Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Hii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi....

Tumesikia wimbo huu wa kinafiki kuwa, Rais John Pombe Magufuli ni Rais na kiongozi wa wanyonge, wananchi wa hali ya chini wa nchi hii....

Si kweli, ni uongo mtupu na ni propaganda za kisiasa tu kwa ajili ya wapambe na wanafiki wachache wanaomzunguka huku uhalisia wa mambo ukiwa tofauti.....

## Mfano wa kuthibitisha hili ni huu;

Bunge limevunjwa juzi tarehe 16/6/2020. Hawa wabunge lililovunjwa juzi wameingia kazini mwaka 2015. Wamefanya kazi yao miaka mitano (5) tu toka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020....

Inasemekana mafao ya kiinua mgongo kwa miaka mitano tu kila mbunge + wabunge - mawaziri ni zaidi ya Tshs. 250,000,000....

Na inasemekana wakati Rais Magufuli (eti Rais wa wanyonge) anahutubia ndani siku hiyo "alipokuwa analivunja" bunge hilo, huko nje tayari mzigo wa fedha wa kila mbunge ulishaingia kwenye Bank Account zao na ndiyo maana ya yale makofi na vigelegele na wanawake kukata viuono mlivyokuwa mnaviona Siku hiyo....

Mtu ambaye hana uhakika na kesho yake hangekuwa na furaha isiyo na sababu kama walivyokuwa nayo hawa watu mle ndani. Sababu ni kuwa wao, Rais wao Magufuli na Spika wao walishajazana mapesa yasiyo na jasho tayari....

## Sasa hebu tazama na soma hiki cha upande wa pili wa wanyonge halisi kinachotokea....

Huko Sengerema mkoa wa Mwanza (na naamini na kwingine kote Tanzania nzima), yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi....

Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 70,000,0000 hivi.

Kinacholeta shida ni kuwa, tangu huyu mwalimu masikini amestaafu kwa mujibu wa sheria mwezi january mwaka huu. Hadi Juni hii ya mwaka huu, 2020 (miezi 6 sasa) bado anasotea mafao yake haya kidogo. Yaani hajalipwa....!

## Sasa swali la kujiuliza ni hili;

Kati ya wabunge hawa ambao bunge linavunjwa leo huku mafao yao tena makubwa kuliko kipimo cha kazi yao yakiwa yameshalipwa jana yake ama siku kadhaa nyuma kabla hata hawajavunja rasmi mkataba wao; na huku upande wa pili yupo huyu mwalimu ambaye ndiye mnyonge halisi kastaafu miezi sita (6) iliyopita na lakini mpaka leo bado hajalipwa vijisenti vyake vya mafao. Hivi hapa ni nani hasa mnyonge? Nini mantiki (logic) ya unyonge kwa mujibu wa CCM na viongozi wao?...

Na huu usawa katika nchi hii uko wapi? Iweje mbunge aliyefanya kazi miaka mitano tu alipwe mafao ya kiinua mgongo makubwa kuliko kipimo cha kazi halisi karibu mara tano ya mtumishi wa kawaida kama mwalimu ama nesi ama daktari aliyefanya kazi kulitumikia taifa hili kwa jasho na damu kwa miaka 35?

Na iweje acheleweshewe mafao yake haya kiduchu kwa miezi 6, wengine mwaka na wengine zaidi? Wanajisikiaje hawa kusikia wabunge wamestaafu juzi na mafao yao yameshalipwa tangu jana yake kabla hata ya kustaafu rasmi...?

Huyu mtetezi wa wanyonge (Bwana Magufuli) anatetea wanyonge na unyonge upi hasa?

Mimi nasema Tanzania haina kiongozi Rais mtetezi wa wanyonge.....!!

Haijapata na hakuna kizuri wala kiongozi mzuri atakayetokana na CCM ili kubadilisha hali hii na kuleta TOFAUTI, HAKI na USAWA....

