Hii nayo ni Kauli Mbiu ya Shule?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Katika pitapita zangu kitaa siku moja niliibukia mitaa ya Kimanga. Shule ya Msingi (ambapo kimsingi ziko mbili ... Kimanga na Tumaini). Nikakumbana na bango la kwanza ambapo ilinilazimu nipige picha na kuwa na shauku ya kuchek upande wa pili ambako nako nilipiga picha.

Utata wangu ni hilo bango la Kimanga P/School. Kweli takataka si kitu kizuri na tunapaswa kutunza mazingira, lakini je, kweli kauli "Usitupe Takataka Ovyo" inaweza kutumika kama kauli mbiu ya shule?

Nilidodosa kwa baadhi ya wananchi kuhusu performance ya wanafunzi kati ya hizi shule mbili majirani nikaambiwa kwamba: Tumaini ni ya Vipanga, Kimanga ni ya Vilaza.

Wadau tafadhali.

Kauli Mbiu 1.JPG


Kauli Mbiu 2.JPG
 
Back
Top Bottom