technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 11,662
- 47,525
Wakati tunaangaika na Reli wenzetu kwenye mwaka wa tatu huu SGR yao ishaanza kazi na inabeba mzigo kweli kweli kutoka Mombasa kwenda Nairobi.
Wakati tunabishana na bandari ya Bagamoyo wenzetu Kenya tayari bandari ya lamu walishazindua na itakuwa inabeba mzigo wa Somalia, Sudani, Ethiopia na nchi zingine sisi ndio kwanza tunabishana juu ya mradi ufanyike au usifanyike!
Wakati tunafunga Maduka ya kubadilishia pesa wenzetu Kenya Ukiwa Nairobi hata SAA 9 usiku unabadilisha pesa yako maduka ya kubadilisha pesa yamejaa kila konda mtaani na kwenye mahoteli.
Wakati tunajenga barabara kubwa ya kwenda Kibaha wenzetu walishajenga Thika highway miaka 10 iliyopita tena Thika highway haina kizuizi cha taa hata kimoja yaani ukitoka umetoka mpaka unafika unakoenda ila sisi angalia tunavyopanua ile barabara kwenda Kibaha kama kweli itaruhusu movement ya magari kutoka mjini bila kusimama mpaka Kibaha na hiyo stand ya Magufuli pale Mbezi.
Angalia madaraja yaliyojengwa halafu yanawekewa taa hii kitu haipo unapojenga fly over duniani kote unatakiwa kuweka njia za automatic rotation ya magari yote kutoka sehemu zote! Madaraja yote yanayojengwa kwenye makutano Dar yanahitaji marekebisho makubwa.
Juzi tulibishana kuhusu Mahindi kupelekwa Kenya wenzetu wakaja na wazo la kujenga mradi mkubwa wa umwagiliaji ambao utaweza kulisha Kenya na kuuza nje chakula na usishangae wakaanza kutuuzia tena mahindi kwa bei nafuu kuliko sisi tunavyowauzia.
Nchi yetu ina shida sana kwenye kufanya project kubwa kubwa