Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Hakuna kada inayolipa kama siasa nchi hii. Mtu anaacha kazi yake anaingia siasani, 5yrs on ana kibunda cha 230milioni. Acheni masihara na siasa.
 
Hii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi....

Tumesikia wimbo huu wa kinafiki kuwa, Rais John Pombe Magufuli ni Rais na kiongozi wa wanyonge, wananchi wa hali ya chini wa nchi hii....

Si kweli, ni uongo mtupu na ni propaganda za kisiasa tu kwa ajili ya wapambe na wanafiki wachache wanaomzunguka huku uhalisia wa mambo ukiwa tofauti.....

## Mfano wa kuthibitisha hili ni huu;

Bunge limevunjwa juzi tarehe 16/6/2020. Hawa wabunge lililovunjwa juzi wameingia kazini mwaka 2015. Wamefanya kazi yao miaka mitano (5) tu toka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020....

Inasemekana mafao ya kiinua mgongo kwa miaka mitano tu kila mbunge + wabunge - mawaziri ni zaidi ya Tshs. 250,000,000....

Na inasemekana wakati Rais Magufuli (eti Rais wa wanyonge) anahutubia ndani siku hiyo "alipokuwa analivunja" bunge hilo, huko nje tayari mzigo wa fedha wa kila mbunge ulishaingia kwenye Bank Account zao na ndiyo maana ya yale makofi na vigelegele na wanawake kukata viuono mlivyokuwa mnaviona Siku hiyo....

Mtu ambaye hana uhakika na kesho yake hangekuwa na furaha isiyo na sababu kama walivyokuwa nayo hawa watu mle ndani. Sababu ni kuwa wao, Rais wao Magufuli na Spika wao walishajazana mapesa yasiyo na jasho tayari....

## Sasa hebu tazama na soma hiki cha upande wa pili wa wanyonge halisi kinachotokea....

Huko Sengerema mkoa wa Mwanza (na naamini na kwingine kote Tanzania nzima), yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi....

Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 70,000,0000 hivi.

Kinacholeta shida ni kuwa, tangu huyu mwalimu masikini amestaafu kwa mujibu wa sheria mwezi january mwaka huu. Hadi Juni hii ya mwaka huu, 2020 (miezi 6 sasa) bado anasotea mafao yake haya kidogo. Yaani hajalipwa....!

## Sasa swali la kujiuliza ni hili;

Kati ya wabunge hawa ambao bunge linavunjwa leo huku mafao yao tena makubwa kuliko kipimo cha kazi yao yakiwa yameshalipwa jana yake ama siku kadhaa nyuma kabla hata hawajavunja rasmi mkataba wao; na huku upande wa pili yupo huyu mwalimu ambaye ndiye mnyonge halisi kastaafu miezi sita (6) iliyopita na lakini mpaka leo bado hajalipwa vijisenti vyake vya mafao. Hivi hapa ni nani hasa mnyonge? Nini mantiki (logic) ya unyonge kwa mujibu wa CCM na viongozi wao?...

Na huu usawa katika nchi hii uko wapi? Iweje mbunge aliyefanya kazi miaka mitano tu alipwe mafao ya kiinua mgongo makubwa kuliko kipimo cha kazi halisi karibu mara tano ya mtumishi wa kawaida kama mwalimu ama nesi ama daktari aliyefanya kazi kulitumikia taifa hili kwa jasho na damu kwa miaka 35?

Na iweje acheleweshewe mafao yake haya kiduchu kwa miezi 6, wengine mwaka na wengine zaidi? Wanajisikiaje hawa kusikia wabunge wamestaafu juzi na mafao yao yameshalipwa tangu jana yake kabla hata ya kustaafu rasmi...?

Huyu mtetezi wa wanyonge (Bwana Magufuli) anatetea wanyonge na unyonge upi hasa?

Mimi nasema Tanzania haina kiongozi Rais mtetezi wa wanyonge.....!!

Haijapata na hakuna kizuri wala kiongozi mzuri atakayetokana na CCM ili kubadilisha hali hii na kuleta TOFAUTI, HAKI na USAWA....

Tupaze sauti zetu kwa njia mbalimbali na zozote halali juu ya jambo hili. Haiwezekani wengine tufanyishwe kazi usiku na mchana kama watumwa, jasho letu likaliwe na RAIA wachache wanaojiita "FIRST CLASS CITIZENS"....

Sasa wakati ni huu kuamua kuwa, kazi za kisiasa kama ubunge, uwaziri, Urais nk ziwe kazi za WITO na siyo za UJIRA na MAFAO makubwa. Kwa njia hii tutapata viongozi halisi walio tayari kutumika kwa ajili ya wengine, siyo hawa wa sasa....
Miazi sita Wazee wanadao huu mwaka wa 2
 
Wabunge walifanywa vichaa baada ya Spika kuliharibu kimaslahi. Safari hii ndio litakuwa baya zaidi likiongozwa na ngongoti.
 
Unahitaji kwanza kufanya mambo haya matatu, halafu endelea na mengine:
1. Usiwaamini wanasiasa;
2. Usiwaamini wanasiasa; na
3. Usiwaamini wanasiasa.
 
