samia.
Ni moto wa kuotea mbali,hakika CCM ina hazina ya viongozi.
Vyama vyote vimeshalegea wanakuna vichwa,wafuasi wao wote mko na Mama Samia.
Twende na Rais Samia Tanzania tupige hatua.
 
Kimetoka Chuma kilichotuaminisha ATCL imeleta faida ya Bil 27 kimeingia chuma kinatuambia ATCL imetengeneza hasara ya Bil 60.

Kimetoka Chuma kimeweka mtu aidhibiti bandari kimeingia Chuma kinamsimamisha kwa wizi wa Bil 3.6.

Siku Tanzania tutakapoacha unafiki tutakuja kugundua kwamba CCM ndio wanaofuga wezi wote wanaotafuna hii nchi tangu uhuru
 
Viongoz wengi wa ccm wanajua watz wengi coz n MASKINI sn hufurahia wakisikia flan kafutwa kaz...na ndo ilikuwaa kiki za hayat...huyu mama ajiepushe na kikombe hicho
Hawa Nashangaa sana kuona mtu anafurahia kitendo cha kufutwa kazi
 
Kwanza niwatakie heri ya siku ya Bwana ya Matawi.

CCM ina hazina kubwa sana ya uongozi na katika hilo haina ushindani kabisa.

Kaondoka hayati Magufuli ameingia mama Samia moto ni ule ule tena unaelekea kuzidi.

Subirini huo ukaguzi wa hapo benki kuu wa fedha zilizotoka kuanzia January hadi March 2021 ndio mtajua CCM haina mambo ya kulindana kama wale watani zetu Chadema.

Nilitaka kusahau, pengo la Dr Slaa hapo Ufipa lingalipo hadi leo.

RIO Magufuli!

Sasa kama mna hazina kubwa mbona mlitaka atawale milele!! Tupe Sababu ya kwa nini mlitaka mbadilishe katiba ili atawale tu.
 
Back
Top Bottom