Hii Nayo Imekaaje?

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
15,297
11,082
Vyombo vya habari vinavyofanya uchunguzi kupata ruzuku

2007-10-17 15:32:55
Na Job Ndomba, Jijini


Vyombo vya Habari nchini vianatarajia kunufaika na ruzuku kwa ajili ya kuandika habari za uchunguzi na zile za jamii kwa nia ya kuendeleza demokrasia nchini.

Hayo yamesemwa na Mshauri wa Utawala Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Uswisi, Bi. Sara Furrer wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari MAELEZO Jijini Dar es Salaam.

Bi. Sara amesema ruzuku hiyo inatarajiwa kutolewa na Mfuko wa Kuendeleza Vyombo vya Habari, TMF kwa ufadhili wa mashirika mbalimbali ya kimataifa na balozi ambapo mchakato wa kuanzishwa mfuko huo ulianza tangu Oktoba mwaka jana.

Amesema kuwa ruzuku hiyo itaanza kutolewa mwakani baada ya taratibu za awali kukamilika ambapo itawawezesha pia waandishi wa habari kupata fedha za kuwawezesha kutafuta taarifa mbalimbali zinazohusu jamii na maendeleo yake.

Akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo Bi. Sara amesema ni kuendeleza habari za uchunguzi na za kijamii kama njia ya kuhamasisha utawala bora nchini.

`Waandishi wataweza kuomba fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali ili waweze kufanikisha kuandika habari za kijamii ama za uchunguzi,` akasema Bi. Sara.

Akaongeza kuwa wengine watakaonufaika na mfuko huo ni vyama vya waandishi wa habari na vyuo vya uandishi wa habari na kwamba mfuko huo pia unatarajia kuwezesha namna ya kupata vifaa vya uandishi wa habari vikiwemo kamera, vinasa sauti na vinginevyo muhimu.

Aidha, Bi. Sara amesema hivi sasa mfuko huo upo kwenye mchakato wa kutangaza mzabuni, ambaye atapaswa kuwa ni taasisi ya ndani au nje ya nchi.

Akasema taasisi hiyo ndiyo itakayosimamia mfuko kwa miaka mitatu kabla haujaachiwa kujiendesha wenyewe.

Akassema taasisi hiyo itaanza kazi mwezi Januari mwakani.

Aidha, akasema mfuko huo utafadhiliwa kwa pamoja na Shirika la Maendeleo ya Ushirikiano la Uswisi, Idara ya Kimataifa ya Maendeleo ya Uingereza, DFID, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Canada, CIDA na wahisani wengine watakaojitokeza.

SOURCE: Alasiri

Naomba tuijadili kwa kina habari hii, tukitilia maanani vuguvugu la kisiasa lililopo sasa.
 
Back
Top Bottom