Hii nchi ukitaka kuwa mzalendo kwa nyakati hizi basi cha kwanza lazima uwe mbumbumbu haswaa.

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
Ndio, ni lazima uwe mbumbumbu asiyeweza kupata taarifa ya mambo yanavyoenda hapa nchini hasa upande wa siasa, na hata ukizipata basi usiwe na uwezo wa kuchenjua mbivu na mbichi.

Uzalendo ni kama imani, ili uwe na imani thabiti pale mbele kwenye usukani lazima akae undisputed role model (mchukulie Yesu Kristo kwa Wakristo au Mtume Muhamad S.A.W kwa Waislamu).

Vivyo hivyo na kwenye nchi viongozi wa juu ndio wa kuwafanya wananchi wawe wazalendo kweli ama wawe na uzalendo geresha. Mfano nchi zenye raia wazalendo kwelikweli kama China, Russia n.k ni kwa sababu viongozi wao wako kwenye mstari ulionyooka kwelikweli.

Sasa tukija hapa kwetu, enzi za Baba wa Taifa uzalendo ndio ulikuwa kwenye peak ya hali ya juu kwelikweli kwa sababu kuanzia yeye mpaka wasaidizi wake walikuwa wanayaishi yale wanayoyahubiri. Tofauti na sasa ambapo mnahubiriwa elimu bure,huduma za afya kuimarika, lakini ukienda kwa ground mambo ni tofauti kabisa.

Bahati mbaya sana viongozi wa sasa ni kama wameishiwa mbinu hivi kwa sababu hata propaganda wanazopiga ni kama tuko mwaka 1960 wakati tupo 2021. Kibaya zaidi viongozi wa serikali ileile wanapingana wao kwa wao, huyu akisema hivi leo, kesho mwingine anaamka na lingine ambalo linakinzana na mwenzie.

1.jpg
 
Back
Top Bottom