Hii ndio BONGO!...

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,752
7,856
Mkurugenzi wa zamani Wanyamapori asota hotelini miezi saba
Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Chuo cha Kimataifa cha Usimamizi na Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka (CAWM), Emmanuel Severe, anaishi hotelini kwa miezi saba sasa tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo kutokana na ukarabati wa nyumba aliyopangiwa kiushi kutokukamilika.

Kabla ya uteuzi huo, Severe alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kabla ya Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo, Profesa Jumanne Maghembe, kumhamishia chuoni hapo.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Severe amekuwa akiishi chumba namba 209 katika Hoteli ya Kilimanjaro Crane ya mjini Moshi.

Gharama za kuishi katika Hoteli hiyo kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu zimefikia Sh9,924,000 ambazo zinahusisha Sh60,000 kwa siku zikiwa ni gharama za chumba na gharama nyingine za chakula.

Ukarabati wa nyumba hiyo aliyokuwa akiishi mtangulizi wake, Deogratius Gamassa, umechukua muda mrefu kutokana na ukosefu wa fedha kutoka serikalini.

...Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alipoulizwa sababu za wizara yake kutoa pesa kwa mafungu hali inayosababisha ukarabati wa nyumba hiyo kuchelewa, alisema suala la utoaji wa fedha ni la kiutendaji ambalo hawezi kulizungumzia.

...hivi? ...haka kamtindo ka viongozi wanapoteuliwa kushika nyadhifa mpya (hata huko ubalozini yapo!) kupangishiwa hoteli kabla ya kuhamia kwenye nyumba mpya za serikali utakoma lini? ndio kusema kiongozi anayetemwa ('ndivyo tulivyo') anang'oa mabati, milango hadi swichi za taa kwenye hizo nyumba za 'sirikali'???

inahuzunisha inapotajwa tatizo ni ukosefu wa fedha wakati huo huo gharama za hoteli mpaka sasa lishakaribia shilingi milioni kumi, fedha za ukarabati bado hapo hesabu yake, naye akihama hadithi inaendelea hivyo hivyo...!!!

'Kula na kipofu au Wajinga ndio waliwao?'
 
Kwanza hiyo ni bahati kuwa nyumba haikuuzwa enzi za Magufuli!

Kuishi hotelini mbona ni fasheni TZ hii.

Ikipigwa hesabu kwa all new appointments taking place, the sum is shocking!!!
 
sio "kula na kipofu" kwa sababu tunaona kwa macho mawili tena mchana kweupeee, hii inaitwa "wajinga ndio waliwao"
 
Back
Top Bottom