Hii nchi haitakuja kuendelea kwa namna yoyote ile hadi haya yaishe

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,225
4,662
Tatizo la maendeleo ya hii nchi ni upumbavu wa Sheria na taratibu zilizowekwa na wanasiasa na wasomi wapumbavu ambao wapo tu kwa ajiri ya matumbo yao,ufuatao ni upumbavu ambao hadi uishe ndio hii nchi itaanza kupiga hatua.

1.Msururu wa viongozi wanaolipwa mishahara minono pasipo na tija yeyote ile wanayoizalisha.
(A). Kuna raisi,makamu waziri mkuu,nhivi kama angebaki tu rais na waziri mkuu nchi itasimama,kuna vitu vinakwama, haijulikani kazi ya hawa watu wanachokisimamia na ikitokea mmoja hayupo mwengine anacover vipi, ukiacha kufungua mikutano na warsha,kuongea kauli za kuhamasisha hamna cha maana wanachokifanya zaidi ya kulipwa mishahara minene na mafao makubwa kwa maisha yao yote.

(B).Mawaziri,manaibu waziri,makatibu wakuu na manaibu katibu mkuu. Hawa wote mishahara yao ni zaidi ya milioni 20 kila mmoja,kichekesho zaidi ili mtu awe waziri ni lazima awe mbunge,kwa hio mtu anavuta mshahara wa uwaziri na ubunge kwa kazi ambayo hata haijulikani ni ipi?

lazima hawa watu wapunguzwe,mwaziri wawe hata 10 tu na makatibu wakuu bila wasaidizi wake, kazi nyingi zitafanywa na maafisa wa chini, utaratibu wa usaili ufanyike apatikane mtu "competent" atakayeweza kutatuta matatizo na kithink beyond. Huu utaratibu wa hao wateule kuchaguliwa na rais wa chama chao, hamna wanachokifanya zaidi ya kumsifia raisi tu.

Ukipunguza baraza la mawaziri kwa zaidi ya asilimia mia,pesa zinazookolewa zinauwezo wa kujenga Barabara ya lami zaidi ya kilomita 500 kwa mwaka mmoja tu,amini hili suala.

(C).wabunge wa viti maalum,wanafanya nini? mbunge mmoja wa kiti maalum mapato anayolipwa kwa mwezi yanazidi hata matumizi ya hospitali ya mkoa kabisa kwa mwaka,hospitali inayohudumia halmashauri zote Tanzania Nzima.

Serikai ikivunja hio inayoitwa viti maalum ina uwezo wa kujenga "scheme" kubwa za umwagiliaji kila mkoa na chuo kimoja cha VETA ,ambapo vijana wangeweza kupata skills mbali mbali za kujiajiri, Kwa huo upuuzi hii nchi haitakuja kuendelea

(D).kupunguza idadi ya wabunge,.
Kuna wabunge hata hawajui wanachokisimamia zaidi ya kupiga kura za ndio tu hivi kila mkoa ingetoa wabunge watatu tu,unataka uniambie tungekua masikini?, watu watatu wanaofanya kazi kila siku wanashindwa kujua matatizo ya maji,umeme na bararabara etc ya mkoa husika?, pesa tunazookoa kwa kupunguza wabunge zingetumia hata kutegeneza kiwanda kila mkoa labda Morogoro cha vikombe,Mbeya ya pikipiki,Iringa cha radio etc...ni ujinga hata toothsticks za 200/= hii nchi inaagiza kutoka nje.

Huku mbunge ambaye kazi yake ni kupiga debe raisi aongezewe muda analipwa milioni 12 kwa mwezi,hatutakuja kuendelea hata iweje.

(E). Wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,RAS na DAS?,DED?.
Wote hawa wanafanya kazi gani special?,hivi kama tungekua na mkuu wa mkoa ambaye anafanya majukumu ya RAS,na mkuu wa wilaya anayefanya majukumu ya DAS na DED na hawa wote wanachaguliwa kwa usaili mkali unaozingatia elimu,uzoevu na ubunifu tungepungukiwa nini?

Hivi kuna haja gani hii nchi kila kukicha tunagawa tu mikoa na halmashauri, wakati hizo fedha zingeweza kuboresha miundombinu ya kuunganisha mkoa mmoja na mwengine ili kuchochea maendeleo mkoa mmoja unakuta una halmashauri zaidi ya 5 jamani ili iweje?

Halmashauri tatu tu zinatosha kwenye kila mkoa na mikoa isizidi 10, ukiweka watu wenye vigezo,hii nchi itasonga sana na kuendelea kwa spidi ya umeme.

Yaani unakuta matumiz ya ofisi ya mkuu wa wilaya kwa mwezi ni makubwa kuliko hata ya shule zote kwenye hio wilaya, kamati ya ulinzi na usalama inalipana posho tu hadi za milioni 5,kwa kwenda kukagua soko la milioni 50. Hivi kwa huu upumbavu hii nchi itakuja iendelee kweli?


