Hii nayo ni taaluma rasmi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii nayo ni taaluma rasmi?

Discussion in 'Entertainment' started by The Boss, Mar 16, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Siku hizi ukisikiliza radio za fm,utagundua jambo moja..
  kwamba radio karibu zote zimeaajiri mashangingi kwa
  ajili ya kuendesha vipindi hasa mchana......
  mwanzo ilikuwa radio moja tu.sasa ni zote
  mpaka TBC Taifa nao,
  yaaani mashangingi na ushangingi kwenye airwave
  zote mchana,na muziki unaotawala ni taarabu tu,
  as if wasikilizaji wao wote tunaishi Mwananyamala na Magomeni....
  na wote labda ni wamama wa nyumbani........
  najiuliza hivi hizi radio za fm zikiajiri decent women kuendesha
  vipindi vyao vitakosa wasikilizaji????
  so ushangingi sasa ni taaluma rasmi na ndio popular culture
  hapa TZ hasa Dar???
  halafu main topic ya vipindi hivyo ni taarabu,kurushana roho,mbinu
  za kukamata mabwana na kadhalika...yaani ushangingi full...
  wako wapi decent women ambao wanaweza ku insipire
  wanawake kuwa more independent na kupendana badala ya
  ku promoti vijembe na rusha roho culture kila siku?????
  hivi wasichana waliosoma seminary mfano wanaweza kweli kuajiriwa
  kwenye radio hizi??au ndio kuwa decent na kujiheshimu ndo imekuwa
  ushamba these days????
  mara sjui mcharuko,yaliyomo yamo,mitikisiko ya pwani na kadhalika
  ili mradi ushangingi umekuwa mainstreem culture naona........
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhh.......
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kumbe. Nikija mjini sintasikiliza kabisa RADIO MARIYA.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhh..karibu mjini....
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Aramba aramba ammh! ammh! aramba tena! Wanayoyazungumza wadada hawa ndio life halisi ya majority. Let be fair they are entertaining while teaching sikiza Leo tena, Kitchen Party, Nyumbani Leo, rafiki yangu Salma Dakota sijamsikiliza siku mingi kidogo n.k. WANAFUNDISHA bana
   
 6. P

  Penguine JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2010
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180

  Jamani sasa hapo walamba lamba nini tena ati?
   
 7. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  The Boss tutake radhi tunaokaa Mwananyamala kwa Msisiri.Wengine tuna ustaarabu wetu na sio wote mashangingi.Ni maisha tu yametufanya tuishi huko.
   
 8. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pole sana bibie haya ni mambo ya.... samaki mmoja....The Boss alisahau kuweka neno .....majority...
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  The Boss sauti tu zinakufanya utambue hayo ni mashangingi?:D
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha N-Handsome kumbe weye ni mzee wa vidole juu mmh!
   
 11. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dah! Asante Kimey! Yani wote tunaonekana hatufai.Tukikaa wote Oysterbay nani atakaa Mwananyamala?
   
 12. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Unasahau yafuatayo.......

  kuwa mwenye FM stesheni ndo anayataka hayo.................... vinginevyo wangeshafukuzwa kazi.

  Yale ndo maisha yetu halisi huku mitaani................................

  Wanaoishi huko "MASAKI" ndo wasikilizaji wakubwa wa redio hizo......... na ndiyo maana shigongo anauza saaanaaa magazeti yake kuliko hizo "dele nyuzi" zenu. na wa huko huko ndo wanunuzi wazuri wa "ze udakuzi"

  Redio zipo nyingi..........kinachokufanya ututukanie redio zetu ni nini.....??? .......we si ubaki kusikiliza malenga wetu huko kwenye redio zako......???

  Taarabu ina wapenzi wengi hapa Dar kuliko unavyodhani .............. NA "WAPENZI IS DAIREKTI PROPOSHENO NA MANEI".... sishangai kuona bongo fleva wanahamia kwenye taarabu.....lakini wa taarabu kwenda bongo fleva sijasikia............??? SI UNAKUMBUKA JIPU LA KWAPA......???

  MTUACHE NA FM ZETU................... PILI PILI YA SHAMBA INAKUWASHIANI........????
   