Mleta mada yeye kaona katika hili wa kulaumiwa ni Magufuli na ccm tu,ila mie naona hawa wanasiasa wa upinzani ndio wanatakiwa kulaumiwa kwa unafki wa kutopigia kelele masuala yenye kugusa masilahi yao.
Wapo radhi kuandaa kiki zao za kipumbavu ndo ujue jinsi gani walivyoukuwa wabinafsi na Rejea kisa cha mbwa wa nasari alivyouwawa kwa risasi uongozi wa chama CDM walikusanyika kwenda kumzika mbwa full makamera na hata hao wanasiasa wa chama tawala halikadhalika...hii inchi ina mfumo mbovu sana juu ya kutetea mtu wa tabaka la chini...ukitaka kuona rangi yao halisi wakate posho za vikao vya bunge ndo utawaona front wakitafuta huruma ya wananchi. Yaani wapinzania walinisikitisha sana haswa Chadema walishindwa hata kwenda front baada ya tukio la lissu badala yake wapo tweeter wanatweet ugoro tu.

Watu tunateseka huku tuna vimilioni vyetu kwenye akaunti za mifuko ya hifadhi ya jamiii hizo kalenda sasa kama unafukuzia demu wa kihindi....Wanasiasa angalieni na watu watabaka la chini sio wanaumia huku...nyie mkija majimbo mbwembwe nyingi maneno mengine anayatumia kuwaomba wawasaidie kupita,mkishapita mnawa dump this is not fear
 
Usawa hautakuwepo kamwe
Hata kama huo usawa usipokuwepo lakini haki itendeke kwa kila mtu apate chake kwa wakati sio mtu ana amana yake lakini haipati kwa wakati tena kwa kuisujudia ....Je ingetokea hao wabunge waliohudumu hizo nafasi na kuja kulipwa mafao yao baada ya 70 tena kwa kuwasujudia watu ungewaona humo bungeni?..Kikubwa serikali itengeneze utaratibu wa kuwasaidi hawa wastaafu kupata chao mapema bila ya kughuza hii itasaidia watu kutokufa kwa kihoro maana kazini anawajibika kwa kutoa jasho ikifika wakati wa mafao nao atoe jasho.
 
Inasikitisha sana, yeye mwenyewe MTUKUFU MFALME anajilipa 1.2 Bilioni kila mwezi (NJE YA MSHAHARA NA MARUPURUPU YAKE), kwaajili ya kufanyia STAREHE NA ANASA TU.
Nchi hii inaliwa na wenye meno, wajinga ndio waliwao. Ndio sababu haya ma CCM yapo tayari KUCHAPA RISASI MPINZANI YEYOTE MCHANA KWEUPE..
Ila mbunge mpinzani mwenzio anakula mema ya nchi.
 
Hii ilipaswa iwe SAUTI KUU YA WATANZANIA
Wabunge wanafaidi wao wakirudi majimboni story nyingiiiii hawana lolote

WABUNGE KWA NINI MAISHA YENU YAWE YA UHAKIKA ZAIDI KULIKO MTANZANIA
BUNGENI HUWA HAMUONGELEI POSHO MISHAHARA MIKOPO YENU??!
TUANZIE HAPA
HAMSTAHILI MEMA YA NCHI KULIKO MTANZANIA WA KAWAIDA
KWENYE MIKUTANO YENU TUNAOMBA MTUJIBU HILI
WABUNGE WA KUTEULIWA NI KICHAKA CHA UHUNI HAWANA WANALOFANYA BUNGENI

ALL THIS CRAP HAS TO STOP !
Hao jamaa wajanja wametugawa tusiwe wamoja hatuwezi kuwa na sauti moja,leo humu ukisema uhoji yale waliyoyafanya wabunge wetu majimboni utaona watu wanaanza kuwatetea wabunge wao.
 
Kama wabunge wa ccm awamu hii ni hasara kabisa wamekula bure Kodi zetu, wametumia mda kumsifia mungu wao kuliko kuzuia matumizi mabaya ya Kodi zetu.
Bunge limekuwa kibogoyo Kama Umoja wa Africa kushindwa kumlinda Gaddafi asiuwawe na mabeberu.
 
Wapo radhi kuandaa kiki zao za kipumbavu ndo ujue jinsi gani walivyoukuwa wabinafsi na Rejea kisa cha mbwa wa nasari alivyouwawa kwa risasi uongozi wa chama CDM walikusanyika kwenda kumzika mbwa full makamera na hata hao wanasiasa wa chama tawala halikadhalika...hii inchi ina mfumo mbovu sana juu ya kutetea mtu wa tabaka la chini...ukitaka kuona rangi yao halisi wakate posho za vikao vya bunge ndo utawaona front wakitafuta huruma ya wananchi. Yaani wapinzania walinisikitisha sana haswa Chadema walishindwa hata kwenda front baada ya tukio la lissu badala yake wapo tweeter wanatweet ugoro tu.

Watu tunateseka huku tuna vimilioni vyetu kwenye akaunti za mifuko ya hifadhi ya jamiii hizo kalenda sasa kama unafukuzia demu wa kihindi....Wanasiasa angalieni na watu watabaka la chini sio wanaumia huku...nyie mkija majimbo mbwembwe nyingi maneno mengine anayatumia kuwaomba wawasaidie kupita,mkishapita mnawa dump this is not fear
Hawa jamaa hawana utofauti wowote ndio walewale tu wamefanikiwa kutugawa kuna watu hawagundua unafki wa hawa wapinzani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom