Hii Nashidi nimeisikiliza mpaka mwili unasisimka ndugu zangu

Sol de Mayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
6,324
5,934
Zanzibar na Oman ♥♥♥♥♥♥

Katika historia ya Oman si rahisi kuielezea bila kuhusisha uhusiano wake na kisiwa cha Zanzibar na maeneo mengine ya Afrika Mashariki.
Kuna kipindi katika historia Zanzibar ulikuwa mji mkuu wa himaya ya Oman.
Tamaduni nyingi za Oman na Zanzibar zinafanana, kuanzia kwenye upande wa lugha ya kiswahili, chakula, mavazi na mtindo wa majengo yao vilevile yanashabihiana.
 
Huo mnyororo ndiyo hasa unatibua uhusihano...! Mababu zetu waliumizwa na mnyororo! Kibaya hao waliotumia mnyororo huo kuwaumiza babu zetu wala hawajaomba radhi na kutubu dhambi hii. Kwenye suala la imani twaweza kuzungumza kwa jicho lingine.
 
Ewe galatia unaongea madudu gani, yani waombe radhi/msamaha kwa kitu ambacho hawajafanya! Unaweza kuleta ushahidi wowote hata wa picha tu?
 
Ewe galatia unaongea madudu gani, yani waombe radhi/msamaha kwa kitu ambacho hawajafanya! Unaweza kuleta ushahidi wowote hata wa picha tu?
Mbona unakuwa 'provocked' kirahisi! Ibua hoja ya kutetea uhusiano unaozungumzwa kwenye Clip. Clip si maneno tu yanayoimbwa bali na mandhari inayoonyeshwa inakuwa na ujumbe mahususi. Nimeuona mnyororo kwenye clip hiyo ndipo sasa nikaibuka na hoja ya maumivu kutokana na myororo huo.

Sasa ni wakati wako kutoa changamoto unayoiona kwenye hoja yangu kisha kupendekeza lililo bora ili nijifunze kitu kutoka kwako. Katika mapendekezo unaweza kuweka majibu ya kudhibitisha nilichokiandika juu ya maumivu na mnyororo ni makosa.

Karibu.
 
Mbona unakuwa 'provocked' kirahisi! Ibua hoja ya kutetea uhusiano unaozungumzwa kwenye Clip. Clip si maneno tu yanayoimbwa bali na mandhari inayoonyeshwa inakuwa na ujumbe mahususi. Nimeuona mnyororo kwenye clip hiyo ndipo sasa nikaibuka na hoja ya maumivu kutokana na myororo huo.

Sasa ni wakati wako kutoa changamoto unayoiona kwenye hoja yangu kisha kupendekeza lililo bora ili nijifunze kitu kutoka kwako.

Karibu.

Akili na fikra yako yoote imelenga kwenye utumwa bila hata kuuliza maana ya huo mnyororo.

Huo mnyororo hauna mahusiano yoyote na utumwa,,

Sitaki maneno mengi, lete ushahidi hapa hata wa picha tu! Usipoleta tafadhali usiniquote!
 
Mkuu kuna maelfu na maelfu ya watu wanafuatilia mjadala huu hapa JF. Sasa kama unajibu hoja niliyotoa kwa staili hii unakuwa unapunguza radha ya hoja zako.

Mfano, unaandika kuwa "Huo mnyororo hauna mahusiano yoyote na utumwa,," Sentensi hii inatakiwa ikamilishwe kwa wewe kuleta udhibitisho usio tiliwa shaka juu ya uhalali wake. Hivyo, Mkuu, shusha 'nondo zinazoeleweka' kuipa uhai hoja yako. Si mimi ninayetakiwa kuleta ushahidi wa kutetea hoja yako.

Karibu tena.
 
Huo mnyororo ndiyo hasa unatibua uhusihano...! Mababu zetu waliumizwa na mnyororo! Kibaya hao waliotumia mnyororo huo kuwaumiza babu zetu wala hawajaomba radhi na kutubu dhambi hii. Kwenye suala la imani twaweza kuzungumza kwa jicho lingine.

Acha kuongea usichokijuwa, Oman na zanzibar wana mahusiano ya karibu sana. Hiyo Qaswida inaashiria uhusiano wetu na waomani ulivyo imara, na sio hicho unachohoji wewe.

Kwaheri.
 
Umechanganya, ni hapa kwetu mabinti wanateswa na kuuliwa, na isitoshe mshahara wanapewa mdogo. Upo hapo!
wahapa tunaona wahalifu wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Ila watesaji wa uko kwenu arabuni atuoni wakichukuliwa atua?
 
wahapa tunaona wahalifu wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Ila watesaji wa uko kwenu arabuni atuoni wakichukuliwa atua?

Umejuaje kama hawachukuliwi hatua? Wewe unafikiri bongo huko.

Na kama kweli wanateswa mbona wanaendelea kufanya kazi na wengine wanaenda kila day, kwanini wasikate mguu!

Chuki zenu, na ndio maana hamsongi mbele.
 
wahapa tunaona wahalifu wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Ila watesaji wa uko kwenu arabuni atuoni wakichukuliwa atua?

Swala la kutesa mabinti ni duniani kote, hapa bongo ndio usiseme mabinti hunyanyaswa na kuuliwa kabisa, hilo mbona hulisemi tena hiyo ni murder case maana umekusudia kuuwa lkn end of the day mtuhumiwa yuko mtaani anakula life, Uarabuni sheria inafuatwa awe mhindi, mfilipini, mwafrika au bangali.

Tatizo lenu mtu mweupe akifanya jambo linakuzwa hususani waarabu, ila sisi kwa sisi jambo linapotokea tunalipotezea na wala hatulisemi. Hii sio fair kabisa.
 
Back
Top Bottom