 13. K

  KIJASHO Member

  #13
  Mar 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulimwenguni kote kwa sasa kuna kitu kinaitwa media commercialization, kweny hii kitu wamiliki wa vyombo vya habari wako zaidi kutafuta faida na ili wapate faida wanaangalia ni kitu gani kinapendwa na wasikilizaji wengi, na kama kitu kinapendwa na wasikilizaji wengi hii inamaana kuwa watapata matangazo mengi ambayo at the end of the day wanapata faida kubwa.

  Sasa radio nyingi kwa sasa kuangukia kwenye mfumo huu wa alamba alamba nadhani wamekwisha establish target audience na wameona kwa saa hizo za mchana wasikilizaji wengi huwa mashangingi.

  Pia media commercialization imefanya karibu radio stations nyingi kuwa na uniformity of the programs, mfano utakuta mda wa usiku radio stations karibu zote huongea kuhusu mapenzi tuuuu, asubuhi karibu radio stations zote zinakuwa na the same programs. Jioni vile vile the same programs. Hivyo tusilaumu kuwa na mashangingi kwenye radio stations bali ni mfumo wa soko la habari ndo unafanya hivyo

  TBC kuingia kwenye mkumbo huu, hii ni mbaya sana maana hiki chombo halitakiwa kufanya biashara lkn chenyewe ndo kimejikita kufanya biashara utafikiri ni commercial media house.
   
 14. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ha ha ha umenikumbusah song ya afande Sele....kwani wanaokaa Oysterbay wakifa hawaozi??? tuache kuwatenga watu kutokana na makazi.........
   
 15. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mkuu thread yako imeonyesha wazi kuwa unachukizwa na uharo wa baadhi ya watangazaji wa kike wa redio hapa nchini.

  Mimi ninachotaka kukukumbusha ni kuwa, sisi binadamu tuko kama vidole vya mkono.
  Hata iweje hatufanani.

  Wewe ukisema ya nini?
  Mwenzio anauliza itarudiwa lini?
  Ili apate kuburudika nayo hiyo mipasho na mirindimo ambayo wewe inakuchefua.

  Kuna mtu mmoja kakushauri hapo juu kwa kukwambia kuwa radio ziko nyingi, so kama unaona vp fungulia TBC international ule ngoma za kinyamwezi unazozitaka wewe ambazo huko mwananyamala na Magomeni hazina maketi.

  Mwisho ningependa uombe radhi kwa mkurugenzi wa TBC Taifa, kwa wasikilizaji woote wa TBC Taifa, kwa watangazaji woote wa TBC Taifa na watuma post kadi woote kwa kuwa umetudhalilisha.

  Naomba pia uchukue fursa hii kuuthibishia umma wa wana jamiiforums kuwa TBC Taifa ina watangazaji wapayukaji kama hao wa FM zako hizo na muda wa matangazo ya huo uharo wao unatakiwa uuanike ili kila mmoja aweze kuusikia.

  TBC tuna kombora
  Nyie mna power breakfast...

  TBC tuna Jambo
  Nyie mna burudani ya Muziki...

  TBC tuna wakati wa kazi
  Nyie sijui mna utumbo gani yailah...

  TBC tuna mchana mwema
  Nyie sijui mna XXL

  TBC tuna malenga wetu
  Nyie bado mna XXL...

  Sasa je ni saa ngapi TBC itatangaza huo upuuzi?

  Na watangazaji wenyewe ndo walewale kina shaaban kisu, malima ndelema, na wazee wengine, sasa hayo mambo ya ''halo ya invisible kuuntu...kuuuuntuuuuuuu uuuh kuntu'' je ni nani wa kuyatangaza?

  Kama unataka kujifunza, kupata habari za uhakika, kuelimika na kuburudika nakushauri kusikiliza TBC taifa.

  Hizo nyingine ni kujipotezea Muda tu coz unaweza ukaisikiliza mwaka mzima na usimjue naibu waziri wako wa kilimo na umwagiliaji ni nani...
   
 16. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kwani katika radio nzima kuna vipindi hivyo mwanzo mwisho? Ukitaka habari subiri muda wake na michezo na vipindi vingine hali kadhalika so ukiona vinakera we switch off tu au hama station bana iache mishangingi ya watu
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  unajua Tanzania ina lundo la wafuata mkumbo wasiojua nini na lini ni hatma yao na ndio maana nchi haina maendeleo.