2.Uwazi kwenye mashirika ya umma.
Ili hii nchi ipige hatua lazima mashirika ya imma yajiendeshe kwa uwazi,nafasi itangazwe mkurugenzi apatikane huu upumbavu wa rais kuteua mtu anayemtaka hakuna cha maana kitakachofanyika,tumeona kwenye utawala wa Vasco Da gama na mwendakuzimu, serikali inachukua pesa mashirika ya umma inafanya inavotaka kisha mashirika yanabaki bila kitu.

NHIF inakusanya kila mwezi mabilioni ya pesa,ila wanachokifanya ni mbingu na ardhi,hamna cha maana bima gani haitoi hata ant venom mtu akin'gatwa na nyoka,si ujuha huu yaani mfanyakazi hata afanye kazi miaka 20 siku akiacha kulipwa mshahara hata kwa mwezi mmoja bima inafungiwa si upumbavu huu ukiuliza sababu hela zote zinarudi serikalini.

Mifuko ya hifadhi ya jamii ndio kichekesho watu wanastaaafu wanakaa hadi miaka miwili hawalipwi haki yao
Mwendakuzimu baada ya kuchota pesa akaona haitoshi, akataka awape 25% hio 75% eti watapewa baadae,serious mtu amefanya kazi ana miaka zaidi ya 60 unamuambia atatumia hela zake baadae. Huu ni upumbavu,lakini sababu mashirika hayapo huru,kiongozi wa shirika amewekwa na Rais haendeshwi na sheria za shirika, analinda cheo chake.

3.Idara ya usalama wa taifa,ifumuliwe
Ni kituko kwa nchi eti kazi ya idara ya usalama wa taifa ni kulinda viongozi wa serikali na kukilinda chama tawala baada ya rasilimali.

Wakina CIA,MOSSAD,KGB hawalali kuhakikisha raia wananufaika na mali zao.

Hapa bongo mkapa anauza migodi miaka 100 kwa 97% ya muwekezaji,eti usalama wa taifa walikuepo nao wanashuhudia huo utiaji wa saini. Wachina wanauza hadi yeboyebo kariakoo eti usalama wa taifa nao wapo,si kichekesho hiki.
Rais anaingia anakopa kila kukicha,eti usalama wa taifa nao wapo.

Ili tuendele lazima tuwe na idara ya usalama wa taifa itakayolinda maslahi mapana ya raia na rasilimali zake na sio viongozi wa serikali na chama tawala

4...
 
Hili jinamizi la kijani ndio chanzo cha yote..hakuna chama pale bali ni zimwi mla watu..sio muda wa kukaa kulia na kulalamika its enough.

Watu wakija na hoja za katiba mpya wanaonekana maadui wa nchi wakati iko wazi katiba imepitwa na wakati.

Mfumo umeoza tunahitaji kuupiga chini na kuanza moja.

#MaendeleoHayanaChama
 
tuna hoja nzuri mitandaoni.....ila UZALENDO NA KIBURI cha kudai hayo ni sawa na POPO ambaye kunako giza anamtisha hata BIN-ADAMU....
 
Weee Acha tu hii nchi inasikitisha sana wakuu,Kuna mambo yanakatisha tamaa sana sana aiseee,

Chama chakavu na Nyumbu wao utaona watakavyokuja juu kutetea huu upupu wao unaolisababishia hasara Taifa na wananchi wake wakiendelea kua maskini wa kutupwa miaka nenda Rudi!
 
Tanzania ukiwa kada wa ccm wewe tayari ni usalama wa taifa Hiko ndo kigezo kikubwa hawaangalii vigezo vingine
 
Ndio maana inafikia mtu akisimama kuhutubia, mheshimiwa.....,mheshimiwa......mheshimiwa.....! Anatumia dk5 kutaja idadi ya waheshimiwa.

Ndio maana akipita kiongozi ni lazima shughuli za uzalishaji zisimame hata 1hr ili yeye kwanza apite nyie ndio mfanye shughuli zenu.

Ndio maana hata albino walipata shida sana coz watu wanatumia mbinu zote ili kupata hizo nafasi. Na ndio maana kulogana hakuishi kwa sababu hizi.
 
Ndio maana tunapiga kelele ya kuhitaji KATIBA MPYA,tuwe na mifumo huru,mfano mahakama,bunge nk.

Haiwezekani kuwe na changamoto za upandaji bei hovyo wa vitu alafu viongozi wasingizie vita.

There something wrong somewhere.
 
maneno mazuri chakufanya tutumie nguvu za umma kufikisha ujumbe huu nguvu iwe kubwa kuliko ilivyokuwa kwa mbowe
 
Wananchi masikini, viongozi na familia zao ni matajiri. Muda wa kuhangaika na maslahi ya Taifa hawana. Muda wote wameshiba na kusinzia na glass za mvinyo mkononi.
 
Back
Top Bottom