Hii nchi inayotajwa hapa sio Tanzania? Na hawa watu warefu ni kina nani?

Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,804
4,444
Naomba modes msihamishe hii mada kwenye jukwaa la dini.....


Wakuu nimeona hapa kwenye kitabu cha ISAYA 18:1 kuna nchi inazungumziwa.. Naomba wataalamu mnijuze hii ni nchi gani?


1Ole, wake nchi iliyojaa mvumo wa mabawa,

nchi iliyoko ngambo ya mito ya Kushi!

2Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili,

wamepanda mashua za mafunjo.

Nendeni, enyi wajumbe wepesi,

kwa taifa kubwa na hodari,

la watu warefu na wa ngozi laini.

Watu hao wanaoogopwa kila mahali

na nchi yao imegawanywa na mito.

3Enyi wakazi wote ulimwenguni,

nanyi mkaao duniani!

Ishara itakapotolewa mlimani, tazameni!

Tarumbeta itakapopigwa, sikilizeni.

4Maana, Mwenyezi-Mungu ameniambia hivi:

“Toka makao yangu juu nitatazama yanayotukia,

nimetulia kama joto katika mwanga wa jua,

kama wingu la umande wakati wa mavuno.

5Maana, kabla ya mavuno,

wakati wa kuchanua umekwisha,

maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu,

Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea,

na kuyakwanyua matawi yanayotanda.

6Yote yataachiwa ndege milimani,

na wanyama wengine wa porini.

Ndege walao nyama watakaa humo

wakati wa majira ya kiangazi,

na wanyama wa porini watafanya makao humo

wakati wa majira ya baridi.”

7Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
 
Tanzania inatajwa kwenye Isaya 50:11
“Tazama! Ninyi nyote mnaowasha moto, mnaowasha cheche, tembeeni katika nuru ya moto wenu, na katikati ya cheche ambazo mmeziwasha moto. Hakika mtapata hili kutoka mkononi mwangu: Mtalala katika maumivu matupu.+
 
Jambo la msingi na la uhakika kabisa ni kwamba; chanzo cha maisha ya binadamu ni Tanzania na mustakabali wa maisha ya baadae ya binadamu yata-amuliwa Tanzania.

Amani ya Bwana iwe nasi sote.
 
Back
Top Bottom