  Kwa nchi kama hii ambayo bado ina ombaomba waliojipanga kwenye mitaa, ina watu ambao hawana uhakika wa milo mitatu.
  Ina lundo la watu ambao wanakufa kwa magonjwa kama maralia na kuharisha, ina wanafunzi ambao wanakaa chini huku miundo mbinu na vitendea kazi vikiwa finyu, na mlundikano wa watu wasio na ajira mijini.

  ni wazi kuwa nchi hii haitakiwi iwe na vipindi vya kishangingi ktk radio na badala yake kuwe na vipindi vya kijasiliamali na njia za kupambana na maisha ili kila mmoja wenu ajikwamue ktk wimbi hili la umasikini.

  Masikini wa shenz area huwezi kumsaidia kwa kumpa mipasho na maneno ya kipuuzi, huku ukimfundisha mbinu za kumkamata mume wa mtu au kuwa na wanaume wengi ili wamtatulie matatizo yake.

  Huu ni upuuzi uliopevuka, na nimeshangazwa na baadhi ya wana JF kusapoti ushangingi wa watangazaji wasiokuwa na staha na elimu ya utangazaji hata kidogo.

  Kumepambazuka sasa na watanzania mnatakiwa muamke na kufuata ya maana na muachane na yoote ambayo hamna faida nayo.

  Nyie hamtakiwi kukaririshwa mipasho na kuburudishwa na muziki.
  Watanzania mnatakiwa muelimishwe, muelekezwe na kufundishwa mambo mbalimbali yenye manufaa, amkeni na msiwe wapuuzi tena.

  Wakati nyie mnadanganywa na mipasho redioni...kule wao wanachangisha viingilio milangoni ktk tamasha la Maralia na kujinufaisha...
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  thanx........
   
 19. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Wanafundisha nini?
  Hebu andika ni lipi la msingi umejifunza kupitia kwa hao wapayukaji wako?
  Kama unataka kujifunza kitu basi sikiliza TBC taifa au uvizie redio DEUTSCHE WELLE uwasikie watangazaji kama Mohamed Abdurahman, Abdul Mtulya, Josephat Charro, Sekione Kitojo, Home Boy Aboubakar Lyongo, Ramadhan Ally, bi Thelma Mwadzaya, Umil Kheri, Prima Martin, Saumu Mwasimba, na Bi Halima nyanza.

  Hawa nilokuorodheshea kama ubongo wako uko sawa basi nina uhakika ndani ya wiki moja ukifuruliza kuwasikiliza hutotamani tena kusikiliza uharo wa hao mashangingi wako...

  Kumekucha ndugu.
   
 20. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hakuna aliyewashika sheikh, ila tunajaribu kuwaamsha.
  Yaani hata kwa kuwamwagia maji mtaamka tu.

  Ishu ni kuwa hakuna aliyeiponda Taarab na wala hakuna aliyeyaponda magazeti ya Udaku.

  Ishu ninayojaribu kukuelewesha ni je ktk hayo matangazo ya hao mashangingi kuna lipi la maana linalokuingia na kukusaidia kwa siku za usoni?

  kuna mangapi ya muhimu ambayo yakitangazwa ktk FM hizo yanaweza kusaidia kuelimisha jamii ya watanzania fulani ambao wanaishi ktk maisha ya chini na umasikini usioelezeka kirahisi?

  Au we unahisi kuburudishwa huku ukiwa huna uhakika wa karo ya mwanao, huna uhakika na mlo wa kesho, huna income ya uhakika, huna kiasi au hata njia ya kukupatia hicho kiasi ndo utakuwa umepunguziwa matatizo yako?

  Napenda kukukumbusha msemo wa wahenga uliosema...
  Mpe mtu Mbegu
  Ila usimpe Mboga.

  Wakimaanisha ukimpa Mbegu atakwenda kujifunza kupanda na nyingine ataweka kwa ajili ya msimu mwingine wa kupanda.

  Lakini ukimpa Mboga ''atakomba'' yote kisha kesho atakuja kukugongea hodi.

  TBC Taifa wanatupatia watanzania wenye utimamu Mbegu.
  Na hao mashangingi wako wanakupa mboga.
  So tutaonana mwisho wa siku...
   
Loading...