Tupaze sauti zetu kwa njia mbalimbali na zozote halali juu ya jambo hili. Haiwezekani wengine tufanyishwe kazi usiku na mchana kama watumwa, jasho letu likaliwe na RAIA wachache wanaojiita "FIRST CLASS CITIZENS"....

Sasa wakati ni huu kuamua kuwa, kazi za kisiasa kama ubunge, uwaziri, Urais nk ziwe kazi za WITO na siyo za UJIRA na MAFAO makubwa. Kwa njia hii tutapata viongozi halisi walio tayari kutumika kwa ajili ya wengine, siyo hawa wa sasa....
 
Ndio maana wanatoa rushwa, kulogana, kujipendekeza ili wapate ubunge, na kazi yao kubwa bungeni nikupiga tu makofi na kusema ndio. Ningekuwa Raisi ningeshusha mshahara wa wabunge ka kada nyingine ili wapatikane wazalendo wa kweli wakutunga sera za kimaendeleo kwa nchi.
 
Hii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi.

Tumesikia wimbo huu wa kinafiki kuwa, Rais John Pombe Magufuli ni Rais na kiongozi wa wanyonge, wananchi wa hali ya chini.

Si kweli, no uongo na ni propaganda za kisiasa tu kwa ajili ya wapambe na wanafiki wachache wanaomzunguka huku uhalisia wa mambo ukiwa tofauti.

Mfano wa kuthibitisha hili ni huu;

Bunge limevunjwa juzi tarehe 16/6/2020. Hawa wabunge lililovunjwa juzi wameingia kazini mwaka 2015. Wamefanya kazi yao miaka mitano (5) tu toka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020.

Inasemekana mafao ya kiinua mgongo kwa miaka mitano tu kila mmoja ni zaidi ya Tshs. 250,000,000.

Na inasemekana wakati Rais Magufuli (eti Rais wa wanyonge) anahutubia ndani hiyo juzi kulivunja bunge hilo, tayari mzigo wa fedha wa kila mbunge ulishaingia kwenye Bank Account yake.

Hebu tazama upande wa pili wa wanyonge halisi kinachotokea.

Huko Sengerema (na naamini kwingine kote Tanzania nzima), yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi. Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 75,000,0000 hivi.

Kinacholeta shida ni kuwa, tangu huyu mwalimu masikini astaafu kwa mujibu wa sheria mwezi january hadi Juni hii mwaka huu, 2020 (miezi 6 sasa) bado anasotea mafao yake haya kidogo, hajalipwa.

Sasa swali la kujiuliza ni hili;

Kati ya wabunge hawa ambao bunge linavunjwa leo huku mafao yao yakiwa yaneshalipwa jana na huyu mwalimu ambaye kastaafu miezi sita (6) iliyopita na bado hajalipwa vijisenti vyake vya mafao, ni nani hasa mnyonge?

Na huu usawa katika nchi hii uko wapi? Iweje mbunge aliyefanya kazi miaka mitano tu alipwe mafao ya kiinua mgongo kikubwa hivyo kwa takribani mara tano ya mwalimu ama nesi ama daktari aliyefanya kazi kwa miaka 35?

Huyu mtetezi wa wanyonge (Bwana Magufuli) anatetea wanyonge na unyonge upi hasa?

Mimi nasema Tanzania haina kiongozi Rais mtetezi wa wanyonge. Haijapata na hakuna kizuri wala kiongozi mzuri atakayetokana na CCM ili kubadilisha hali hii na kuleta tofauti na usawa.
Hivi Kuna mtu analizimishwa kuwa mwalimu au police?ukilaza wenu ndo unafanya mfe masikini.
 
Ndio maana wanatoa rushwa, kulogana, kujipendekeza ili wapate ubunge, na kazi yao kubwa bungeni nikupiga tu makofi na kusema ndio. Ningekuwa Raisi ningeshusha mshahara wa wabunge ka kada nyingine ili wapatikane wazalendo wa kweli wakutunga sera za kimaendeleo kwa nchi.
Aanze kwanza kushusha mshahara wake au kutoa slip salary yake Kama alivyowadanganya wanyonge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom