Hii nchi kuna watu itawashinda, Vifurushi vya Internet vimepandishwa kimya kimya

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Kuna mambo lazima tuseme ukweli, hata kama ni ukata lakini si kwa hali hii. Mitandao yote ya simu wamepandisha gharama za bando za internet bila hata kujulisha wateja wake, nini kimetokea ikiwa ni miezi 3 tu baada ya vifurushi kupandishwa wananchi wakapiga kelele sana vikashushwa chini, leo kimya kimya vimepamdishwa tena.

Kwamba sasa nchi yetu imekosa udhibiti sasa mitandao inajipandishia tuu au serikali imeamua kuwahujumu wananchi wake kimya kimya? Kwanini mbona awali walitoa taarifa kwa wateja wao lakini leo wamepandisha kimya kimya?

Wanasheria tunaweza kuungana katika hili kuondoa huu uonevu na udhalimu. Ni lazima tujue nini kimesababisha hili jambo? Mitandao ya simu tutaiburuza mahakamani.
 

Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
2,237
2,000
Ukweli ni kwamba Serikali ilishajua wananchi wengi ni lopo lopo,

Ilishaona kutangaza ni matumizi mabaya ya vyombo vya habari kwani watanzania fanya ufanyalo liwe BAYA kiasi gani watapiga kelele siku mbili baada ya hapo ni kama hakuna kitu kilichotokea.

Serikali ya kuiinulia macho na kuzidisha maombi ni kwa Mungu tu ili azidi kupukutisha viwavi/nzige waliovamia taifa Hili bila hivo twafa.
 

ALLGAMES

JF-Expert Member
Aug 28, 2021
322
500
NIKAJUA KWANGU MIMI TU ,

KUMBE HADI KWENU NINYI.

sema kimeumana!

Anyway anaupiga mwingi.

Sijui mwenda zake mnamkumbuka?

Au bado kdg ....!!!
Au hadi watuguse kunakkkko?

IPO HIVI WENYE BIG IQ HAWANA MADARAKA ...NA WENYEADARAKA vice versa iz true .....
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,510
2,000
Kuna mambo lazima tuseme ukweli, hata kama ni ukata lakini si kwa hali hii. Mitandao yote ya simu wamepandisha gharama za bando za internet bila hata kujulisha wateja wake...
Nyie wanaccm tukiwaona mnavyojigamba huwa tunadhani mna maisha bora sana kumbe hovyo tu hata kifurushi tu cha internet kukipa kinakutoa jasho.

Kama unaona kifurushi bei ghali zima simu.
 

Mzee Wa Kale Kabisa

JF-Expert Member
Mar 25, 2018
2,498
2,000
Serikali haiwezi na haitokaa ilesemee hili la sasa kwa sababu lima baraka zote toka serikalini... Walipowaambia wapunguze 10% ya tozo za miamala walijua fika hiyo 10% inayopunguzwa na makampuni itakuja kujaziwa huku kwenye vifurushi... Nchi hii ngumu sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom