Inabidi tuachane kwanza na haya mawazo ya kudhani kuwa kila masahibu yanayotukabili yanatoka nje ya nchi. Hakuna aliyetulaani wala hakuna mtu au kitu kinacholaani nchi zisiendelee. Waswahili walisema "Kikulacho Ki Nguoni Mwako" tujiangalie kwanza ndani na kujisahihisha kabla hatujaangalia nje kwa hao tunaowaita ana mabeberu au wadau wa maendeleo.